Kimei akerwa kukatika umeme bila ratiba maalumu, awatuliza Wananchi anafuatilia

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Kutoka Vunjo

Mbunge wa jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Kimei amepita maeneo mbalimbali ya wafanyabiashara na kukutana na kilio cha kukatika kwa umeme kila siku bila ratiba maalum.

Wafanyabiashara na wajasiriamali wengi wamemueleza hali hiyo inawaathiri sana kwani shughuli zao zinategemea nishati hiyo ya umeme.

Mhe Dkt Kimei amewaeleza anafahamu hasara inayosababishwa na kukatika huku kwa umeme ambapo alitaja baadhi kama kuharibika kwa vyakula vinavyohifadhiwa kwenye majokofu kama vile samaki wabichi, nyama, mbogamboga, matunda, vinywaji baridi, adha kwa watu kuvaa nguo zilizokunjamana na huduma za afya zinazohitaji umeme kusuasua kama huduma za vipimo maabara.

Vile vile alisema athari nyingine ni kuathirika kwa biashara zinazohitaji umeme kama vile maduka ya nguo na viatu wanakosa wateja sababu ya giza bidhaa hazionekani, uchomeleaji vyuma, viwanda vidogo vya wasagaji nafaka, viwanda vikubwa kama Maji ya Tanza, Himo Tanners pamoja na joto vyumbani kwenye nyumba za makazi na biashara.

"Nafahamu maeneo mengi ya jimbo letu umeme umekuwa unakatika na kurudi karibu kila siku wakati mwingine unachukua muda mrefu kurudi na mbaya zaidi hauna ratiba maalum. Hali hii inaleta usumbufu mkubwa sana. Naomba kuwatoa hofu wananchi wenzangu kwamba hakuna mgao wa umeme. Nimefuatilia na nafuatilia kwa karibu kuhakikisha Tanesco wanashughulikia matatizo yaliyopo kwa haraka ili hali ya upatikanaji wa umeme irejee katika hali ya kawaida. Nawapa pole wote na nawaomba tutulie ndani ya muda mfupi changamoto hii itamalizika kwani awamu ya tano chini ya Rais Magufuli mgawo wa umeme ni msamiati uliosahaulika."

Mwisho, amewaomba wananchi waendelee kuchapakazi katika maeneo yao kwa amani na utulivu. Amewahimiza ofisi ya Mbunge ipo Himo mjini hivyo kwa wale wote wenye changamoto au ushauri wafike ofisini au watumie simu namba yake 0763510049 watahudumiwa.

PAMOJA TUNAWEZA

IMG_20200902_145513_188.jpg
 
...."Nafahamu maeneo mengi ya jimbo letu umeme umekuwa unakatika na kurudi karibu kila siku wakati mwingine unachukua muda mrefu kurudi na mbaya zaidi hauna ratiba maalum. Hali hii inaleta usumbufu mkubwa sana. Naomba kuwatoa hofu wananchi wenzangu kwamba hakuna mgao wa umeme. Nimefuatilia na nafuatilia kwa karibu kuhakikisha Tanesco wanashughulikia matatizo yaliyopo kwa haraka ili hali ya upatikanaji wa umeme irejee katika hali ya kawaida. Nawapa pole wote na nawaomba tutulie ndani ya muda mfupi changamoto hii itamalizika kwani awamu ya tano chini ya Rais Magufuli mgawo wa umeme ni msamiati uliosahaulika'....View attachment 1634331
Kwa hiyo ameshaelewa tatizo linasababishwa na nini, kwanini anakimbilia kutoa ahadi ya utatuzi wa tatizo haraka. Nadhani TANESCO walikuwa hawajabadilisha setting ya mifuno yao ile waliyoiweka wakati Jimbo la Vunjo lipo chini ya upinzani.
 
Back
Top Bottom