Kina mama wanaosafisha barabara

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,824
2,381
Hawa akina mama wanafanya kazi ngumu saana na huenda kwa ujira mdogo pia. Wengi wao ni watu wazima.Kwanza ni nani amewaajiri hawa? Kufanya kazi katika mazingira yale ni hatari saana kwa afya zao, maana muda wote wapo kwenye vumbi. Lakini pia vyombo vya usafiri ni hatarishi kwa maisha yao na lile jua, uwezekano wa kupata kansa ya ngozi unaongezeka.

Swali la kujiuliza, siku hizi kuna magari maalum yanayoweza kufagia barabara kwa ufanisi. Kuna sababu gani kuwatumia watu hawa katika hii kazi? Lakini pia wale ambao si waaminifu hupeleka michanga katika mifereji. Licha ya kwamba watu hawa wanahitaji ajira lakini wanahatarisha mno maisha yao. Watu wa OSHA wanaishia wapi?
 
magari yatabana space,afu hyo pia ni ajira,unataka wawe omba omba? Kikubwa wapewe vifaa safety gears vinavyokidh mazingira yale
 
Usemayo mleta mada ni kweli hata hivyo Umenikumbusha maisha yangu mimi mwenyewe wakati nipo chuo!

Mi bhana mvivu kweli kweli linapokuja suala la kufua! Sasa ikawa kila weekend anakuja jamaa room nampa nguo akanifulie! Sasa kulikuwa na mzee mmoja ambae nae ilikuwa daily lazima aje hostel kuomba vibarua hata kama ni vya kufua soksi! Sasa kv alifahamu kwamba nami ni mtoa tenda za kufua; ikawa kila weekend anawahi kuja kuuliza ikiwa nina nguo chafu! Kwa uchungu mkubwa nikawa namkatalia! Nilikuwa najisikia uchungu kv mara zote nguo nilikuwa nazo lakini kwa upande mwingine nilikuwa najisikia vibaya sana kumtuma mzee kama yule ndo maana nilikuwa namkatalia!

Kadri cku cku zilivyoenda nahisi kama nikaanza kupata ufahamu na kujiuliza "sawa, haipendezi kumtuma mzee kama huyu; lakini je hivi namsaidia chochote kwa kutofanya hivyo?" Nikajua huyu mzee ni shida ndo maana anahangaika hivi; sasa hivi nikijisikia vibaya ndo nitakuwa nimemsaidia chochote?! Ningekuwa na uwezo I believe ningemsaidia in other way round lakini sikuwa na uwezo huo! Hapo hapo nikakata shauri kwamba Mungu nisamehe but from now on huyu ndo atakuwa mfuaji wa nguo zangu!

Kwahiyo ukikuta mtu kaajiri Mzee usimlaumu-- wengi inakuwa ni very hard decision sasa ni wewe umwache ashinde njaa huku akinufaika na huruma yako isiyoweza kununua hata andazi moja au uamue kuchukua uamuzi unaoweza kuonekana wa kibedui lakini angalau unaoweza kumpa japo andazi moja asubuhi! Ni very complicated hadi ukumbane na hiyo scanario!

Hivyo basi, issue hapo iwe mambo mengine kv issue za kiusalama n.k lakini nani anawaajiri; ni very complicated!
 
magari yatabana space,afu hyo pia ni ajira,unataka wawe omba omba? Kikubwa wapewe vifaa safety gears vinavyokidh mazingira yale
Haya magari hufanya kazi usiku wa manane. Huwezi kuiita hii ni ajira wakati inawapunguzia umri wa kuishi. Vipi kuhusu skin cancer?
 
Back
Top Bottom