Mserengeti
Member
- Mar 1, 2007
- 20
- 0
Kimbembe:Mahabusu Dar wazua zali upyaa!
2007-10-02 17:05:12
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Baada ya kutuliza boli kwa muda, mahabusu Jijini Dar es Salaam wameanzisha zali upyaa kwa kutia ngumu kushuka kutoka kwenye karandinda na kwenda kortini.
Kimbembe hicho kimeanza leo asubuhii ambapo mahabusu kutoka gereza la Keko waling`ang`ania kwenye makarandinga yao huku wakifoka kwa kusema, `safari hii hakitaeleweka hadi tupewe haki zetu `.
Licha ya mapolisi kuwalilia wakiwataka washuke na kwenda kortini, waliendelea kukomaa huku wakiwarushia makombora ya tuhuma kibao.
Mahabusu hao ambao huanza kushushwa katika Mahakama ya Mwanzo na ya Wilaya ya Temeke kabla ya kusambazwa kwenye mahakama nyinginezo Jijini, waliwaliza polisi kwa kukataa amri yao ya kuwataka washuke kwenye karandinga ili waende kortini.
Badala yake, mahabusu hao waliokuwa wamejazana tele wakawa wakizomea na kupiga kelele za kila aina.
Kisha kwa umoja wao wakawa wakiimba nyimbo za kukumbushia madai yao ya kutaka watendewe haki kwa kesi zao kusikilizwa na hatimaye waweze kupata dhamana badala ya kuendelea kusota rumande.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililozua zogo la aina yake pale Temeke, ni kwamba mahabusu hao toka Keko walikuwa wakiimba nyimbo za kuilalamikia Serikali juu ya kuahirishwa kwa kesi zao kila kukicha na wakati huohuo, wakawa wakisisitiza kuwa wanataka kuonana na Waziri Mkuu Edward Lowassa, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Mary Nagu na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema.
`Tumechoshwa, tunataaaka?.haki yeetu!` mahabusu hao wakasikika wakiimba kwa jazba huku wengine wakipunga makaratasi yenye ujumbe unaofafanana na huo.
Katika madai yao, mahabusu hao wamekumbushia sababu zilezile zilizowafanya wawahi kugoma mwanzoni mwa mwaka huu, ambazo ni pamoja na kutaka haki ya kusikilizwa fasta-fasta kwa kesi zao ambazo wamedai zimekuwa zikiahirishwa kila mara kwa maelezo kuwa `upelelezi bado haujakamilika`.
`Tunakabiliwa na matatizo kibao huko mahabusu, haki hakuna kabisaaa tunamtaka Waziri Mkuu (Lowassa), Waziri Nagu na IGP Mwema ili tuwaeleze kuwa hakuna kilichofanyika kati ya wale waliyowahi kuahidi,`akasema mmoja wa mahabusu hao aliyekuwa akizungumza kupitia kwenye nondo za karandinga.
Walipoamriwa na polisi kushuka kwenye karandinga, mahabusu hao toka Keko waliendelea na msimamo wao na kudai kuwa hata wakirejeshwa lupango, pia hawatashuka na watang`ang`ania kukaa ndani ya karandinga hadi waonane na viongozi wanaowataka.
Hata hivyo, wakati mahabusu wa Keko wakigoma kutinga kortini leo, wenzao wa magereza ya Ukonga na Segerea walishuka kama kawaida na shughuli za mahakama ziliendelea kama zilivyopangwa.
Wakati wa mgomo kama huo mwanzoni mwa mwaka huu, mahabusu walitoa madai kadhaa, kubwa likiwa ni kusikilizwa haraka kwa kesi zao.
Walichukua hatua hiyo ikiwa ni siku chache tu baada ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Kapteni Mstaafu Ditopile Mzuzuri kuweza kuachiwa kwa dhamana katika kesi yake ya kutuhumiwa kumuua dereva wa daladala.
SOURCE: Alasiri
mwamko sasa umehamia hadi magerezani,i wish wakati wanaimba wangemtajakaramagi na buzwagi