Kimya hiki kwa upoteaji wa Ben Saanane, Serikali imeshindwa?

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,685
1,111
Kimya kingi kina mshindo mkuu,serikali ilisema ipewe muda kufuatilia upoteaji wa Ben Rabiu Wasanane,toka waziri mkuu ajibu swali la Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani huko bungeni hatujapata taarifa kuhusiana na uchunguzi zaidi ya kusikia taarifa zisizo rasmi kuwa yale makaburi ya wale maiti walio opolewa mtu Ruvu makaburi yao yamefukuliwa na miili ile kupotea au kutekwa.

Iko wapi intelejensia yetu makini ikiwa imeshindwa kubaini chanzo cha kupotea ndugu huyu ilihali mawasiliano yake ya mwisho yanajulikana aliwasiliana na namba ipi! Ni muda sasa toka kupotea kwake lakini hakuna hata dodoso toka upande wa watu wetu wa uchunguzi angalau tupatiwe taarifa za awali.

Tumekuwa tukisikia jinsi jeshi letu la polisi lilivyo hodari kupambana na waharamia waliofanya mauwaji ya askari wetu huko Kibiti na Mkuranga,lakini mbona hatusikii ufuatiliaji wa Ben. Kama ni marehemu tuelezwe na kama mzima ila yupo kizuizini tujulishwe pia.

Ukimya unaozidi kutawala usitegemee kuwasahaulisha Watanzania ilihali ndugu yetu haonekani,tuna haja ya kujua hatima ya ndugu yetu, kama serikali imeshindwa ni bora kuweka wazi na kukaribisha taasisi zenye uwezo mkubwa kiuchunguzi zifanye kazi hiyo. Kwa ukimya huu si tu kunaibua maneno na maswali mengi kwa wananchi,bali kunawaondolea wananchi imani na serikali yao juu ya suala zima la ulinzi kwa wananchi wake.

Narudia maneno ya baba yake Ben,Ben si mbuzi yangu ni mwanangu,naiomba serikali na CHADEMA inisaidie kumpata mwanangu awe hai au amekufa ,kwa nini serikali inashindwa kusema au kukiri kushindwa kwa vyombo vyake vya uchunguzi na kuomba msaaada kwa mashirika ya kiuchunguzi ili kufuta sintofahamu inayojenga taswira mbaya kwa wananchi dhidi ya serikali yao.

Kupotea kwa hayati Robert Ouko nchini Kenya na hatimaye kupatikana akiwa amekufa na mwili wake kuchomwa moto ili kupoteza ushahidi kuliibua uwazi wa tukio zima kwa serikali ya Kenya kuruhusu shirika la uchunguzi toka nje ya nchi hiyo kufanya uchunguzi,iweje kwetu ionekane mtihani?

Amekufa faru John,uzito kwa kifo chake umegharimu gharama sawa na ujenzi wa barabara kilometa moja kwa kiwango cha lami au mabweni ya chuo kikuu,iweje ishindikane kwa binadamu ambaye ana haki ya kuishi kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano ibara ya 14 . Every person has the right to live and to the protection of his life by the society in accordance with the law.

Serikali imekuwa ikilalamika kuwa kuna makundi ya watu wanao ichonganisha serikali na wananchi wake ili serikali ichukiwe,lakini serikali inashindwa kujua kuwa msingi mkuu wa chuki dhidi yake ni kuacha kusimamia katiba ibara ya 14 .

Tunaitaka serikali kurudi kwenye msingi wake mkuu kwa ustawi wa wananchi bila kuwabagua kwa matabaka ya itikadi,kikanda au kwa namna yoyote kwa kuwa wote tuna haki sawa mbele ya sheria,iwe polisi,Kiongozi au raia wa kawaida.

Nikuombe mh. Mbowe urudie swali siku ya alhamisi,wakati wa maswali ya papo hapo kwa mh. Waziri mkuu juu ya mrejesho wa taarifa za awali za uchunguzi wa kupotea kwa Ben.

##Bring back Ben,si mbuzi yetu ni Mtanzania mwenzetu anayestahili kulindwa kwa mujibu wa katiba ibara ya 14###
 
Serikali imeshindwa kweli? Siamini, yaani kuna wapelelezi wenye uwezo wao lakini kimya!!!. Basi kama tumeshindwa tuombe msaada toka ng'ambo maana wale hawashindwagi kizembe namna hii
 
Ben ni Mtanzania, ni jukumu la Serikali kumtafuta siyo Chama. Elewa tunazungumzia uhai wa mtu, kuwa mstaarabu.
 
Ben ni Mtanzania, ni jukumu la Serikali kumtafuta siyo Chama. Elewa tunazungumzia uhai wa mtu, kuwa mstaarabu.
Mnavyohangaika na rambi rambi za Arusha,ingekuwa mnahangaika na Ben kama hivyo saa hizi tumeshapata mwanga
 
Majaliwa si alisema Apumzike kwa amani, yaani R.I.P sasa wamtafut wapi wakati wanajua wamemtanguliza ahera?! Hizi ndio laana mpka serikali inafikia kula rambirambi kwenye shughuli za kiserikali.
 
Tunapohoji uhalali wa kupotea wananchi bila serikali kushtuka tunaingiwa na uoga wa maisha yetu, tunaogopa kuumizwa lakini kama utaangalia upande wa pili wa shilingi jambo lililompata Ben ama likakupata wewe au ndugu yako ndipo utakapopata ujasiri wa kuhoji,Ben ana haki ya kulindwa na jamii inayomzunguka kwa nini kupotea kwake serikali ikae kimya?
 
Ben ni Mtanzania, ni jukumu la Serikali kumtafuta siyo Chama. Elewa tunazungumzia uhai wa mtu, kuwa mstaarabu.
Na ndio inamtafuta haijakataa, lakini BAWACHA akiwemo MBOWE hatoi ushirikiano - au kuna deadline wamepewa ?
 
Mkaruka said:
Na ndio inamtafuta haijakataa, lakini BAWACHA akiwemo MBOWE hatoi ushirikiano - au kuna deadline wamepewa ?
Mbowe alishamuuliza waziri mkuu,amesema serikali ipewe muda,ipewe muda mpk lini,au mpk itakamaliza muda wake madarakani!
 
Na ndio inamtafuta haijakataa, lakini BAWACHA akiwemo MBOWE hatoi ushirikiano - au kuna deadline wamepewa ?
Hivi BAWACHA & MBOWE wana kitengo kama vile polisi nk. ili waweze kutoa ushirikiano. Ninavyojua taarifa (last calls/messages)iliwakilishwa polisi/sehemu inayohusika. Pia waliwapa polisi namba za simu ambazo Ben alikuwa anapigiwa au kutumiwa messages nk. Lakini mpaka leo polisi hawajatoa jibu, ulitaka ushirikiano gani?
 
Sidhani kama wameshindwa ila wanajua nani sababu ya Ben kutoonekana,na wanshindwa kumtafuta maana wanajua alipo
Kwahiyo huyo aliyemhifadhi hawawezi kumforce amtoe? Au anamapembe? Unajua kinachofanyika hapa ni kubeti tu kuwa huenda yupo kwa Fulani au fulani anahusika. Tusiishi kwa kubahatisha namna hii ni hatari sana, wafikie mahala waweke Vitu wazi hata kwa kutumia nguvu
 
Back
Top Bottom