Kimsingi, Bunge linapaswa kurushwa mubashara

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,278
25,846
Sina nia ya kumkwaza wala kumfurahisha yeyote katika hoja yangu hii. Nia yangu ni kutoa maoni yangu juu ya matangazo mubashara ya Bunge, hasa katika kipindi hiki cha Bajeti. Bajeti, kadiri ya uelewa wangu, huainisha mipango ya Serikali na namna ya kuitekeleza katika kipindi cha mwaka mmoja.

Ndiyo wakati muafaka wa Serikali kujieleza na wananchi kusikia mipango ya Serikali yao. Pia, ni wakati muafaka wa Wabunge kuichambua Bajeti ya kila Wizara na kutoa michango yao ya kuiboresha, kuikosoa na kuijenga Bajeti ya Wizara husika. Katika uga wa kisiasa, ingawa mimi si mwanasiasa, kuonekana na kusikika ni kila kitu.

Mwanasiasa, ninaamini hivyo, ni mtu anayepaswa kuonekana na kusikika kila wakati na kila mara. Kikubwa ni kuonekana na kusikika kwa mema kwa taifa lake;wananchi wake na chama chake. Mwanasiasa asiyeonekana wala kusikika mahali popote hupoteza ladha na hakika hafaidi kabisa uanasiasa wake.

Bunge, kwa tafsiri yangu, ni uwanja rasmi wa kisiasa wa chama tawala na vyama vya upinzani. Ndiko huko, wanasiasa wanakoonyeshana umahiri wa kujenga hoja na kukosoana kwa staha kwa ajili ya Taifa letu. Kimsingi, kusitisha kuonyeshwa mubashara kwa matangazo ya Bunge kumeondoa ari kwa Wabunge na kuwanyong'onyesha wananchi.

Sasa wananchi wanaishia kupata 'vi-clip' vya Wabunge wao mitandaoni na kuyadaka yale tu yaliyo kwenye 'vi-clip' hivyo. Ni kama vile tumerudi enzi za mpira wa Simba na Yanga kutangazwa redioni-tena RTD. Tunahitaji kuwasikia na kuwaona Wabunge na Serikali yetu wanapoucheza mchezo wa kisiasa ulengao maendeleo ya nchi mubashara kabisa.
 
Naunga mkono hoja, zile airtime wanazopewa akina bashite zingehamishiwa mjengoni. Ila sometimes bunge huwa linaboa balaa
 
...sijui nani kawaroga hawa Watawala wetu hadi wanashindwa kuona Umuhimu wa Bunge kwa Wapiga kura.Kama ni pressure ya Matokeo ya Uchaguzi,2015 mbona hali imeshatulia!..tuzidi kuwaombea kwa kweli!
 
Back
Top Bottom