Kinachodhoofisha uchaguzi TZ

Kinachodhoofisha uchaguzi TZ

Kagosaki

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2010
Posts
208
Reaction score
57
Leo hii watu dunia inasherehekea ushindi wa Obama na tayali mpinzani wake Romney amekubali matokeo kwamba yeye ameshindwa. Lakini ukiangalia uchaguzi wa wenzetu, haukuwa na vitisho kama hapa kwetu.

Ikifika wakati wa uchaguzi hapa, basi TBC wanaanza kuweka kila documentary za vita (meaning watu wakichagua upinzani watakaribisha vita), Makamanda wa vikosi mbalimbali nao wanaanza kutoa vitisho "Sisi tumejipanga, atakaeleta chokochoko atakiona".

Sasa sisi huku watu wa Ikwiriri na Mpitimbi tukisikia vitisho hivyo tunajificha msituni na kukacha kupiga kura! Kujitokeza kwa watu wengi kupiga kura inawezekana hata hapa kwetu kama mazingira ya uhamasishaji yakiwa mazuri, halafu serikali ikiachana kabisa na vitisho.

Lazima tuige demokrasia ya wenzetu. Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom