security guard
JF-Expert Member
- Sep 27, 2011
- 799
- 603
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Ndugu Idd Ame wakati wa mapokezi katika mkoa wa Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Costansia Buhiye mara baada ya kuwasili Nyakanazi mkoani Kagera ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake ya siku 10 katika mkoa wa Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na wakazi wa Nyakanazi mkoani Kagera.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwa amembeba mtoto Aloyce Atukuzwe wakati wa kusalimia wananchi wa Nyakanazi mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyakanazi waliojitokeza kumpokea ambapo anategemewa kuwa na ziara ya siku 10 mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana amewasili katika Kijiji cha Nyakanazi wilayani Biharamulo Mkoani Kagera ambapo amepata mapokezi makubwa kijijini hapo ambapo mamia ya Wananchi walijitokeza katika uwanja wa shule ya msingi Nyakanazi.
Katibu Mkuu aliwahutubia wananchi na kuwaeleza lengo la ziara yake kuwa ni kuhimiza hatua za utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2010 - 2015, kukagua uimara wa Chama pamoja na kuhimiza wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura na kuwaandaa wanachama wa CCM na watendaji katika kuelekea uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka huu.
Pia, Katibu Mkuu amefanya mazungumzo na uongozi na wanachama wa chama cha wafugaji Mkoa wa Kagera, ambapo wamemueleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika shughuli zao za ufugaji ambapo wamedai kuwa hifadhi ya pori na askari wa wanyamapori wanawatesa na kuwanyanyasa. Katibu Mkuu anaendelea na Kikao hicho aitaka Serikali kurudisha mifugo iliyokamatwa kwa wananchi na kisha yafanyike mazungumzo baina ya Serikali na Wafugaji hao ili kupata suluhu ya kudumu ya tatizo la malisho na maji kwa wanyama na wafugaji na baada ya hapo ataelekea Biharamulo na kisha wilayani Bukoba tayari kuanza ziara yake ya siku 28 Mkoani Kagera, Geita na Mwanza.