Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Judith Kappinga, ameongoza akina mama wa Kabila la Wamatengo kumlaki Mwenyekiti wa CCM Taifa na Mgombea Urais, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa njia ya kiutamaduni iliyohusisha wimbo maalum na kugalagala chini kama ishara ya heshima.
Tukio hilo limefanyika leo, Septemba 21, katika mwendelezo wa ziara za kampeni za Rais Samia za kuomba ridhaa ya wananchi na kuinadi Ilani ya CCM 2025–2030 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Tukio hilo limefanyika leo, Septemba 21, katika mwendelezo wa ziara za kampeni za Rais Samia za kuomba ridhaa ya wananchi na kuinadi Ilani ya CCM 2025–2030 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.