Kinachoendelea kule Afrika Kusini na duniani kote

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
4,573
9,809
Kuna misukumo yenye kuto kukamatika, yaani "unleashed drives" ambayo viongozi na watawala duniani kote hushindwa kukabiliana nayo. Hofu kubwa kwao ikiwa ni kutotaka kuwaudhi vijana ambao ndio mtaji mkubwa wa kisiasa wa kura ktk nyakati za uchaguzi. Wanasiasa wakiyatambua makundi ya vijana wenye ushabiki na chama chao, hata kama wanajihusisha na matendo ya jinai, wao huyanyamazia kimya tu kana kwamba hakuna jambo la ukiukwaji wa sheria ambalo limefanyika kiasi kwamba kutambulika kuwa linadhuru haki za msingi za watu wengine (mifano ni mingi na wala hakuna haja ya kuelezea).

Kile kinachoendelea kule SA kuhusiana na "Xenophobia" ni muendelezo wa mambo kama hayo. Wanasiasa hawana majibu ktk changamoto halisi zenye kuwakabili vjjana, tena hili ni tatizo la kidunia, na wala sio kwa SA, TZ ama Afrika tu.Tupo sote kwenye dimbwi la mkwamo wa kiuchumi, kiutamaduni, kijamii na kila nyanja ya maisha.

Pengine ni vyema kwa sasa tukatambua vyanzo halisi vya chuki dhidi ya wageni, ama ya wenyewe kwa wenyewe, ili angalau tupate fununu za kuanzia ktk kutaka kutafuta ufumbuzi wa muda ama kwa kuanzia kuelekea kwenye ufumbuzi wa kudumu.

Kupitia ktk kazi za kifasihi za watu tofauti ktk shule za mawazo, nimeweza kutambua michango yao kwa ujumla ambayo ingegawanyika ktk sehemu kubwa tano. Kwa leo ningependa kuainisha vyanzo hivyo kama ifuatavyo:

Chanzo cha kwanza ni tofauti za kiuchumi kati ya wenye nacho na wale wasiokuwa nacho. Hapa ndipo huzalishwa chuki ktk kugombania fursa za kiuchumi.

Chanzo cha pili kinatokana na mazingira ya historia, ambapo ndani yake kuna mambo yenye kuambatana na vijana kukosa uvumilivu ktk "social, culture and racial phenomena" Kile walicholichwa na kuingia akilini ndicho ambacho uamini kuwa ni ukweli usiotia shaka yoyote ile kwao.

Chanzo kingine ambacho nimekitambua, kinatokana na chuki za kidini na kiimani. Chanzo hiki ni kama ilivyokuwa ktk kilichotangulia hapo juu. Vijana hulishwa kasumba ambazo ndani yake wanafungwa na "limits"za kuweza kufanya udadisi na kutambua kuwa wameathiriwa na utumwa wa fikra za kurithi.

Chanzo kingine ni anguko kubwa la kimaadili, ambalo limeleta misukumo mpya ya "life styles" ambazo hata UN imelazimika kupitisha maazimio ya aibu na kuyaridhia. Eti kumaanisha utu ni kwa kutambua haki za jamii za LGBT, haya ni mambo ambayo hata Ibilisi hutucheka pale tuendapo misikitni ama makanisani.

Chanzo cha mwisho sasa, ni kukosekana kwa utawala wa kidunia wenye kuweza kukabiliana na changamoto hizi zote. League of Nations ilishindwa, UN imeshindwa, kwa utaratibu mpya wa kidunia unaitutwa, yaani "New World Orders" Jitihida zimekamiika za kumuuandaa mtu mwenye hadhi ya kuiongoza dunia nzima ili ikapate suluhisho la kudumu kwa changamoto hizi za kidunia, hasa kwa vijana wa sasa.

Hitimisho: Kule ambapo dunia inategemea matokeo chanya ndipo ambapo anguko kuu limesimama. Desiparetly we are seeking for potential benefits without responsibilities. Every effort will be in vain, if our Almighty God can not intervene for our favour and fate, we are perished. Ndiyo! Ni "drive" ya kidunia ambayo inatupeleka ktk anguko kuu, na kila mtu atabakia akimlaumu mwingine. Kila mwenye sikio na alizingatie andiko hili.
 
Back
Top Bottom