Kinachoendelea Mashariki ya Kati, Dunia ndio ya kulaumiwa

Fredwash

JF-Expert Member
Oct 27, 2009
1,041
1,375
1620987558122.png

Hivi kweli watawala wa dunia (Europe and Arab League) kwa miongo zaid ya hamsin wameshindwa kutafuta suluhu ya hili tatizo. Najua kuwa kuna maudhui ya kidini na kiasili kwenye mgogoro huu lakini mbona kuna migogoro mingi yenye maudhui kama hayo kwingine na mambo yalizungumzwa yakaisha hadi Inchi zikagawanywa. Je, huku Mashariki ya Kati kunashindikana nini.

Ukiangalia Expansion ya Israel toka miaka ya arobain huko utaona kuwa aidha ni kwa makusudi ama kupuuzia kwa Watawala wa Dunia kwenye hili. Wake up call ilitakiwa iwe ile vita ya siku sita kati ya myahud na Arab Nations. Hivi kwa nini kusingekuwa na makubaliano ya kuigawanya kimipaka huu ukanda. Paleatina na jews wakaishi kila mtu kivyake hata kama hawatak kushirikiana..

Pia meneo ambayo yana utata wa urithi wa kidini kama vile Jerusalem, basi yawekwe chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa (UN) tena ifanywe kama ni urithi wa Dunia, kama tunavyoona Pyramids au Ngorongoro kiundwe chombo maalum kinachojumuisha pande mbili plus wajumbe neutral kutoka kwingine.

Hayo maeneo yawe urithi wa dunia watu wanaenda kutalii kwa mujibu wa iman yako, kama ilivyo sasa maana sasa hv jerusalem na telaviv waislam wanaenda wayahud wanaenda , wakristo wanaenda. Mapato yakipatikana pasu kwa pasu na kama kuna maboresho yanaongelewa pande zote mbili.

Lakini naamini kuna mengi ambayo wakubwa hawa hawasemi, kuanzia Israel kwenyewe hadi hao Hamas pamoja na Europe na Arab League Elites ( Iran + Saudia na wengineo). Ni kweli kuwa Israel at some point waliwahi kui fund Hamas, na pengine hata sasa bado wanaifund hii ni worldwide ni politic game inatumika to take control au kufaidika na vitu flan, kwa wakat flan, kuna allegations ya Marekani kufadhili vikundi vya kipiganaji na hata Africa kuna allegations kama hizo mfano Rwanda na Congo.

Ila kwa haya ya Mashariki ya Kati we only knows half of the story and its the story hao wakubwa wa Dunia wanayotaka tuijue. Jiulize hicho unachookiita palestina sasa angalia hapo chini ilivyokuw zaman had sasa na hao wakubwa wa Dunia kuanzia Europe had Arab League walikuwepo lakini Palestina inazidi kutetereka. Unaweza ukashangaa inaachajwe hii itokee ndo utajua there is more to this than what know.

Rejea pia vita ya siku sita kati ya Israel na Arab League ikiongozwa na Misri na matokeo yake. Sipend na sifurahii kinachoendelea huko bila kujali nani mwenye haki. Wanazuoni wanakwambia 'War does not bring lasting peace Only lasting death and it doesn't determine who is right only who is the last man standing'.

Ukisema Israel kamzidi Palestina maana ameua 30 Palestina kaua wawili tu nenda kawapongeze ndugu wa hao Israel wawili waliokufa kuwa wameshinda maana wao wamekufa wawili tu ndo utajua vita haina mshindi wa kweli. Aand the so called nobel prize winners ambao ndo world runners wanaishia kuongea kinafiki ila nyuma ya pazia wana make money

Asikwambie mtu kuzaliwa na kuishi Mashariki ya Kati ni zaid ya vita

Mtu akaangalie Series ya FAUDA ya Wayahud ndo utaona maisha ya kila siku ya Palestina na Uyahudi yakoje
 
Back
Top Bottom