Kimachale machale ndio mpango mzima.

Sijajua haya mapenzi mwisho wa siku inakuaje! sijui ndivyo ilivyokuwa hata kwa wazee wetu ujanani mwao au haya ya enzi hizi yamezidi!! .....
Naambiwa zamani hali ilikuwa ni tofauti maana binti kuolewa ilikuwa ni must kabla ya kuzaa na kuweka kitambaa cheupe juu ya kitanda ilikuwa ni fahali kubwa kwa wazazi wa binti. Binti hawakuwa na tamaa ya kununua gari au kujenga nyumba bali zawadi za mabinti ilikuwa hankachifu na mafuta ya vaselini. Wazazi wa binti hawakutegemea kupata fedha kila mwezi kutoka kwa mabinti zao bali vijana wao. Kuolewa kwa binti ilikuwa ni mwisho wa kuwa katika familia ya kwao na mwanzo wa kuwa katika familia ya mume wake. Hii yote imekufa kifo cha mende, na hata ukisoma makala nyingi za akinamama hapa JF ni ubingwa wa ki-Mohamed Ally kuwa na mabwana wengi wakisingizia kuwa wanatumia DUME ingawa kiuhalisia ni kavukavu ambapo uzeeni kansa ya kizazi inawasubiri kwa kuchanganya yale maji ya uzima kutoka kwa watu mbali mbali. Kwa sasa mabinti wengi wanazaa watoto wao na kuendelea na maisha bila kuwekwa ndani. Wengi wetu miaka 22 kama Njilinji hatuwajui baba zetu na maisha yanasonga mbele.

My take: Ukiishi Roma fanya kama waroma waishivyo. Mawazo ya kuoa mpaka kifo kiwatenganishe hayapo bali mpaka hamu ya kugegedana ikiisha ndo iwatenganishe, ndo mpango mzima. Nadhani umenipatatata -Karibu Njinjo.
 
Mh! Eti mletewe wengine unadhani nani anawaharibu kama siyo nyie wenyewe? Think twice!! Labda humtoshelezi mahtaji yake ndo mana anaminjemba mingine! Think again!!Chamsingi muombe mungu akupe binti mtulivu ! Masuala ya kuishi et kimachale mguu ndani nje kama sungura porini anayeogopa mishale c kujikosesha amani huko?tulizanaaa!!
 
women are cheating now days aiseee ........never seen before
 
Tatizo wanawake malaya na wanaume malaya ndiyo maana kila mtu analalamika, wanawake waache umalaya watulie na mpenzi moja na wanaume waache umalaya watulie na mpenzi moja. Tatizo kila mtu yupo kimachale, mwanamke kimachale na mwanaume kimachale .We need change , the change it start wth you. mimi nimeamua kuwa na mpenzi moja tu ambaye ni mke wangu wa ndoa , ndoa yetu inamiaka kumi na nne, tunaaminiana, tunauhuru na simu zetu, mke wangu anaweza kutumia simu yangu mda wowote anaotaka hapa mimi pia.
 
mambo mengine tunajitakia halafu tunalalamika, hivi wewe umetoka out na mpenzi wako badala ya kuwa busy na mpenzi wako unakuwa busy na gemu, kwanini usinunue gemu zile za watoto ukawa unatoka nayo? maana mpenzi wako hana umuhimu zaidi ya gemu, kwa hiyo na yeye ana wengine wanaomuona ni wa muhimu kwao. ukiona mwanamke anakucheat ujue kuna sababu, wanawake huwa ni waaminifu sana, may be unamtoa hiyo out ya mara moja kwa wiki halafu matumizi haumpi, kwa hiyo anawakumpa matumizi ila kwa vile anakupenda anakuvulia tu. jichunguze kwanza wewe ni wapi unakosea sio kulaumu laumu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…