Kinachomharibia Lowassa ni imani yake nyepesi

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,307
6,514
Kama wanasiasa wangekuwa wanapimwa kwa uzani, Waziri Mkuu wa kwanza katika Serikali ya Awamu ya Nne, Edward Ngoyai Lowassa, angetamkwa bila shaka kuwa mwanasiasa wa uzani wa juu (the heavy weight politician).

Sifa zake ni nyingi katika siasa za Tanzania, alikuwa mgombea urais aliyetajwa zaidi mwaka jana wakati wa Uchaguzi Mkuu 2015. Alitikisa kwenye kilichokuwa chama chake (CCM), kisha akawa kinara wa upinzani, alipohamia Chadema, alikopewa tiketi ya kugombea urais.

Lowassa ndiye mwanasiasa nyota katika siasa za kipindi chote cha Uchaguzi Mkuu 2015 lakini hakufanikiwa kuingia Ikulu. Ni mwanasiasa aliyejenga matumaini makubwa ya kushinda na watu wengi waliamini hivyo lakini alishindwa na Rais John Magufuli, aliyegombea urais kwa tiketi ya CCM.

Safari ya Lowassa na mkwamo wake wa kuingia Ikulu mwaka jana, iliharibiwa na imani yake nyepesi. Hata sasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020, imani hiyo ndiyo inakwenda kumharibia.

Lowassa anaamini kushinda kutokana na nguvu anazokuwa nazo. Anachokosea ni kushindwa kuyawaza matokeo kutokana na nguvu ya anayeshindana naye.

Usiwaze kushinda kwa sababu unajiona unaweza kupambana, bali jenga matarajio kwa kupima uwezo wako ukilinganisha na mshindani wako. Je, ana nguvu kiasi gani ukijilinganisha naye?

Baada ya kuhama CCM mwaka jana na kujiunga na Chadema, jinsi kampeni zake alivyoziendesha, aliamini CCM wanahaha kumzuia, kwamba yeye ndiye mwenye nguvu, alisahau kuwa yeye ndiye alipaswa kupambana na CCM kwa nguvu nyingi.

Kama Lowassa angeamini anashindana na chama chenye nguvu, vilevile mgombea wake, Dk Magufuli alikuwa anauzika kirahisi kwa wapigakura, angejikita vizuri kimapambano kutafuta ushindi. Aliamini CCM na Magufuli walikuwa wakishindana naye, siyo yeye kushindana na CCM pamoja na Magufuli.

Imani ya Lowassa CCM

Kuelekea Julai mwaka jana wakati wa mchakato wa kuteua jina la mgombea urais wa CCM, wasiwasi ulikuwa mkubwa kwamba Lowassa angekatwa. Uvumi ulikuwepo hata kabla ya dirisha la uchukuaji fomu kwenye chama halijafunguliwa.

Muda wote, kabla hajachukua fomu na hata baada ya kutangaza nia yake kwa kishindo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, Mei 30, mwaka jana, kila alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kukatwa, Lowassa alijibu hakuna mtu aliyekuwa na uwezo wa kumkata jina.

Majibu ya Lowassa yalitokana na nguvu kubwa ya kimtandao aliyokuwa nayo. Ni kweli alikuwa na watu wengi, aliamini mtandao wake ulikuwa na nguvu kuliko mamlaka za chama.

Lowassa aliamini kuwa viongozi wa CCM walikuwa wanatishwa na mtandao mkubwa alioutengeneza na uliokuwa ukimtii. Wapo wanasiasa wakubwa kabisa waliokuwa wakimuunga mkono. Uwepo wao ulimfanya Lowassa ajione tishio.

Zipo nyakati alionywa na mamlaka za chama kuhusu tamthiliya za watu waliokuwa wakimfuata nyumbani kumuomba agombee urais. Mashehe, wachungaji, maaskofu, wanafunzi na watu wa taasisi mbalimbali walimiminika nyumbani kwa Lowassa kumuomba agombee urais.

Lowassa alipoambiwa kuwa hiyo ilikuwa ni michezo ya kuigiza aliyokuwa anafanya, alijibu: “Siwezi kuzuia mafuriko kwa mikono.” Na kweli yalikuwa mafuriko. Watu walimfuata na na michango ya fedha za kumwezesha kuchukua fomu.

Baada ya kuchukua fomu, aliitikisa nchi alipokuwa anazunguka kutafuta wadhamini. Angani helikopta na ndege zilipasua anga, ardhini mabasi na magari mengi ya kifahari yalitengeneza misafara. Nguvu ambayo Lowassa aliitumia kutafuta tiketi ya CCM, ilizidi ile ya kuusaka urais alipopewa tiketi na Chadema.

Imani hiyo nyepesi, iliwafanya watu wengi waamini kuwa viongozi ndani ya CCM hawakuwa na uwezo wa kumkata Lowassa. Mbwembwe zilikuwa nyingi. Kwa macho rahisi, ilionekana tayari Lowassa alikuwa mgombea urais wa CCM na alisubiri wakati ufike apigiwe kura kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Yapo maneno yalikuwa yakitamkwa na yalisikika, kwamba aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais mstaafu, Dk Jakaya Kikwete alikuwa hamtaki Lowassa lakini hakuwa na nguvu za kumzuia, maana hata mtangulizi wake, Benjamin Mkapa, naye hakumtaka Kikwete lakini alizidiwa na nguvu ya mtandao.

Lowassa alikuwa na imani nyepesi ya kubebwa na mtandao wake pamoja na ushawishi aliokuwa nao ambao kwa hakika haukuwa haba. Alichokosea ni kutoifikiria sawasawa nguvu ya JK kama mwenye mamlaka yote ya chama na uwezo wake wa kudhibiti mpasuko baada ya kumkata.

Kwa vile alikuwa ameshajua kikwazo ni JK, angeweza pia kuitathmini nguvu yake. Alipaswa kuitafuta tiketi ya chama kwa kumzunguka JK. Isingekuwa vibaya kujifanya mtiifu kwake ili kufanikisha malengo kwenye chama. Huo siyo unafiki wa kisiasa bali ni mbinu za kuutetea ushindi.

Ni kuutetea ushindi kwa sababu kimazingira Lowassa alikuwa ameshashinda tiketi ya kuwa mgombea urais wa CCM. Kilichofanywa na Kamati ya Maadili ya CCM Dodoma, Julai, mwaka jana, ilikuwa kumnyang’anya Lowassa ushindi wake.

Lowassa alionesha viongozi wa CCM hawakuwa na nguvu ya kumkata. Vitendo alivyovionesha vilibeba tafsiri kuwa aliwadharau viongozi wake kwenye chama. Kwa kawaida mtu anapoona unamdharau, hufanya juu chini kukulazimisha umheshimu. Ndicho ambacho Lowassa alikutana nacho.

Imani ya Lowassa Chadema

Lowassa alipojiunga Chadema, aliamini kuwa angeshinda kwa urahisi. Katika kampeni zake, alisema: “Nipigieni kura nyingi hata CCM wakiiba, zibaki za kuniwezesha kutangazwa mshindi.”

Alidanganywa na nani kuwa alikuwa anakubalika kiasi hicho kwamba angepigiwa kura za mafuriko mpaka CCM washindwe kumuibia? Aliamini maandamano na wingi wa watu kwenye mikutano. Alisahau kuwa alikuwa anapambana na CCM, chama kikongwe, kilichozoea kushiriki uchaguzi na kushinda.

Lowassa alitakiwa kufahamu kuwa kuna kushindana kwenye uchaguzi dhidi ya chama, vilevile kushindana na chama tawala. Ukweli huu alitakiwa kuuzingatia kisha angebadili maneno yake. Nchi za Afrika, vyama tawala hushindwa kwa mshangao wa kushtukiza.

Matamshi ya Lowassa yalikuwa yanawaandaa CCM kujizatiti kwa ushindi, hata kama kweli angepigiwa kura nyingi za mafuriko, maneno yalishtua na kuwafanya wajipange hasa kimapambano.

Lowassa aliwahi pia kusema: “Nipigieni kura, kuhusu tume itamtangaza nani hilo niachieni mimi.” Lowassa aliyasema hayo akifahamu sheria zimekaa vibaya, Rais ndiye anayeteua viongozi wote wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).

Ni baada ya maneno hayo, ikashuhudiwa baadhi ya viongozi wa Nec wanabadilishwa, wengine wakipangiwa majukumu mapya kisha sura mpya zikaingizwa. Matokeo yalipotoka, Lowassa alipata kura asilimia 40, Rais Magufuli asilimia 58. Baada ya hapo Lowassa alilalamika kuibiwa kura.

Lowassa aliharibiwa na imani yake nyepesi kuwa angeweza kuishinda CCM kwa urahisi kama alivyokuwa anatamka. Na kwa kawaida ukitarajia ushindi kirahisi maana yake unakuwa unamdharau mpinzani wako. Kumdharau mpinzani mkubwa kama CCM ni imani nyepesi ambayo ilimharibia Lowassa.

Imani ya Lowassa 2020

Hivi karibuni Lowassa alitangaza kutabiriwa ushindi wa urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2020. Alimtaja mtabiri kuwa ni kiongozi wa Kanisa la Synagogue, Church Of All Nations (Scoan), Temitope Balogun Joshua ‘TB Joshua’, anayeongoza huduma ya TB Joshua Ministries.

Kwa jinsi alivyotangaza ni wazi Lowassa anaamini kweli atamshinda Rais Magufuli kama watagombea wote. Ikumbukwe pia iliwahi kuzungumzwa kuwa TB Joshua alimtabiria Lowassa ushindi mwaka jana na haikuwa. TB Joshua alimtabiria pia ushindi Hillary Clinton wa Democrats kwenye uchaguzi wa Marekani mwaka huu na akashindwa na Donald Trump wa Republican.

Lowassa anasema anaendelea kutengeneza mtandao wa chama chake (Chadema) kwa ajili ya ushindi. Sipingi kwamba Lowassa anaweza kushinda urais kwenye uchaguzi ujao lakini haiwezi kuwa kirahisi kama anavyosema.

Yapo mambo ya kutazama. Katiba ni hii iliyopo, Rais ndiye mteua mwenyekiti, makamu wake, mkurugenzi wa uchaguzi na makamishna wa tume. Watu hao kwa kulipa fadhila, kama wanaona zipo njia za kumsaidia Rais aliyepo madarakani hawatasita kuzitumia.

Ni juzi tu Rais Magufuli alimteua Jaji Semistocles Kaijage kuwa Mwenyekiti wa Nec. Mungu akipenda ni Kaijage ndiye atasimamia uchaguzi kisha kutangaza matokeo kati ya Lowassa, Magufuli na wengine watakaojitokeza.

Imani ya ushindi lazima iwepo kwa mshindani wa kweli lakini siyo kuamini kushinda kirahisi kama ambavyo Lowassa amekuwa akiamini. Anatakiwa kubadilika na kuuona mchakato kwa ugumu wake kisha ajiandae kikamilifu kumkabili mpinzani mgumu na mwenye nguvu kuliko yeye.

CHANZO:MAANDISHI GENIUS
 
Mimi nakubaliana kabisa na wewe. Lowassa huwa anatabia ya kufikiri kuwa watu wote wanamoyo kama wa kwake.
_ si waongo
_ si wezi na watenda haki
_ si wanafiki kuwa wanachokwambia ndio ukweli wenyewe
_ kila anaekuja kwake ni wake hata muacha
_ wanaurafiki wa kudumu
_ watamsikiliza kwa lolote atakalosema
Kitu ambacho binadamu ni tofauti na hayo yote na anahitaji mikakati kumthibiti

_
 
Jiulize ni kwa nini kule marekani wananchi wengi walimchagua Clinton lkn hakupewa uongozi, ndicho kilimtokea Lowassa,
 
Kinachomuharibia lowassa ni hiki.
OTH_7406_1.jpg
edo3.jpg

Anapigwa saundi kirahisi halafu anatoa hela.
 
wewe mbona kila siku Lowasa?

hebu achana na huyu kipenzi cha watu,

hamumuwezi hata nafsi yako inashuhudia hilo

leo kesho mwatamani arudi ccm
 
Jiulize ni kwa nini kule marekani wananchi wengi walimchagua Clinton lkn hakupewa uongozi, ndicho kilimtokea Lowassa,
Rudia kusoma kuhusu uchaguzi wa marekani kisha utofautishe kati ya electoral vote na popular vote. Kisha uelewe mshindi anapatikanaje.
 
wewe mbona kila siku Lowasa?

hebu achana na huyu kipenzi cha watu,

hamumuwezi hata nafsi yako inashuhudia hilo

leo kesho mwatamani arudi ccm
Una uwezo finyu sana wa kuchanganua masuala.....

Jitahidi kusoma makala za siasa zitakusaidia.....maana najua vitabu huwezi.
 
Me nahisi bila katiba mpya kuwaondao hawa maccm ni ndoto na ni ukweli usiopingika Tanzania hatutapiga maendeleo yeyote kw hali hii ya kuongoza nchi kibabe na kutishiana yaani rais akisema kitu ata kama ni porojo hakuna wa kumshauri wala wa kuhoji ni upumbavu mtupu ni lazima ifikie hatua tujitambue na kuwa na demokrasia ya kweli na sio mwenye nguvu ndo kila kitu na watoto wa masikini tutabaki kuwa masikini mana serikali yetu hakuna mkakati wa kumkwamua watu wa chini
 
Ccm wana akili sana baada ya kuona maji yapo shingoni wakachagua mtu anayetoka kabila kubwa vingine ccm ingekuwa chama cha upinzani muda huu, Mwanza, Shy, Kangera, Simiyu na Mara ni ngome ya Cdm.
 
Back
Top Bottom