SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Jimbo la Vunjo lilishuhudia mabadiliko ya mbunge aliyekuwepo Ndg James Mbatia ambaye alikataliwa na wananchi kwa sababu ya kuwatelekeza na kushindwa kuwasemea masuala yao ndani ya bunge.
Uchaguzi huo ulipelekea kupatikana kwa mbunge mwingine ambaye ni msomi, mchumi na mtaalam aliyebobea kwenye masuala ya kifedha Dkt Charles Stephen Kimei ambaye aliiongoza kwa mafanikio makubwa benki ya CRDB kutoka kuwa na tawi moja na kuiacha ikiwa na matawi zaidi ya 250 ndani na nje ya Tanzania kwa pamoja. Rekodi yake bora kwenye utendaji na masuala ya uongozi iliyoakisiwa na mafanikio makubwa kwenye benki ya CRDB na ushiriki wake kwenye maendeleo jimboni Vunjo pamoja na sera au ahadi zake wakati wa kampeni zilikuwa kichocheo cha yeye kuaminiwa na umma wa wananchi wa Vunjo.
Ikiwa ni takribani siku 100 tangu achaguliwe na kula kiapo kuwa Mbunge wa bunge la Tanzania Mhe Dkt Kimei amethibitisha kuwa wanavunjo walifanya chaguo sahihi kwani ametekeleza ahadi zake nyingi ikiwemo ya kusikiliza kero za ardhi, umeme na maji. Kubwa zaidi ni michango yake ndani ya bunge imekuwa ya viwango vya juu kwani imegusa mahitaji ya wananchi wa jimbo la Vunjo.
Siku sio nyingi aliahidi kuanza kuanzisha mfuko wa wajasiriamali au uwezeshaji wananchi ambao unalenga kutoa fursa kwa wanavunjo kujiajiri na kujipatia au kukuza kipato chao.
Hakika ameanza vizuri Mhe Mbunge Dkt Charles KIMEI.View attachment 1708094