Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,858
Nchi yetu kwa kifupi haina dira na kwasababu haina dira kila siku tumekuwa ni watu wa kupotea njia na matokeo yake tunaenda mbele hatua 10 alafu tunarudi nyuma hatua 20.
Anachokifanya Magufuli leo hakina tofauti na kile kilichokuwa kinafanyika enzi za Kikwete tofauti iliyopo ni style tu ya uwajibishaji na style ya kufikia maamuzi ya kuwajibisha watu.
Enzi za JK mawaziri,makatibu wakuu na watendaji wengine walikuwa wanawajibishwa kwa shinikizo la Bunge lakini hakukuwa na system nzuri ya kuhakikisha watendaji wanawajibika kwa makosa yao na hawapati nafasi tena ya kurudi serikalini.
Leo hii Magufuli hasubiri shinikizo la Bunge kuwajibisha watu na hii ndio tofauti pekee lakini mpaka sasa,kama ilivyokuwa wakati wa Kikwete, hajaweka system ya kuhakikisha ufisadi na wizi serikali unapungua au unakwisha kabisa.
Tunatokaje hapa ni lazima tuzingatie mambo haya.
Katiba ya Mzee Warioba
Mihimili yetu mitatu kwa maana ya Bunge,Serikali na Mahakama haijajengwa katika mfumo ambao kila Mhimili unaweza kufanya kazi yake pasipokuingiliwa wala kuhofia Mhimili mwengine na hii ni kutokana na Katiba inayompa Raisi madaraka makubwa ya kuteua majaji na hata kulivunja Bunge.
Kwa mfano Bunge limekuwa likitoa maazimio mengi tu lakini serikali haitekelezi na Bunge linakuwa halina cha kufanya kwasababu kuna mhimili mmoja umejichimbia chini zaidi.
Madaraka makubwa ya Raisi
Madaraka makubwa ya Raisi ni moja chanzo kikubwa sana cha matatizo katika nchii hii.Raisi anateua karibu kila mtu na hata kumuwajibisha ni kwa hiari yake na sisi kama wananchi tunabaki kuwa wapiga sound tu kama bwana Mwijage ila maamuzi yote ni yake yeye ama Raisi.
Kwa mfano nani leo hii anajua Bashite anafanya nini na si ajabi tusijue mpaka awamu hii imalize muda wake alafu aje Rasi mwingine achukue hatua alafu nae tuanze kumsifia.
Hata maazimio ya Bunge yangekuwa yanafanyiwa kazi na serikali,mtu kama Muhongo na Maswi sidhani hata kama wangepata nafasi ya kuteuliwa na Magufuli kuingia tena serikalini ila kwasabu Bunge halina nguvu na Raisi hana wa kumzuia matokeo yake ndio haya sasa kina Muhongo wamerudishwa serikalini na wameendelea kulea uozo ule ule uliokuwapo kwa miaka mingi.
Usiri wa Mikataba
Bila kuwa na sheria inayotaka mikataba yote kupita Bungeni,madudu haya hayataisha na sitashangaa hata siku jamaa akitoka Madarakani, mrithi wake nae akawa na kazi ya kupitia upya mikataba aliyoingia alafu nae tuanze kumsifia na kumuita Jembe badala ya kuwa na mfumo mzuri wa ku-deal na mambo ya aina hii bila kutegemea utashi wa Raisi aliepo madarakani.
Kiti cha Spika na kanuni za Bunge zinazompa madaraka makubwa spika
Ili Spika aweza kuwajibika ipasavyo, Spika huyu hapaswi kutokana na chama cha siasa kama katiba hii ya sasa inavyoelekeza bali anapaswa kuwa mtu huru na anaewza kusimamia maamuzi ya Bunge bila kujali msimamo wa serikali iliyoko madarakani.
Spika huyu amepewa madaraka makubwa sana na kanuni za Bunge ya kuwez kuamua jambo lolote lile zikiwmo hata hoja binafsi za Wabunge zijadiliwe au zisijadiliwe ndani ya Bunge.
Leo hii hata Mbunge akiamua kuleta hoja binafsi ya kutaka mikataba yote ipite Bungeni Spika anaweza kutumia nafasi yake kwa namna moja au nyingine kuzuia hoja hiyo isiingie Bungeni.
Wabunge kupoteza ubunge iwapo watavuliwa uanachama wa vyama vyao
Sheria hii inawafanya wabunge wawajibike zaidi kwa vyama vyao na serikali yao badala ya kuwajibika kwa wanachi wao na hivyo kushindwa kuibana serikali na Raisi alie madarakani na matokeo yake ni kuchangia Bunge kuwa kibogoyo.
Ukweli ni kwamba bila kuweka mifumo madhubutu ya uwajibikaji maigizo haya hayataishi na kila atakaekuja atatuzuga kwa kufanya hili na lile huku nae akifanya yake kimya kimya au kwa uwazi na hakuna wa kumuuliza na muda wake ukiisha anaondoka na chake hasara inabaki kwetu.
Hata wakati wa Kikwete watu walifukuzwa sana tu ila tunapaswa tujiulize kwakuwa hakukuwa na mifumo mizuri tuli-achieve nini na sasa tunarajia ku-achieve nini ili hali mifumo na taratibu ni zile zile na chama ni kile kile na watu ni wale wale wa kutoka chama kile kile.
Alafu nani ana uhakika mtu akiwa mkali ndio msafi na mzalendo kiasi kwamba hahitaji mifumo ya kumdhibiti?
Magufuli anajitahidi kwa kiasi chake japo ana mapungigu yake lakini akitoka madarakani mmejiuliza anatuachaje?