Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,093
- 22,805
Habarini.
kwa muda mrefu nimekuwa nikichunguza mwenendo wa mabadiliko ya gharama za vifurushi. Kwa maana ya internet bundles.
Nimekuja kugundua kuwa bundle haziliki kwasababu hii mitandao wanatuibia, bali zinaisha kwasababu ya mabadiliko ya teknolojia ya utengenezaji wa simu hizi janja yaani Smartphones.
Kwa wastani, simu ya zamani kwa GB 1 ulikuwa unaweza toboa nayo hata wiki mbili smartphone za kisasa kutoboa 1GB siku nzima ni mtihani. Sasa katika upembuzi nimegundua yafuatayo.
1. Mitandao ya kijamii yenye addiction ya hali ya juu imezidi kuongezeka. Kuna Instagram, TikTok, Facebook, Twitter, Clubhouse, telegram, WhatsApp, YouTube, etc . Hii ni michache ila kuna zaidi.
Mitandao hii inafanya kuongezeka kwa matumizi ya data mara dufu na hii hutokana na upgrades za hizo apps kupitia updates za mara kwa mara ambazo huleta features za kisasa zinazohitaji data zaidi.
2. Apps nyingi huwa zinafanya data collection. YES , majority ya hizi apps ni spy bugs zinazoturekodi na kukusanya mafile ya taarifa na kutuma katika servers huko kwa wenyew. Hili swala kwa nchi zetu za dunia ya tatu sio issue sana sababu less of us pay attention to that ila majority don't sababu wana uelewa mdogo sana kuhusu madhara yake na hivyo haiwatishi.
Hii mada ilishakuwa gumzo sana South Africa hapo baada ya watumiaji wa Sim aina ya Tecno, Infinix, itel kureport juu ya hilo swala. Ukusanyaji huu wa Data hupelekea gharama za ziada kwa watumiaji wakati zinatuma file kimya kimya.
3. Quality za video, audio na images zinabadilika kwa kuongezeka ubora ukilinganisha na za zamani. Imagine kuna sim inatoa video kwa quality kubwa sana kupitia camera zake. Ukitumiwa hizi files zinakuwa katika standard ya juu sana na kuzidownload inagharimu pia. Au ukienda YouTube utaona video nyingi zimewekwa quality ya juu ingawa unaweza adjust quality iwe simple.
Hii ina sababishwa na maboresho ya quality za camera,mic,speakers na Vioo vya simu kama ilivyo kwa devices nyingine kama camcorders,laptops, monitors screens, television sets, etc.
4. Apps nyingi za sasa ni background active yaani unapoiwasha simu wakati wenzako wana interact huko yenyewe inakukusanyia data ili unapoifungua upate history mkusanyiko wa taarifa za yaliyojiri ukiwa offline au mbali na simu. Hii inafanya consumption ya data kuwa unstoppable. Ni sawa na gari ambayo imepaki ila AC inawaka mafuta yataendelea kuchomeka tu.
5. Kubadilika kwa mawimbi na nguvu ya internet kutoka 3G kuja 4G na sasa 5G. Hii inamaanisha the more speed the more mafuta kusapoti kasi. Hivyo basi the more tunachange mawimbi haya ya mtandao the more consumption ya data inaongezeka na kula bundle nyingi.
Therefore, hadi hapo unaweza kuona kuna mabadiliko makubwa sana yanaendelea hivi sasa wakati sisi bado tukitumia bundle zile zile za tokea mwaka 2012. Hii ni kama kwenda dukani kununua mchele kilo 1 ila idadi ya wageni inaongezeka kila uchao, then tuanze kumlaumu muuza duka kuwa anatuibia mchele kwa kupunja na kupima kidogo badala ya sisi kujitathimini mabadiliko katika matumizi yetu.
Ukitazama sim tulizo nazo kwa sasa ni za kisasa sana na ni advanced.
Therefore, nadhani ni muda muafaka wa makampuni ya simu kuwekeza katika teknolojia ya tofauti kama fiber ambayo inasaidia sana upande wa gharama ili internet isiwe inauzwa kama Anasa wakati ni necessity kwa sasa.
Wadau pia ni vema tukaanza mijadala ya wazi ili tutazame namna ya kuiagiza serikali kupitia mamlaka yake itazame namna mpya ya kusaidia na sekta binafsi ili tuweze kubadili bundles za simu na kuziupgrade ziendane na nyakati na teknolojia.
Nilikuwa najiuliza why majuu ni mwendo wa wi-fi na unlimited packages 24/7 now naelewa kuwa ni kwasababu wanafanya urahisi kwa raia wao kupata access nzuri ya internet kuweza kutumia bila shida.
Kwa sasa kwenye simu ya wastani hizi za android kuanzia 8 kwenda juu unahitajika kuwa na wastani wa not less than 5 Gb kwa siku ili uweze kubrowse kwa kujiachia yaani apps zote utumie kwa raha zako. So 5GB mara siku 30 ni sawa na total ya 150Gb kwa mwezi.
Hebu jaribu kutafuta hizo Gb kwa bundle za sasa utalipia bei gani. Halafu kwa bei hiyo tazama gharama za WiFi internet unlimited bundles ni bei gani kisha tujadili nini kifanyike na kushare mawazo.