KIMARO: Hakuna wa Kuning'oa Vunjo!

Kiranja

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2007
Messages
754
Likes
4
Points
0

Kiranja

JF-Expert Member
Joined May 19, 2007
754 4 0
na Charles Ndagulla, Moshi

MBUNGE wa Vunjo, Aloyce Kimaro ‘Simba wa Yuda’, ametamba kuwa hadi sasa hajaona mpinzani wa dhati ndani na nje ya chama chake ambaye anaweza kumng’oa kwenye kiti chake cha ubunge kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.

Akizungumza na Tanzania Daima mjini hapa jana, Kimaro alisema wote wanaotajwatajwa kuwa wanajiandaa kugombea jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa vyama vya upinzani hawakubaliki hata kwa wapiga kura.

Miongoni mwa waliotangaza kuwania jimbo hilo ni Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Kabla ya mfumo wa vyama vingi vya siasa Mrema alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM wakati huo likiitwa Moshi Vijijini.

Wengine ni Mkurugenzi wa masuala ya Halmashauri na Bunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mrema, Mwanasheria wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crispin Meela na Dk. Benny Moshi wote kupitia CCM.

Kimaro, mmoja wa wabunge wanaojipambanua kuwa ni makamanda wa vita dhidi ya ufisadi, alidai hata kama watatoa rushwa kwenye mchakato wa kuwania kuteuliwa na chama kugombea ubunge na hata wakiingia kwenye kura za maoni kwa kuhonga hawawezi kumshinda.

Alisema wanaodhani kuwa atashindwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM na kwenye uchaguzi wenyewe, waende wakazungumze na wananchi na ukweli wataupata huko.

“Kwangu ni salama kabisa na hao wanaokwambia kwamba mimi nitashindwa kwenye uchaguzi mkuu wanakudanganya. Kwa kifupi nakwambia hakuna mpinzani kwangu na hata wakitoa rushwa kwenye kura za maoni wataishia huko huko,” alitamba.

Kauli ya Kimaro inatafsiriwa na wengi kama ni kujibu mapigo kutokana na kauli ya hivi karibuni iliyotolewa na Mrema kwamba jimbo la Vunjo ni mali ya TLP katika uchaguzi mkuu ujao na kujipa matumaini ya chama chake kuwa na angalau jimbo hilo moja kwenye uchaguzi huo.

Naye Mrema wa CHADEMA, amepuuza kauli hiyo ya Kimaro na kuiita kama ni ya kutapatapa kwa kile alichodai kuwa mbunge huyo hajatimiza ahadi zake kwa wapiga kura waliomwamini na kumpa ubunge mwaka 2005.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Mrema alidai Kimaro atapimwa na wananchi kwenye uchaguzi huo kwani hivi sasa amegeuka kuwa mtetezi wa watu wenye uwezo na si wananchi waliomchagua.

“Wanaoamua nani awe mbunge wao ni wananchi na Kimaro hawasaidii tena wananchi waliomchagua badala yake amekuwa mtetezi wa matajiri bungeni na kama unataka ushahidi tunao tutakupa,” alisema. Alisema wananchi wanataka kupata taarifa kutoka kwa Kimaro jinsi yalivyotumika mamilioni ya fedha yaliyotolewa na wahisani mbalimbali kwa ajili ya kusaidia benki za kijamii vijijini maarufu kwa jina la VOCOBA. Mrema alisema hadi sasa mradi huo wa VOCOBA hauna maelezo ya kina na jinsi fedha hizo za wahisani zilivyotumika huku akidai kuwa kuna mchezo mchafu umetumika kwenye matumizi ya fedha hizo.

Source: Tanzania Daima.
 

Ngongo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2008
Messages
12,355
Likes
3,936
Points
280

Ngongo

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2008
12,355 3,936 280
Mheshimiwa Kimaro anadanganya watu bahati nzuri mwaka mpya nilibahatika kutembelea maeneo ya Samanga,Marangu mto,Ashira Kilema na Mamba mpaka Mwika.Maeneo yote niliyo tembelea tathimini yangu ilijionyesha wazi Mheshimiwa Kimaro amepoteza uungwaji mkono kwa namna ya kutisha.

Mheshimiwa Kimaro anakabiliwa na kashfa kubwa ya kuwanunua wenyeviti wawili wa chama cha TLP.Mhe Kimaro pia anakabiliwa na tatizo litakalo waondoa wabunge wengi ambao hawatembelei majimbo yao ya uchaguzi mpaka muda wa uchaguzi unapokaribia ndio wanakumbuka kuwatembelea wapiga kura wao.Mheshimiwa Kimaro anajua maji yako shingoni kwani hata ndani ya CCM tayari anakabiliwa na upinzani mkubwa nje ya CCM CHADEMA na TLP wamejichimbia vyema uchaguzi wa wenyeviti wa vijiji ni salama tosha kwa CCM na Mheshimiwa Kimaro.
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Likes
86
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 86 0
na Charles Ndagulla, Moshi

MBUNGE wa Vunjo, Aloyce Kimaro ‘Simba wa Yuda', ametamba kuwa hadi sasa hajaona mpinzani wa dhati ndani na nje ya chama chake ambaye anaweza kumng'oa kwenye kiti chake cha ubunge kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.

Source: Tanzania Daima.
- Kudos! tunataka viongozi wanaojiamini namna hii, ingawa angejitahidi kuweka yale yote aliyoyafanya toka ashike ubunge, otherwise saafi sana kiongozi kuwa na this kind of confidence.

Respect.


FMES
 

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,135
Likes
70
Points
145

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,135 70 145
Aliyoyafanya ni pamoja na haya, soma Hansard ya Bunge.

BUNGE LA TANZANIA
_____________
MAJADILIANO YA BUNGE
_______________
MKUTANO WA KUMI NA SABA
Kikao cha Nne – Tarehe 30 Oktoba, 2009
(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)
D U A
Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua
HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati ifuatayo iliwasilishwa mezani na:-

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE:

Taarifa ya Utekelezaji wa Ahadi za Serikali Bungeni kwa kipindi cha mwaka 2008/2009.


MASWALI NA MAJIBU
Na. 49

Mashamba ya Kahawa yaliyokodishwa kwa
Wawekezaji Mkoani Kilimanjaro
MHE. ALOYCE BENT KIMARO aliuliza:-

Kwa kuwa, katika Mkoa wa Kilimanjaro kuna mashamba makubwa ya kahama yanayosimamiwa na Vyama vya Msingi vya Ushirika lakini mengi yameshakodishwa kwa wawekezaji:-

(a) Je, Serikali inaweza kuyataja mashamba hayo na yameingiza faida ama hasara kiasi gani kwa Taifa?

(b) Kama kuna mashamba yenye utata na hayaleti faida kwa nchi;Serikali haioni kuwa ni vema kuyagawa kwa Watanzania wenye uwezo hasa wakati huu Serikali inapohimiza kilimo?


NAIBU WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA (MHE. MATHAYO D. MATHAYO) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Aloyce Bent Kimaro, Mbunge wa Vunjo, lenye sehemu (a) na (b) kama ifutavyo:-

(a) Mashamba yasiyosimamiwa na Vyama vya Ushirika vya Msingi Mkoani Kilimanjaro ni 41. Kati ya hayo, mashamba 27 yanazalisha kwa tija na faida. Mashamba 14 hayazalishi kwa faida kutokana na mogogoro kati ya wamiliki na waliokodisha, na uzalishaji mdogo wa wakodishaji. Katika mashamba ynayozalisha kwa faida sehemu ya mapato ya ukodishaji wa mashamba hutumika kuimarisha huduma za jamii ikiwemo shule, zahanati, barabara, na kusaidia malipo ya karo za shule kwa watoto wasiojiweza. Aidha, wananchi wanapata ajira katika mashamba hayo. Mazao yanayozalishwa katika mashamba hayo ni, mboga mboga na nafaka. Mazao hayo yanapouzwa huwapatia wakulima na Taifa mapato zikiwemo fedha za kigeni kwa mazao yanayouzwa nje ya nchi kama kahawa, mauwa na mboga mboga. (Makofi)

(b) Mheshimiwa Spika, kutokana na baadhi ya mashamba kuzalisha chini ya uwezo, uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro uliteua kamati maalum ambayo ilifanya tathmini ya mashamba yote 41 na kubaini viwango vya maendeleo ya uwekezaji na kutoa taarifa kwa uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro. Taarifa hiyo iliwasilishwa kwenye uongozi wa mkoa na kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC). RCC kwenye kikao chake cha tarehe 11 Mei 2009, imeushauri uongozi ufanye upya mapitio ya mikataba ya mashamba hayo ili kubaini mapungufu yaliopo na kuchukua hatua zitakazowezesha mashamba hayo yazalishe kwa tija na faida.


Mheshiiwa Spika, kutokana na maelezo hayo ni vyema kabla Serikali haijafikia hatua ya kuyagawa mashamba hayo kwa Watanzania wenye uwezo kama alivyopendekeza Mheshimiwa Mbunge, ni vema tukasubiri matokeo ya juhudi zilizoanza kuchukuliwa na uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro.


MHE. ALOYCE B.KIMARO: Mheshiiwa Spika,pamoja na majibu ya Mheshimiwa ya Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshiiwa Spika,lengo la kuuliza swali hili ni kutaka kujua Serikali ina mpango gani kambambe wa kufufua zao la kahawa katika Mkoa wa Kilimanjaro kwa kutumia mashamba haya ili wakulima wadogowadogo waweze kuiga. Sasa maswali mawili. Katika majibu ya serikali Naibu Waziri amesema kati ya mashamba 41, 27 yanafanya kazi na faida inayopatikana ina hudumia shule ,zahanati, barabara na kusaidia watoto wasiojiweza. Naomba Naibu Waziri atutajie kwa majina shule ngapi, zahanati ngapi, barabara ngapi na watoto wangapi wamefaidika.

Mheshiiwa Spika, swali la pili. Mashamba 14 hayazalishi kwa faida ama hayazalishi kabisa. Lengo la serikali ya awamu ya nne ni kufufua kilimo cha kahawa kutoka uzalishaji wa tani 40 mpaka tani 120 kwa mwaka. Sasa Waziri kusema kwamba tusubiri matokeo ya mkoa ni kama kukwepa wajibu wa kujibu swali langu. Naomba sasa Waziri anieleze, wizara inashiriki vipi katika kutatua mgogoro huu na wizara inategemea itaisha lini ili mashamba haya yaanze uzalishaji kwa faida?

SPIKA: Swali la kwanza la Mheshimiwa Kimaro ni hakika linadai takwimu. Kusema watoto wangapi wamefaidika sidhani kama Wizara ya Kilimo itakuwa nazo hizo takwimu. Labda itakapo zipata kutoka Elimu waweze kuwasilisha tu kwa maandishi. Kwa hiyo, nitmwomba Naibu Waziri ajibu kwa kifupi hili la pili.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA (MHE. MATHAYO D. MATHAYO): Mheshimiwa Spika, serikali hii ni moja kama nilivyoeleza sasa hivi uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro unashughulikia suala hili, basi ngoja watoe taarifa na sisi tutaona kama wizara tutaingia vipi. Lakini shughuli hii inashughulikiwa na Mkoa wa kilimajaro na ni suala ambalo wanalichukua serious kabisa. Kwa hiyo, nadhani tusubiri chombo hicho kwanza kimalize kazi yake halafu ndipo tujue kwamba tunachukua hatua gani.

MHE. PHILEMON NDESAMBURO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali fupi la nyongeza. Katika majibu ya serikali amesema wanangojea Kamati ya mkoa ifanye pitio ili waweze kujua watagawa lini hayo mashamba kwa watu wenye uwezo na mwenye kuuliza swali anataka mashamba haya wapewe watu wenye uwezo. Kilio cha wakazi wa Kilimanjaro ni ardhi hakuna na wangependa ardhi hii igawiwe kwa wakulima wadogo wadogo ili waweze nao kufaidika.

Je, serikali inataka kuzidi kuwazidishia wenye kipato na kuwasahau wale wadogo wasiokuwa na kipato?

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Mheshiiwa Spika, aliyependekeza kutoa mashamba haya kwa wenye uwezo ni Kimaro sio serikali. Sisi tulichosema katika jibu letu kwamba tunasubiri Mkoa umalize kufanya tathmini halafu tushirikiane na mkoa tuone namna gani tunaweza kumaliza tatizo hilo. Mashamba haya yalipewa watu wadogo kupitia Ushirika. Hiyo ndiyo msingi na msingi huo unaweza ukaendelea kuendelezwa bila kujali Kimaro anatakaje au anataka vipi. (Makofi)
 

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,135
Likes
70
Points
145

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,135 70 145
- Kudos! tunataka viongozi wanaojiamini namna hii, ingawa angejitahidi kuweka yale yote aliyoyafanya toka ashike ubunge, otherwise saafi sana kiongozi kuwa na this kind of confidence.

Respect.

FMES

Umesoma Hansard ukaona Bungeni anaongelea watu gani haswa wa Jimbo lake?
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Likes
86
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 86 0
Umesoma Hansard ukaona Bungeni anaongelea watu gani haswa wa Jimbo lake?
Re: KIMARO: Hakuna wa Kuning'oa Vunjo!
- Mkuu heshima yako, I am missing something hapo au? Naona kama kichwa cha mada ni tofauti na maneno yake bungeni, au?

Respect.


FMES!
 

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,135
Likes
70
Points
145

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,135 70 145
Read this,ama rudi nyuma post ya juu utaona hansard ,

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Mheshiiwa Spika, aliyependekeza kutoa mashamba haya kwa wenye uwezo ni Kimaro sio serikali. Sisi tulichosema katika jibu letu kwamba tunasubiri Mkoa umalize kufanya tathmini halafu tushirikiane na mkoa tuone namna gani tunaweza kumaliza tatizo hilo. Mashamba haya yalipewa watu wadogo kupitia Ushirika. Hiyo ndiyo msingi na msingi huo unaweza ukaendelea kuendelezwa bila kujali Kimaro anatakaje au anataka vipi. (Makofi)
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Likes
86
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 86 0
Read this,ama rudi nyuma post ya juu utaona hansard ,

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Mheshiiwa Spika, aliyependekeza kutoa mashamba haya kwa wenye uwezo ni Kimaro sio serikali. Sisi tulichosema katika jibu letu kwamba tunasubiri Mkoa umalize kufanya tathmini halafu tushirikiane na mkoa tuone namna gani tunaweza kumaliza tatizo hilo. Mashamba haya yalipewa watu wadogo kupitia Ushirika. Hiyo ndiyo msingi na msingi huo unaweza ukaendelea kuendelezwa bila kujali Kimaro anatakaje au anataka vipi. (Makofi)
Re: KIMARO: Hakuna wa Kuning'oa Vunjo!
- Maaan! unaweza kuwa specific unaongelea nini hasa, I mean mashamba na Kimaro kutamba kwamba hakuna wa kumtoa ubunge vinaingiliana vipi, anzisha topic mpya ya mashamba na Kimaro mkuu, au?

Respect.


FMEs!
 

bigilankana

Senior Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
143
Likes
2
Points
0

bigilankana

Senior Member
Joined Dec 15, 2009
143 2 0
- Kudos! tunataka viongozi wanaojiamini namna hii, ingawa angejitahidi kuweka yale yote aliyoyafanya toka ashike ubunge, otherwise saafi sana kiongozi kuwa na this kind of confidence.

Respect.

FMES
anajipa moyo tu. atashindwa na ama mrema wa chadema au mrema wa tlp. wakubaliane tu hawa wawili lakini yeyote atamshinda kwa mbali. nimemsoma huyo mrema wa chadema anasema eti kimaro aliaminiwa, na nani? alipata aslimia 38 ya kura. theluthi mbili ya wapiga kura walimkataa. atahsindaje?
 

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,135
Likes
70
Points
145

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,135 70 145
Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Mrema alidai Kimaro atapimwa na wananchi kwenye uchaguzi huo kwani hivi sasa amegeuka kuwa mtetezi wa watu wenye uwezo na si wananchi waliomchagua.

"Wanaoamua nani awe mbunge wao ni wananchi na Kimaro hawasaidii tena wananchi waliomchagua badala yake amekuwa mtetezi wa matajiri bungeni na kama unataka ushahidi tunao tutakupa," alisema. Alisema wananchi wanataka kupata taarifa kutoka kwa Kimaro jinsi yalivyotumika mamilioni ya fedha yaliyotolewa na wahisani mbalimbali kwa ajili ya kusaidia benki za kijamii vijijini maarufu kwa jina la VOCOBA. Mrema alisema hadi sasa mradi huo wa VOCOBA hauna maelezo ya kina na jinsi fedha hizo za wahisani zilivyotumika huku akidai kuwa kuna mchezo mchafu umetumika kwenye matumizi ya fedha hizo.

Source: Tanzania Daima.

Umesoma hii reaction ya upande wa pili ukalinganisha na story na Hansard?

kiranja
Senior Member
red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png
green.png
green_right.png
Join Date: Sat May 2007
Posts: 232
Thanks: 9
Thanked 18 Times in 12 Posts


report.gif
Report Post
subscribe.gif
Subscription
printer.gif
Show Printable Version
sendtofriend.gif
Email this Page
reputation.gif
Add to kiranja's Reputation
u
 

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,135
Likes
70
Points
145

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,135 70 145
FMES,
Najua pasinashaka kuwa unampenda Kimaro,na unaweza ukawa na mawasiliano naye.

Muulize swali hili, pesa za VICOBA zilizotolewa na Reginald Abrahamu Mengi , zimeenda wapi?
Je?zilitolewa ili akafungue kampuni linaloitwa VUNJO vicoba ltd?
N a muulize ni akina nani ambao ni shareholders wa hilo kampuni.
 

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,135
Likes
70
Points
145

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,135 70 145
anajipa moyo tu. atashindwa na ama mrema wa chadema au mrema wa tlp. wakubaliane tu hawa wawili lakini yeyote atamshinda kwa mbali. nimemsoma huyo mrema wa chadema anasema eti kimaro aliaminiwa, na nani? alipata aslimia 38 ya kura. theluthi mbili ya wapiga kura walimkataa. atahsindaje?
Hata kama alishinda kwa asilimia 20, ni kuwa yeye ndio aliaminiwa na watu wengi zaidi ya wenzake na hivyo alionekana kati ya wenzake waliokuwa 3 basi yeye ndio bora.
 

bigilankana

Senior Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
143
Likes
2
Points
0

bigilankana

Senior Member
Joined Dec 15, 2009
143 2 0
Hata kama alishinda kwa asilimia 20, ni kuwa yeye ndio aliaminiwa na watu wengi zaidi ya wenzake na hivyo alionekana kati ya wenzake waliokuwa 3 basi yeye ndio bora.
anaongoza jimbo ambalo 62% hawakumchagua. point blank. nani wengi? ambao waliona hafai kuwa mbunge. kwa vyovyote idadi hiyo imeongezeka
 

manuu

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2009
Messages
4,071
Likes
9,724
Points
280

manuu

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2009
4,071 9,724 280
Na pia anakashfa ya kununua shamba lilokuwa linamilikiwa na wananchi kule mkoani Arusha,yeye ndio chanzo cha wameru kukata migomba ya shamba alilomilikishwa kiufisadi so kwa kifupi its not type of leader we are looking for coz he has an element of ufisadi.
So wananchi wa vunjo tusimpe kura huyu hatufai.
 

Gagnija

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2006
Messages
6,468
Likes
728
Points
280

Gagnija

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2006
6,468 728 280
Kimaro si mpumbavu, kisha assess hali ya jimbo lake na kujiaminisha kuwa atashinda. Hivi baada ya uchaguzi mdogo kule Tarime hawa kina Mrema wawili wako katika terms za kuweza kuachiana ugombea? Nani atamwachia mwenzake ili Kimaro asirudi bungeni?
 

Recta

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2006
Messages
854
Likes
3
Points
35

Recta

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2006
854 3 35
anaongoza jimbo ambalo 62% hawakumchagua. point blank. nani wengi? ambao waliona hafai kuwa mbunge. kwa vyovyote idadi hiyo imeongezeka

Swali ni je, Alishinda uchaguzi ama lah?

Kama asilimia 38 walimpa kura zao, na kura hizo zikawa nyingi kuliko wagombea wengine wote, kwa mtazamo wangu alipata imani ya watu wengi. Labda kama kuna kitu kimefichwa hapa.

Pia kuna tatizo kuwa kama watu wengi wakiamua kugombea, hata kama asilimia hiyo itabaki kama ilivyo, kuna uwezekano akashinda tena.
 

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,135
Likes
70
Points
145

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,135 70 145
Kimaro si mpumbavu, kisha assess hali ya jimbo lake na kujiaminisha kuwa atashinda. Hivi baada ya uchaguzi mdogo kule Tarime hawa kina Mrema wawili wako katika terms za kuweza kuachiana ugombea? Nani atamwachia mwenzake ili Kimaro asirudi bungeni?

Kwa kuwa CCM watasimamisha wagombea wawili kwenye Jimbo moja ,basi wa CHADEMA hana haja ya kumwachia wa CCM.

Aloyce Bent Kimaro-CCM
Agustino Lyatonga Mrema-CCM (KUSIMAMIA MASUALA YA USHUSHUSHU}
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Likes
86
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 86 0
FMES,
Najua pasinashaka kuwa unampenda Kimaro,na unaweza ukawa na mawasiliano naye.

Muulize swali hili, pesa za VICOBA zilizotolewa na Reginald Abrahamu Mengi , zimeenda wapi?
Je?zilitolewa ili akafungue kampuni linaloitwa VUNJO vicoba ltd?
N a muulize ni akina nani ambao ni shareholders wa hilo kampuni.
- I am looking forward for the day, nitaruhusiwa kuwa na mawazo yangu kama bin-adam wengine humu, sasa yamekua ya mimi kumpenda na kuwa na mawasiliano, mkuu ninasema hivi ninamheshimu kiongozi yoyote anayeweza kusimama na kutamba kwamba hakuna wa kumshinda jimboni kwake hata angekua ni wa Chadema, ningempa hiyo heshima,

- Kieleweke sio siri una duku duku sana na huyu mbunge na utendaji wake wa kazi, tatizo moja tu ni kwamba hapa sio mahali pake, mfungulie topic ya utendaji wake wa kazi jimboni, hapa tuongee kutamba kwake kuwa hawezekaniki, nitaheshimu sana kama next time utaleta statitics sample za polls za wananchi huko jimboni kwa huyu mbunge ili tuchambue kama atashinda kweli au anazuga!

- So far ninampa heshima kwa kusimama na kutamba kushinda!

Respect.


FMEs!
 

Forum statistics

Threads 1,189,736
Members 450,798
Posts 27,645,707