KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana, amemtumia salamu Rais wa Malawi, Joyce Banda kwa kumwambia Tanzania haitishwi na haiko tayari kuingia katika vita ya kugombania mpaka wa Ziwa Nyasa. Alisema Watanzania wana mambo mengi ya msingi ya kuyashughulikia ikiwamo kusambaza huduma za maendeleo vijijini na si kuingia vitani kama anavyotaka Rais Banda.
Akihutubia mamia ya wananchi wa Kata za Lupingu wilayani Ludewa juzi, baada ya kutembelea mwambao mwa Ziwa Nyasa na kujionea shughuli za kiuchumi, alisema hatua ya vitisho vinavyotolewa hivi sasa havina nafasi badala yake Tanzania inaamini katika majadiliano zaidi kuliko kuingia vitani.
Alisema pamoja na kulitumikia Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kwa nafasi ya Kanali anajua kila aina ya hadaha na mapambano lakini si kuingia vitani.
Ni wazi nimetembelea ukanda huu wa mwambao wa Ziwa Nyasa na hata kujionea namna mnavyofanya shughuli zetu za kiuchumi, lakini kutokana na vitisho vinavyofanywa na yule mama wa Malawi ya kutaka watu kutoelewana si sahihi hata kidogo.
Pamoja na kusambazwa kwa ujumbe mbalimbali wa vitisho dhidi yenu, hali inayowafanya muishi kwa shaka, ninachotaka kuwahakikishia laleni na mfanye shughuli zenu bila tatizo na kubwa Serikali yenu imejipanga kwa kila hali.
Suala la vita ni maneno ya kitoto, ila kinachotakiwa kwenu kama Taifa ni kuweza kutumia fedha zetu kwa ajili ya shughuli za maendeleo kwa watu wetu na si vinginevyo kama huyo mama anavyotaka.
Moja kati ya mambo yanayoendelea ni suala la mazungumzo ambayo yanaendelea vizuri. Serikali itakuwa ikitoa taarifa kila hatua ambayo itakuwa imefikiwa katika mazungumzo hayo yanayoendelea, alisema Kinana.