Kinachosababisha Albinisim

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,834
Nime kuwa nikijifunza kwa mda kidogo mambo ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na nimeona niweke jukwaani sababu hasa za mtu kuwa na ulemavu wa ngozi.
Ulemavu wa ngozi huathiri mataifa yote: Weusi, Weupe, Waasia- kila taifa lina watu ambao wana ulemavu wa ngozi.
Ulemavu wa ngozi hutokana na mtu kurithi kutoka kwa wazazi wote wawili wakiwa wamebeba vinasaba vya ulemavu wa ngozi.
Mtu akiwa na ulemavu wa ngozi hukosa langi ya asili ya ngozi yake inayoitwa melanin. Na ikitokea hivyo ngozi ya mtu huyo huwa nyeupe.

Kwahiyo wazazi wote wawili lazima wawe na vinasaba vya ulemavu wa ngozi.

Ukitaka maelezo zaidi unaweza kwenda kwenye NGO inayoitwa UNDER THE SAME SUN ipo mikocheni B kwa Warioba Dar es Salaam. watakupatia maelezo mazuri. Maana ni vigumu kuandika kila kitu hapa.
 
Back
Top Bottom