Kilio mshahara wa mwezi June kwa watumishi wa Umma

barwani

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
238
160
Wadau habari,kwa watumishi wa serikali jioni ya leo ni neema kwani serikali imewahi kulipa mishahara kwa mwezi huu,ila neema hii imekua chungu kwa wale walionza kuonja mishahara mipya miezi ya nyuma kulingana na vyeo walivyopanda.

Kama mwezi April au May ulilipwa kulingana na daraja/cheo ulichopanda ina maana mwezi huu umerudishwa kwenye mshahara wa cheo cha zamani...

Naomba kuwasilisha,tupo kwenye kipindi cha mpito,uvumilivu in silaha kubwa itakayotuvusha hapa tulipo..
 
Nadhani waliopata mishahara ni watumishi wa Halmashauri.
mimi nipo kwa katibu katibu mkuu nimecheki bado ila nimeangalia kwa wife wamemuwekea. pia nilipanda daraja la mshahara mwezi april mey nikapata salary mpya. hapa nahisi joto limepanda maana hiyo hela nimeshaipigia mahesabu
 
katiba tunatupa kule nchi inaendeshwa na mawazo ya mtu mmoja vile alivyojisikia ndivyo anavyoamua hapa kasi tuu demokrasia peleka upinzani
....nchi haiongozwi na mawazo ya mtuoja katu, mawazo anayoyatumia Mh. Rais, ni mawazo yaliyorundikana ambayo yalitakiwa yawe yalishafanyiwa kazi mapema huko nyuma!! Nyuma wapi? pengine nijibu hapahapa, nyuma kabla ya awamu yake!!!!
 
Wadau habari,kwa watumishi wa serikali jioni ya leo ni neema kwani serikali imewahi kulipa mishahara kwa mwezi huu,ila neema hii imekua chungu kwa wale walionza kuonja mishahara mipya miezi ya nyuma kulingana na vyeo walivyopanda.
Kama mwezi April au May ulilipwa kulingana na daraja/cheo ulichopanda ina maana mwezi huu umerudishwa kwenye mshahara wa cheo cha zamani...
Naomba kuwasilisha,tupo kwenye kipindi cha mpito,uvumilivu in silaha kubwa itakayotuvusha hapa tulipo..
Aiseee nilikupinga Bure tu.Samahani kwa hilo.Nilikuwa nimeangalia tu kwa wachache ambao hawajafyekwa.Ila taarifa yako IPO Sahihi waliopanda Mwezi Wa NNE na Wa tano wamerudishwa kwenye mishahara yao Ya awali.

Hii ngumu kumeza bora mshahara uongezeke sio kurudishwa nyuma.
Sio kweli watu wamepata mishahara ya vyeo vipya kama kawaida
Nimefuta hii comment sio valid tena
 
Nadhani waliopata mishahara ni watumishi wa Halmashauri.
mimi nipo kwa katibu katibu mkuu nimecheki bado ila nimeangalia kwa wife wamemuwekea. pia nilipanda daraja la mshahara mwezi april mey nikapata salary mpya. hapa nahisi joto limepanda maana hiyo hela nimeshaipigia mahesabu
Kama Ulipanda May hesabia maumivu
 
Back
Top Bottom