Kinana: Magufuli kuisafisha CCM na Serikali

Kinana: Magufuli kuisafisha CCM na Serikali

Mzee wa Usafi

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2008
Posts
645
Reaction score
294
Leo ndo mnakiri haya.....alikuwa wapi kusafisha chama kama katibu mkuu?


====

Moshi. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, amesema ndani ya CCM wapo watu wa hovyo, wezi na wanafiki, lakini kama watamchagua Dk John Magufuli kuwa rais, ataisafisha CCM na Serikali yake. “CCM tumejitahidi kuleta maendeleo, lakini lazima nikiri ndani ya CCM kuna kasoro. Tuna mijitu hovyo, tuna wezi, tuna majambazi humo na kuna watu wanafiki ndani ya CCM,” alisema Kinana.

Kinana alitoa kauli hiyo jana mjini Moshi katika mkutano mkubwa wa hadhara wa kuzindua kampeni za ubunge katika Jimbo hilo, ambapo Davis Mosha anapeperusha bendera ya CCM.

“Magufuli atakisafisha chama akiwa mwenyekiti... si mjumbe, lakini anakijua chama.... CCM kuna majungu na ulaji, lakini Magufuli atayamaliza, hajatumia fedha kupata urais, hajaenda wilayani ama mikoani bali alienda matawini.

“Hana makundi... wapo waliochangisha fedha wamekusanya watu baadaye wanakuja kuwa mzigo. Yeye hana makundi wala hana mzigo,” alisema Kinana.

Alisema kuna watu wamefanya uozo ndani ya Serikali na ndani ya CCM na kuamua kukimbia na huko waliko wanasema wataleta mabadiliko wakati wameshindwa kufanya lolote wakiwa madarakani.

Kinana alitoa mfano wa Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye ambaye amekuwa Waziri Mkuu miaka kumi, ameshindwa kufanya kitu na kwamba sasa anakuja kuahidi maajabu.

Hata hivyo katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wanachama wa CCM na wananchi, Kinana aliwaomba wamchague Dk Magufuli kwani ndiye anayeweza kubadili mfumo huo.

“Suala hapa ni mfumo. Mkipata mtu mmoja tu mzalendo kama Dk Magufuli atabadili kabisa mfumo huu. Nataka niwahakikishie kuwa Magufuli akiingia madarakani atasafisha CCM na Serikali,”alisema.

Kinana aliwataka Watanzania kutohadaika na ahadi za mabadiliko zinazotolewa na wale aliowaita “makapi” kutoka CCM ambao walishiriki kuharibu mfumo mzuri wa CCM na sasa wamekimbia.

“Halafu watu walioharibu CCM, hawa makapi hawa wanakuja Chadema, wanawapa matumaini na wengine walikuwa mawaziri kwa miaka 40 kwanini hawakufanya hayo wanayoyasema?” Alihoji Kinana.

Kinana alisema endapo wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro na nchi kwa ujumla, watampa kura Magufuli, ataunda baraza dogo la mawaziri lenye tija na litakalowajibika kwa wananchi.

Katibu mkuu huyo aliwatahadharisha Watanzania kufanya mabadiliko kwa chuki na hasira akiwataka warejee mifano ya nchi za Libya, Misri na Zambia ambapo mabadiliko hayajawasaidia sana.

Alitumia mkutano huo kumshambulia Waziri Mkuu mstaafu, Sumaye, akisema katika miaka 10 aliyokuwa madarakani kama Waziri Mkuu, hakuna kitu Watanzania wanachomkumbuka nacho.

“Sumaye amekuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 niambieni kitu kimoja tu mnachomkumbuka nacho. Sokoine (Edward) mbona anakumbukwa kwa uchapakazi na ukali katika kuendesha Serikali?” Alihoji.

Kinana alisema endapo Sumaye atapanda jukwaani mjini Moshi, wananchi wamuulize maswali 100 kwamba chini ya utawala wake amefanya nini hadi leo amuombee mtu kuwa rais.

Kwa upande wao, mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka na Livingstone Lusinde wa Mtera, waliwataka wananchi wa Jimbo la Moshi kutochagua viongozi kwa ushabiki wa kisiasa.

Akizungumza katika mkutano huo Sendeka alisema ni lazima Watanzania wawapime wagombea kwa kujua ukweli si kwa kudanganyana na amewaasa kuepuka dhambi ya ubaguzi wa aina yoyote ile.

Kwa upande wake Lusinde alisema siasa zisigeuzwe kama ushabiki wa mpira kwani ni kucheza na maisha ya mamilioni ya Watanzania.

“Leo hii Askofu akibadili dini na kuwa Muislamu anaweza kukabidhiwa nafasi ya kuwa Mufti?” Alihoji Lusinde na kujibiwa “hapana” na wana-CCM walioshiriki mkutano huo katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi.
 
Duuuh kama kayasema hayo kinywani mwake,kweli ccm wamefikwa.
 
Karopoka sawa na kujifunga goli wakati mnacheza mpira wa miguu.
 
Tangu Rais Magufuli aingie madarakani na hatimaye kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama cha mapinduzin (CCM), yapata miaka miwili na ushee, ameweka rekodi mpya ya kupaisha chama hicho kwa asilimia 85%.

Katika utafiti wangu nilioufanya kwa miaka miwili Rais Magufuli, uliegemea katika aina tofauti ya makundi ya wanachama, makada, wakereketwa na wananchi wasikuwa wanachama wa vyama vya siasa.

nimekuwa nikitumia simu ya kiganjani pamoja na mitandao minginer ya kijamii katika zoezi hili la kujua "watu wanaisemaje CCM" tangu ujiuo wa Rais Magufuli?

Nilibahatika kuwafikia karibu watu laki nne. Maswali yangu yalijikita kwenye maeneo makuu yafuatayo:-

Mchango wa JPM kama mwenyekiti wa CCM katika kuimarisha chama hicho hatimaye na kukubalika katika jamii. pili matokeo ya wasomi na wa vijiweni kwa jinsi gani wanaikubali CCM baada ya yjio wa JPM.

Tatu, makundi ya wanawake wazee bila bila kujali itikadi zao wanaizungumziaje CCM ya Magufuli. Nne, makada wabobezi/watiifu na wanachama wa kawaida wanaupokeleaje uongozi wa Mwenyekiti wa CCM tangu achukue nafasi hiyo.

Tano na ya mwisho wananchi wa kawaida, wapenzi na wakereketwa wanausemaje uongozi wa Mwenyekiti mpya wa CCM.

Pamoja na kutofautiana kwa majibu kutoka kwa wachangiajin lakini, kwa ujumla asilimia 85% walisema wanamkubali mwenyekiti wa CCM, JPM.

Walisema uwepo wake umechangia kwa kwa kiasi kikubwa CCM kuongeza ushawishi na kukubalika mbele ya jamii, itakumbukwa kwamba kabla ya uteuzi rasmi ndani ya chama, kugombea na baadaye kushinda nafasi ya Urais na baadaye kuwa mwenyekiti wa CCM, chama hicho kilikuwa kikielekea kufikia hatua zilizofikiwa na vyama vingine vilivyowahi kukaa madarakani muda mrefu barani Afrika husani KANU (Kenya) UNIP(Zambia nk.

Kama sio ubunifu wa kina Abrulrahma Kinana kusoma alama za nyakati, kwamaba chimbuka la TANU/CCM ilianzia vijijini hakika kwa sasa CCM ingekuwa "inaisoma namba".

JPM amekuwa msema kweli mara zote amekua akihubiri ukweli mbiu isemayo "Msema kweli mpennzi wa Mungu, utafiti umeonyesha mchango mkubwa wa JPM kwa chama chake umezingatia maajabu yafuatao, leo hii ukitembea magerezani utawakuta watu ambao walikuwa hawagusiki pamoja na jinai mbalimbali walizokuwa wailifanyia taifa hili. wengine kesi zao nzinaendelea kuunguruma magerezani jamboa ambalo halikupata kutokea katika tawala zilizopita isipokuwa wakati wa baba wa Taifa tu, Mwl Nyerere.

JPM ameweka historia mpya barani Afrika ya kuwa Rais wa kwanza atakayeingia katika vitabu vya historia ya kutokwenda nje kwenda kutembeza bakula la kuomba misaada, hususani kwa mataifa tajiri ya ulaya, marekani na uarabuni.

Amejizolea umaarufu kwa kutumia rasilimali za nchi kwa kuendesha shughuli za serikali, pia amezidi kukubalika kisiasa kwa kuwashikisha adabu matajiri kutoka nje (wawekezaji) ambao tangu enzi za kikoloni walikuwa wakitumia mbinu chafu chafu kuihujumu rasilimali zetu kwa kuwatumia wachache wasio waaminifu na kuwekeana mikataba mibovu.

Amethubutu kurudisha imani kwa jamii dhidi ya seriakali yao kwa kuwaadabisha watumishi hewa na serikali na taasisi za umma wasiokuwa waaminifu na waliobobea katika kutoa lugha chafu kwa jamii inayohitaji huduma kutoka kwao.

Amepunguza dhana ya kuwa miongoni mwa marais wapya, ombaomba ambao baada ya kuapishwa tu hukimbilia nje kwa mabebari kuomba misaada ili nchi zao zipate misaada kama ilivyozoeleka katika nchi nyingi za Afrika.

kimsingi hayo ni baadhi ya mambo ambayo Rais Magufuli, amekiongezea chama cha mapinduzi kunufaika na mchango wake kwa asilimia 85%

kiukweli kama Rais Magufuli na CCM yake wataendelea na mchakamchaka huu siyo siri vyama vya upinzani vitakufa kifo cha mende kabla hata ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
 
Sasa tangu lini kitu kikafa mara mbili, vyma vya upinzani vilishakufa, ndio maana havina ajenda sahz vinatafita kick na kutoka kutoka kwa njia ya matukio, mfano kama s makinikia na ofsi za imma kuungua lisu angeongea nini? Hivo hiyo ni dalili tayar kua vililshakufa zamani sana...
 
Sasa tangu lini kitu kikafa mara mbili, vyma vya upinzani vilishakufa, ndio maana havina ajenda sahz vinatafita kick na kutoka kutoka kwa njia ya matukio, mfano kama s makinikia na ofsi za imma kuungua lisu angeongea nini? Hivo hiyo ni dalili tayar kua vililshakufa zamani sana...
Mpuzzz

Ova
 
Nikisoma habari juu ya Mh. Magufuli inanipa furaha kwa kweli na ninatoa tabasamu zuri pia. Tangu akiwa waziri na sasa ni Raisi wetu..

Magufuli oyeeee
 
TUTAWAKATA NGEBE KWA JINA LA YESU 2020


Swissme
 
Nategemea Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi atakubali Time.yake.iwe guru na haki halafu tuone kama kweli CCM imepaishwa au imedondoshwa.

Kwa sababu CCM inategemea polisi na Tume ya uchaguzi na Tume ya Vyama vya siasa ndiyo sababu INA kelele Nyingi.

Hakuna kuikaripia CCM kwa inachokifanya sababu waliopewa madaraka waoga,wanatetea matumbo yao .Tanzania ikipata Mahakama,Tume ya Uchaguzi kama ya Kenya kwa 10% tu CCM chali
 
Back
Top Bottom