Ringo Edmund
JF-Expert Member
- May 10, 2010
- 4,879
- 1,134
Kwa mara nyingine sekretarieti ya CCM ikiongozwa na Kinana na Nape imejigeuza kinyonga kwa kutoa maagizo kwa serikali yao wenyewe kwenye mikutano ya hadhara na vyombo vya habari ili kuwazuga wananchi wa Mtwara.
CCM ikijenga barabara hata kwa kiwango cha chini wanajinadi kuwa ni mafanikio ya serikali ya CCM,wakichimba kisima hata cha milioni 2 kwa bilioni moja utasikia ni mafanikio ya ilani ya serikali ya CCM inayoongozwa na mwenyekiti wa CCM rais Jakaya Kikwete.
Sasa kwenye hili la Mtwara wanadai wananchi wa Mtwara wana hoja na wasikilizwe.Sasa kama si ukinyonga huohuo ni nini?.
Kwa nini wasiseme serikali ya CCM inyoongozwa na mwenyekti wa CCM rais Jakaya Kikwete iwasikilize wana Mtwara?
Je mkeo ukinunua gari na kukupongeza kitandani lakini ukifanya kosa anachukua kipaza sauti na kusimama dirishani na kutangazia majirani ubaya wa mume huyu anafaa kuitwa mke?
Na ni kwa nini kama wana busara ya kutosha miaka 36 ya kuzaliwa ccm isifanyike mtwara ili kuleta mshikamano na kurudisha amani mtwara.
Au wanasubiri damu imwagike Mtwara ndipo waje kulaumu watu wasio na dola wala mamlaka ya kuwasikiliza wana Mtwara?
Au Nape na Kinana wanamaanisha upinzani ndio wawasikilize wana Mtwara?
Naombeni ufafanuzi kutoka huko mliko utaliini gombe.