Kimbo Slice afariki dunia

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
93,472
119,275
Hivi huu mwaka una nini?

Kafa Antonin Scalia...kafa Phife Dawg...kafa Prince...kafa Muhammad Ali...na leo habari zimekuja eti Kimbo Slice kafariki huko South Florida!

Kwa mujibu wa CNN, Slice alilazwa jana Jumatatu kwenye moja ya hospitali huko Florida.

Kimbo Slice, jina halisi Kevin Ferguson alikuwa ni mpiganaji ngumi kavukavu kabla hajaanza kupigana kwenye MMA.

Umahiri wake wa kuzipiga pamoja na umbo lake na ndevu zake vilimpatia umaarufu mkubwa sana kwa zaidi ya miaka 10.

Mimi binafsi nilijua kuhusu uwepo wake mwaka 2004 kupitia video za kwenye mtandao.

Mpambano wake wa mwisho katika MMA ulikuwa mwezi Februari dhidi ya Dada 5000.

Pumzika kwa amani Kimbo.

Kiranga

King Shaat
 
Tumwache Mungu amchukue anayemtaka maana akisema amrudishe huyo anichukue mie hata sikubali, kila mtu atakufa siku yake ikifika, Kazi ya Mungu haina Makosa
 
image.jpeg
 
Mbona anafanana na yule jamaa wa kwenye movie ya blood and bone..

Sijawahi kuiona hiyo filamu ila inawezekana maana MMA fighters wengi siku hizi wana dabble katika kuigiza filamu.

Labda uangalie majina ya walioshiriki kuigiza hiyo filamu na ukiona kuna Kevin Ferguson basi huenda ndo yeye.
 
Sijawahi kuiona hiyo filamu ila inawezekana maana MMA fighters wengi siku hizi wana dabble katika kuigiza filamu.

Labda uangalie majina ya walioshiriki kuigiza hiyo filamu na ukiona kuna Kevin Ferguson basi huenda ndo yeye.
R.I.P Kimbo...

Nakumbuka umewahi kuitumia picha yake kama profile yako Nkwingwa..

Ni kweli jamaa ameshiriki kwenye Blood and Bones pamoja na Michael Jai White..
 
R.I.P Kimbo Slice

"Took time but my cash got right
If I want it I'm a buy it, I don't ask no price
Rearview mirror, jumbo dice
Trunk hit hard like Kimbo Slice
Feel right tint, no window lights
Car ride smooth so the rims alright
Dat right thurr see see I like"
 
Back
Top Bottom