Kinachomponza Lowassa

Kinachomponza Lowassa

Robethn

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2015
Posts
2,103
Reaction score
354
KINACHOMPONZA LOWASSA:

Nimejaribu kufatilia kwa umakini kampeni za wagombea wa nafasi ya urais, hasa wa Magufuli na Lowassa, nimebaiini mambo kadhaa yanayompoza Ndugu Lowassa. Tatizo kubwa la huyu jamaa ni kutoa ahadi ambazo hazina tija na pia utaekelezaji wake ni mgumu (yeye mwenyewe anashindwa kufafanua utekelezaji wake).

Ahadi kama kumtoa Babu Seya, kuwatoa magaidi na kumleta Balal (hizi hazina tija kwa wananchi), ahadi za kuondoa umasikini, elimu buree, kufufua viwanda n.k. amekuwa akizitoa kila anapofanya mkutano bila kueleza mipango au mikakati yake itakavyokuwa! Baadhi ya wananchi wanahisi kama kiongozi huyu amekremua kusema hayo!

Lowassa, wananchi wanahitaji mikakati na si ahadi hewa, ahadi unazotoa bado hujaweza tushawishi maana hata mtoto mdogo wa darasa la pili anaweza ongea unayoongea!!
 
rais anaahidi kama anatoa command kwa ummaa mfano mtwara anawambia mmenielewa wakasema hapana!!!!!!! akaendelea kuahidi
 
Si heri huyu anayesema atafufua viwanda na mengineyo kuliko anayerudia matapishi?ashindwe miaka kumi then Leo aweze?ndoto hizo.peopleeeees tuamke
 
Mbona sisi Wapumbavu,Malofa,Kunguni na Mbumbumbu tunamwelewa!!Na ndio chaguo letu piga ua!!
 
Mlitaka asemeje? Lowassa ndiyo tiba kwa maisha magumu ya Watanzania.
 
Kuna jamaa alikuwa anapiga push ups Karagwe,amesahau anaomba kura ya kuwa Rais.Ama anadhani urais ni kama kuwa Baunsa wa Twaweza?
 
Hivi Lowassa ana kipi kipya cha kuwa rais wa TZ, mbona hana sifa za kuwa rais?
 
Kweli kabisa, Rais aliyeuliwa Na Wa-Libya........ hapana, Saddam Rais wa Kuwait.

saddam675.jpg


Ahadi zisizotekelezeka. Madini makubwa makubwa huyu mzee tatizo anaugwonjwa wa kusahau atasahiv kasha sahau kuwa anagombea urais
 
Kinachowaponza ccm ni kutumia muda mwingi kutukana. Hiyo ndiyo tija kwa ccm.
 
Mzee tamaa inamsumbua huyo, aendelee kujifariji.
 
Kituko kikubwa zaidi kiko kwa mgombea wa CCM ambaye ana waahidi wananchi kuanzisha mahakama ya kuwafunga mafisadi wakati karibu CCM wote ni mafisadi na ndio wanaompigia kampeni,sijui akiwafunga atabaki na nani kwenye chama.

Anawaahidi kufufua viwanda vilivyokufa lakini anashindwa kueleze kuwa kama viwanda vilikuwepo ni nani aliviuwa kama siyo CCM wenyewe walioko madarakani.

Anawaahidi watanzania elimu ya bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha 4 lakini ana shindwa kuwaeleza watanzania kuwa utawala wa CCM ndio uliokuwa unazunguka nchi nzima kupinga kuwa elimu bure haiwezekani CHADEMA walipokuja na elimu ya bure katika ilani yao ya mwaka 2010.

Anawaahidi watanzania kuwa utawala wake utakuwa ni wakidikteta lakini ana shindwa kuwaeleza watanzania athari watakazo zipata kutokana na utawala wake wa kidikteta.

Ana waahidi watanzania kuwa atapambana na madaktari na wa uguzi wanaoiba madawa ya hosptali lakini ana shindwa kuwaeleza wananchi ni kitu gani kinachomfanya asipambane nao sasa hivi wakati uwezo huo anao kwa kuwa ni kiongozi katika serekali hiyohiyo inayoshindwa kuwachukulia wahalifu hatua.

Ni heri kumwamini kichaa aliyetoroka chini ya ulinzi wa askari mgambo wa milembe kuliko kumwamini Magufuli na CCM yake.
 
Ikiwa wenye PHD wa chama chako hawajamwelewa wewe utamwelewaje wakati hata cheti cha darasa la saba huna?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom