KIM JONG-UN:Rais anayesumbua vichwa vya dunia

KIM JONG-UN:Rais anayesumbua vichwa vya dunia

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,083
Reaction score
34,859
kim_jong.jpg

Rais Kim Jong-un

KWA UFUPI
Msimamo wa kwanza wa Rais Kim Jong-un ulikuwa ni kupinga msaada wa chakula unaotoka Marekani ili kuondoa kifungo cha kufanya majaribio yake ya silaha za nyuklia.

Mwaka wa 2010 uliingia katika kumbukumbu za Korea Kaskazini baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Kim Jong-il kuzindua kombora lake ambalo wakakti wowote kuanzia sasa litafanyiwa majaribio.

Baada ya kifo cha rais Kim Jong-il , Desemba mwaka 2011 nchi hiyo ilikabidhiwa mikononi mwa mtoto wake Kim Jong-un aliyeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kulingoza vyema taifa hilo.
Baada ya kuapishwa rasmi Aprili 2012 , Kim Jong-un alichukua jukumu hilo na kuzindua satellite iitwayo "rocket-mounted' kama sehemu ya kumbukumbu ya kuenzi siku ya kuzaliwa kwa babu yake ambaye ni muasisi wa taifa hilo Kim Il-Sung.

Msimamo wa kwanza wa Rais Kim Jong-un ulikuwa ni kupinga msaada wa chakula unaotoka Marekani ili kuondoa kifungo cha kufanya majaribio yake ya silaha za nyuklia.

Kwa sasa taifa hilo la kaskazini limeimarisha vitisho vyake kama hatua ya kujibu mazoezi makali ya kivita, yanayondeshwa na Korea Kusini kwa ushirikiano wa Marekani, sanjari na kupinga vikwazo vilivyowekewa dhidi yake katika hatua yake ya kuimarisha zana za kinyuklia.
Katika ilani yake ya hivi karibuni, Rais huyo wa Korea Kaskazini amesema kuwa mpango wake umelenga makombora ya masafa marefu na yale ya kawaida kwa lengo la kuvamia vituo vya Marekani vilivyo Bahari ya Pacific wakati wowote.

Kim Jong-un ameweka tayari makombora hayo kukabiliana na tishio la mashambulio kutoka kambi za kijeshi za Marekani na ndege zake za kivita.
Rais Kim anasema hatua zake zitakwenda sambamba na kujibu ndege za kivita za Marekani kuruka katika anga ya Rasiya Korea.

Kim amesema kuwa kwa sasa muda umewadia wa kumaliza mgogoro na Marekani. Kwa upande wake Marekani na Korea Kusini zinasema kuwa hadi sasa imefanikiwa kunasa mipango ya ndani kutoka Korea Kaskazini kwamba ina kombora lenye na uwezo wa kushambulia umbali wa kilomita 3,000 likiwa na ujazo wa mafuta, tayari kwa kulipuliwa.

Mgogoro huo ulitokana na Peninsula ya Korea kugombewa na mataifa hayo, hatua iliyowahi kusababisha vita baina ya nchi Korea Kaskazini na Korea Kusini iliyopiganwa kati ya mwaka 1950 hadi 1953 ikijumuisha pia China,Umoja wa Kisovyeti na Umoja wa Mataifa (UN).
Machi 29 mwaka huu, mataifa makubwa duniani, China na Urusi yameelezea hofu ya kukithiri kwa mzozo katika Rasi ya Korea na kutaka pande zote kujiondoa katika majibizano.

Makubaliano ya mkutano huo ilikuwa ni kumaliza mgogoro uliopo kati ya nchi hizo.
Taarifa za kiuchunguzi uliofanywa na Korea Kusini zinaeleza kuwa Korea Kaskazini inajiandaa kukamilisha mipango yake ya kuzindua kombora, baada ya kuhamisha makombora yake mawili upande wa Pwani mwa nchi hiyo.

Katika mipango ya kujibu tishio hilo, Korea Kusini kwa ushirikiano na Marekani, zimeimarisha mitambo yake ya kuchunguza shambulio lolote kutoka kwa Rais Jong. Kufuatia hali hiyo, Korea Kusini nayo imeeleza kuimarisha hali yake ya tahadhari baada ya habari kuwa Korea Kaskazini inajiandaa kufanya jaribio la kombora lake moja la masafa ya kati, lililotarajiwa kufanyika April 15, mwaka huu kama sehemu ya kumbukumbu za kuzaliwa muasisi wa Taifa hilo Kim Ill-Sung.

Rais mpya wa Korea Kusini, Park Geun-Hye, amehimiza Korea Kaskazini kubadilisha mkondo wake wa siasa, ili kutuliza uhasama unaoendelea kukuwa kati ya mataifa hayo mawili.
Hali iliyopo kwa sasa kati ya nchi hizo mbili inadaiwa kutokuwa salama kwani Korea ya Kusini imedai kuwa Korea Kaskazini inawazuia hata raia wake kufika katika upande wa pili wa mpaka.

Wakati Marekani akiunga mkono harakati za Korea Kusini, Januari 25, mwaka huu, China pia imesema itaendelea kutoa ushirikiano wa misaada ya chakula kwa swahiba wake Korea Kaskazini, huku ikithibitisha kushiriki endapo kutatokea vita yoyote kati ya nchi hizo.

Mbali na kauli hizo, Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki moon amemtaka Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kupunguza makali yake kwa mzozo unaoendelea kushika kasi, akidai kuwa umeanza kuvuka mpaka. Ban Ki moon ameeleza kuhuzunishwa na namna ugomvi huo unavyotishia maisha ya wananchi wa kawaida na kutoa wito kwa viongozi wa Korea Kaskazini, kubadili mwenendo wao. Awali, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Urusi alisema kuwa uamuzi wa Korea Kaskazini kuendeleza mpango wake wa kuimarisha uwezo wa zana za kinyukilia, unavuruga mipango ya kuanzisha upya mashauriano yanayohusu mataifa sita ya kupatanisha Korea Kusini na Kaskazini.



Imeandaliwa na Kelvin Matandiko kwa msaada wa mashirika. chanzo. KIM JONG-UN:Rais anayesumbua vichwa vya dunia - Makala - mwananchi.co.tz






 
Namuunga mkono kim dhidi ya ulaghai wa USA.
Nipo nyuma yake
 
Marekani wako obsessed na Kim aisee hususan media zao.

Ila wiki jana alikuwa upstaged na Boston marathon bombing.

Pierce Morgan alikuwa kaanda special on North Korea iliyokuwa iruke Jumanne iliyopita lakini bahati mbaya haikuweza kurushwa.

Naisubiri kwa hamu sana.
 
Ukitaka wachangiaji wengi weka mzozoz wa nchi ya kiislamu. Huo ni uzoefu nilioupata humu JF mkuu......
 
wsj_print.gif



  • ASIA NEWS
  • Updated March 30, 2013, 11:36 a.m. ET
U.S. Pledges Further Show of Force in Korea

Officials Aim to Discourage Pyongyang From Rash Action With More Displays of Military Might, Following B-2 Flyover




By JULIAN E. BARNES

WO-AN209_NKOREA_G_20130329180720.jpg
Associated Press North Koreans punch the air during a mass rally at Kim Il Sung Square in downtown Pyongyang on Friday, amid escalating tensions.



WASHINGTON—American defense officials are vowing additional displays of advanced U.S. military might as they continue joint maneuvers with South Korea in the midst of growing tensions on the Korean peninsula.
Defense officials declined to detail their next steps, citing operational security concerns. But a new show of force would come after a pair of B-2 bombers flew over South Korea on Thursday and dropped dummy munitions. Earlier this month, U.S. B-52s flew over the peninsula.
The assertive U.S. response came in an intensifying exchange of threats and oaths with North Korea and as Russia and China appealed for calm. On Saturday, North Korea warned Seoul that the Korean Peninsula had entered "a state of war" and threatened to shut down a border factory complex that is a symbol of inter-Korean cooperation, the Associated Press reported.
While technically, the peninsula has been in a state of war for 60 years, U.S. officials are seeking to dissuade Pyongyang from rash steps. At the same time, Washington seeks to assure allies that, if necessary, American force would be used to defend them.
With joint U.S.-South Korean exercises scheduled to last for about 45 more days, there will be additional demonstrations of American firepower. "The United States will continue to demonstrate unique advanced capabilities as these exercises continue," said a defense official.

How far did B-2 stealth bombers travel for a "practice run" in South Korea? Why is North Korea threatening missile strikes against U.S. cities like Austin, Texas? WSJ's Jason Bellini has the Short Answer.


Although the use of U.S. heavy bombers risks provoking the North into a dangerous miscalculation, U.S. officials believe the joint exercises with South Korea ultimately will have a stabilizing effect.
In the U.S. view, provocations by Kim Jong Eun, the young North Korean leader, so far have been variations on actions taken by Pyongyang in the past.
"The North is running the same playbook, but using their more aggressive options. Everything they have done, they have done before," said the defense official. "The real worry will be when they throw out the playbook."
A key unanswered question, one U.S. official said, is how much risk Mr. Kim was willing to take to show "he's a tough guy."
"His inexperience is certain—his wisdom is still very much in question," the U.S. official said.
Seoul is expected to respond militarily should Mr. Kim go beyond threats and do something akin to attacking a South Korean ship, as North Korea did three years ago.
Mkuu MziziMkavu kajamaa kale ka N Korea hakana options zaidi ya kujipigia debe na kuraise the tension.Marekani yenyewe inajua hiyo ni geresha na mwisho atatoa demands zake.
Un wa Korea ni kama mtoto mdogo aliyeharibika, anapiga makelele mengi ,kupiga mateke na kuvunja vikombe na kumwaga maji ovyo, mwishowe anachotaka ni maziwa tu.


Bada ya kuona B-52 zinavinjari hewani akili ikamrudia na wiki iliyopita Un atakata maongezi ya amani.Jamaa wameshawazoea N Korea.
 
Ukitaka wachangiaji wengi weka mzozoz wa nchi ya kiislamu. Huo ni uzoefu nilioupata humu JF mkuu......
Kwa sababu wengi wetu tunapenda kushindana na mambo ya U-Dini wakati wazungu wanashindana kuhusu mambo ya upatikanaji wa Pesa na Maendeeo ya nchi sisi bado tupo nyuma kiakili na mambo ya U-Dini tutaendelea kweli jamnai? Malyenge Waliotuletea Mambo ya Dini wamekwisha sahau sisi bado tupo na mambo ya U-dini ni wapumbe pumbe tu sisi Wa-Danganyika.
 
Iwapo China atatia miguu yake kijeshi katika hii vita, basi itakuwa ni vita ya wababe wa dunia kupigania kwenye ardhi jirani. North Korea anayo backup nzuri sana ya China na Russia, ndipo jeuri zaidi itokeapo kwa Kim Jong Un.
 
Iwapo China atatia miguu yake kijeshi katika hii vita, basi itakuwa ni vita ya wababe wa dunia kupigania kwenye ardhi jirani. North Korea anayo backup nzuri sana ya China na Russia, ndipo jeuri zaidi itokeapo kwa Kim Jong Un.
Well said mkuu, at least Ka-marekani na kenyewe katakuwa kamepata vita ya size yake..! Na huo ndo utakuwa mwisho wa haka ka-nchi kutawala dunia. Natamani vita hii ianze haraka..! Ila kwa maoni yangu ikiwa North Korea ana assurance ya back up from China na Russia lazima Ka-marekani kataingia mitini faster..!
 
Back
Top Bottom