Bishanga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2008
- 15,323
- 10,063
Kijana wangu wa karibu kaniomba ushauri.Yeye anaishi Dar na kapata mpenzi anayeishi na kufanya kazi Mtwara. Anasema anampenda sana na Inshallah wakijaliwa angependa amuoe.Tatizo nii hii distance relationship,anasema inaelekea kuna mtu kamtonya mdada kuwa jamaa ni kiwembe,hivyo masaa 24 binti roho juu juu,akiandika sms zikipita dakika tano haijajibiwa roho hiyo inakuwa juu juu,usiku jamaa asipompa g nite mapema ndo kabisa dada haamini kama hali ni shwari,mradi tu full mastress binti wa watu.Nauli ya kwenda Mtwara kila weekend jamaa uwezo hana,barabara ya Mtwara ndo hivo kipande cha Ikwiriri_ Somanga kibovu kweli kweli.Kinamama you are the ones who knows a woman's heart,naomba mnipe tip kijana nimshauri nini,afanye nini kumtuliza la'aziz wake ili roho iache kumwenda mbio? Kijana amenihakikishia kuwa ame reform mambo ya ukware hataki tena. Natanguliza shukran.