TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Ni katika muendelezo wa Kampeni funga kazi ambapo Katibu Mkuu wa CCM Comrade Abdulrahman Kinana ameendelea na ziara yake katika Mikoa kumi ambapo jana na leo ni zamu ya Mkoa wa Mbeya na majimbo yake.
Akiwa katika ubora wake, Kinana amehutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika Viwanja vya shule ya msingi Tunduma na kuwaeleza wananchi wa Tunduma kuwa Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dr John Pombe Magufuli ana uwezo mkubwa wa kuibadilisha Tannzania, kubadili mfumo wa chama na atakuwa na Baraza dogo la Mawaziri, atapunguza matumizi yasiyo ya lazima Serikalini na pia ataondoa kodi ndogo ndogo zinazowapa kero wananchi na kurahisisha njia za kufanya biashra kwa wananchi wa mipakani.
Pia Kinana amewasisitizia wananchi wa Mbeya kuwa sifa ya kwanza kuu ya Kiongozi bora ni UADILIFU, sifa ambayo katika wagombea wote wa Urais, ni Dr John Pombe Magufuli pekee ndie aliyekidhi sifa hiyo.
Kinana akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa mji wa Tunduma kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Tunduma.
Wananchi wa Mbeya wakishangilia...
Vijana wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mkutano huo wa Mzee Kinana.