Katika hali inayoendelea ya mwenendo wa siasa zetu hapa Tanzania, unaweza ukajiuliza masuala mengi bila majibu. Kutokana na mtiririko wa matukio ya Zanzibar walau kwa kuangalia chaguzi zetu kuu, nguvu inayotumika, malalamiko na migogoro unapata picha moja kuu kwa upande hasa wa Zanzibar. Chama tawala CCM kimeelemewa.
Hebu chukulia mfano wa Kuanzia uchaguzi wa 1995,2000 na huu wa 2015 malalamiko yalivyojitokeza kutoka UPANDE WA CCM. Yaani CCM kinalalamikia upinzani kuwafanyia rafu na kuwaibia kura kweli? Uchaguzi wa 2000 Baada ya CCM kushindwa walifuta matokeo ya majimbo sita ya Mjini magharibi Unguja hali ilioyopelekea CUF kususia na mwishowe CCM kujitwalia ushindi. Kama kawaida 2015 tena, siku tatu baada ya uchaguzi na CCM kushindwa walifuta uchaguzi wote na sio majimbo au maeneo yenye utata kama walivyotaka kutuaminisha. Mpaka leo hakuna ushahidi wowote.
Nimetanguliza maelezo hayo ili watu waelewe kuwa siasa zetu zina mashaka na walakini. CCM ukweli wanaujuwa kuwa wameshakataliwa Zanzibar tena kwa muda mrefu. Ukweli huu hauwezi kufichwa kwa kutumia bunduki, mazombi, au hadaa za kura za maruhani. Mara ngapi watawala na dola imetumika kulinda maslahi ya CCM Zanzibar? nani asiyejuwa figisu hizo. Nina imani iko siku jiwe litaongea pale waliotumika watakapofichua siri.
Licha ya jitihada za watawala kuficha ukweli, hii ya 2015 imekuwa kali sana na yumkini jumuiya ya kimataifa imengamua janja ya CCM kuhusu Zanzibar. Tunaambiwa sasa CCM imeunda Kamati Maalum kuchunguza kwa kina. Sawa iwe iwavyo kama wanatafuta waliosaliti kama wenyewe wanavyosema sawa au kama kuna lengine sawa. Bado kuna watu watabebeshwa mzigo wa kushindwa kwa CCM Zanzibar, lakini itakuwa wanaweaonea bure, Ni imani yangu viongozi wote wakuu na wastaafu wanajuwa kuwa CCM haiuziki Zanzibar na kutaka kuwahukumu wengine ni kujitoa fahamu kuliko wazi.
Wengi wa waanzibari, wameshaikataa CCM tokea uchaguzi wa awali wa vyama vingi wa 1995, wakati ule mazingira ya kisiasa na Diplomasia yaliwasaidia kufanya walichokifanya kuweza kuishi. CCM walisahau kitu kimoja kwamba Katiba ilishafanyiwa marekebisho na kutambuwa uwepo wa GNU na walisahau kwamba hii ilikuja kutokana na jitihada za dunia kuchoshwa na mgogoro wa Zanzibar. Hapa walisahau. UNDP kama taasisi ya kimataifa ilitumia rasilimali nyingi kuwezesha na kuondowa mianya ya malalamiko katika chaguzi lakini kwa mazoweya CCM wakasahau na mwisho wakaja kulalamika eti CUF imewaibia na kuwafanyia fojari kule Pemba, Lakini cha ajabu ni wao pekee walioona hayo matatatizo na vyama vyengine vyote pamoja na waangalizi iwe hawakuona maajabu...'
CCM watafute dawa ya kukataliwa kwao Zanzibar na ningewashauri wawe tayari hasa kukabiliana kupata ushawishi na kuungwa mkono. CCM wanakijuwa wanachotaka Wazanzibari, kiu yao wanaijuwa tatizo CCM hufungwa na sera zao AMBAZO ZINAKATALIWA ZANZIBAR.
Kwa mtiririko huo ni wazi, Kinachoendelea kuitesa CCM kwa Zanzibar ni kivuli chake mbele ya Wazanzibari na hilo wanalijuwa. Kutafuta sababu nyengine na kubereuza mambo hakusaidii
CCM ibadilike kweli ili kuepusha mazingaombwe yanayojitokeza kila baada ya MUDA NA KUINGIZA NCHI KATIKA SINTOFAHAMU.
Ni imani yangu safu mpya ya CCM itaelewa ukweli huu na kuja na njia mbadala za kukijenga CCM upya hasa Zanzibar. Ushauri wa bure. CCM ijikite kujuwa nini wazanzibari wanataka na kuja na majibu, vile vile wakumbuke kuwa vitisho, ghilba, ubabe vimeshindwa kuifanya CCM ipendwe.
"Yanayosemwa yapo kama hayapo hwenda yakaja"
Asubuhi njema
Kishada