Kimbembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kimbembe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Apr 17, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Staili ya wanawake wengi nchini kuyatengeneza maumbo yao kwa kutumia dawa za Kichina, imeungwa shubiri na serikali ambayo imetangaza kuwa wote ‘walioshepu figa’ zao hawawezi kupata msaada wa bima ya afya.

  Ijumaa a.k.a the Highest Quality Paper, lina data za kutosha kuhusu tamko kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwamba wanachama wote walioathirika kutokana na kutumia dawa za kuongeza makalio na sehemu nyingine za mwili, hawatogharamiwa.

  Mkuu wa Elimu kwa Umma wa mfuko huo, Rehani Athuman aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akiwasilisha mada kwenye semina ya wapigapicha na wachora katuni kuhusu huduma za NHIF.

  Mbali na waathirika wa dawa za Kichina, Rehani alisema kuwa NHIF pia inawatenga wale wanaopatwa na athari za upasuaji kwa ajili ya kutengeneza shepu zao ili waonekane warembo (cosmetic surgery).

  Meneja Madai wa NHIF, Dk. Aifen Mramba alichambua kwa jumla kwamba mfuko huo haufungamani na maradhi yatokanayo na vitendo vya uvunjaji wa sheria za nchi kama utumiaji wa pombe haramu, ulevi wa kupindukia, utumiaji wa dawa za kulevya na utoaji haramu wa mimba.

  Alichambua nyingine kuwa ni upasuaji wa urembo (cosmetic surgery), athari za mkorogo, dawa za China za kuongeza sehemu za mwili pamoja na tiba za nje ya nchi ambalo ni jukumu la serikali.

  Matumizi za kuongeza viungo, yameshika kasi nchini ambapo wanawake wengi wamekuwa wakiyashughulikia maumbo yao halisi na kuyageuza katika mtindo ambao wanaamini unavutia zaidi.

  Katika moja ya matoleo yake mapema mwaka huu, Ijumaa liliandika kuhusu mwanamke mmoja mkazi wa Tandale, Dar es Salaam ambaye ameathirika na matumizi ya dawa za kuongeza makalio.

  Ndani ya toleo hilo, ilielezwa kuwa mwanamke huyo alianza kutumia dawa za Kichina za kuongeza makalio na hipsi kutokana na kuchekwa na wenzake mitaani kwamba ni kimbaumbau.

  Ijumaa lilieleza kuwa baada ya mwanamke huyo kuchoshwa na kadhia ya kadhia za kusemwa hivyo, aliamua kutumia dawa za Kichina ambazo zilimpa matokeo mabavu kwa kunenepa hovyo na makalio kua makubwa kupitiliza hadi kumpa kero.

  Mbali na huyo, yupo Mtanzania mwingine anayedaiwa kutumia dawa za Kichina kwa lengo la kukuza kiungo chake nyeti lakini matokeo yakawa mabaya baada ya sehemu zake za siri kukua hadi kufikia kilogramu 10.

  Sakata la dawa za Kichina linaendelea zaidi kwa sababu imebainika kwamba warembo wengi maarufu wanatumia dawa za kupunguza au kuongeza kati ya makalio, hipsi na matiti kwa lengo la kuboresha ‘shepu’ zao.

  Mmoja kati ya watumiaji ni mwimbaji wa taarabu anayeshika kasi kwa sasa nchini ambaye yeye anatumia tatu kwa mkupuo, kukuza hipsi, makalio na matiti.

  Mrembo aliyetwaa taji la Miss Tanzania miaka michache iliyopita, naye anadaiwa kutumia dawa za kukuza hipsi kwa kile kinachoelezwa kwamba ni ili zilingane na makalio yake ambayo ni makubwa kiasi. http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/kimbembe-1   

  Attached Files:

Loading...