Kilio cha waliokuwa wafanyakazi wa NIDA kwa mheshimiwa rais

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,321
11,315
YAH: BARUA YA WAZI KUTOKA KWA WALIOKUWA WATUMISHI WA MUDA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)
Mheshimiwa Rais, sisi ni wafanyakazi tuliokuwa tukiitumikia mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambao mikataba yetu ya ajira ilisitishwa mnamo tarehe 07/03/2016 kupitia chombo cha habari (TBC). Taarifa hiyo ilitolewa na kaimu Mkurugenzi mkuu wa NIDA Dr. Modestus Kipilimba ambapo kwa mujibu wake idadi yetu tulikua wafanyakazi 597.
Mheshimiwa Rais, tunapenda kuujulisha umma wa watanzania kua sisi wafanyakazi 597 tuliokua watumishi wa NIDA bado hatujalipwa stahiki zetu ikiwa na pamoja na mishahara yetu ya kuanzia Januari 2016 mpaka mikataba yetu ilipositishwa, michango ya mifuko ya jamii GEPF, PSPF, NSSF, LAPF, PPF na NHIF, na stahiki nyingine.
Mheshimiwa Rais, tunapenda kusema kwa pamoja kwamba taarifa ambazo zimekua zikitolewa na kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dr. Modestus Kipilimba kupitia vyombo vya habari kwamba eti ameshatulipa stahiki hizo, taarifa hizo ni za uongo, tumelitumikia taifa letu kwa upendo, kujitoa na uaminifu wakati mwingine bila kulipwa chochote kama ilivotokea kipindi cha kati ya Januari na Machi 2016 tulifanya kazi bila kulipwa ujira wowote, mheshimiwa Rais utapata wapi watumishi kama hawa?? leo taifa limetuacha tuko mtaani hatuna pa kushika licha ya kwamba wengi wetu ni vijana
wenye nguvu na elimu kubwa.
Mheshimiwa Rais, tunashindwa kuamini kama leo hii tumekuwa watu wakulilia haki halali inayotokana na jasho letu ndani ya nchi hii iliyokwisha pata uhuru. Tunatambua kuwa nchi hii inaendeshwa katika misingi ya sheria na kusimamia haki ya kila mwananchi kama katiba yetu ya mwaka 1977 ilivyoamuru, lakini Mh. Rais haya yanayoonekana mbele yetu ni kinyume na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Ujira ni sehemu halali tunayostahili kulipwa kutokana na jasho letu.
Mheshimiwa Rais, kushindwa kutulipa stahiki zetu hadi hivi sasa, madhara na athari vimeendelea kujitokeza kwetu kama vile kushindwa kabisa kuendesha maisha yetu, kushindwa kuhudumia familia zetu, wazazi wetu, ndugu zetu na taifa kwa ujumla, wengine wamepata matatizo ya kiafya kama kupooza baadhi ya viungo vya mwili, pia wengine wamefukuzwa kwenye nyumba walizokua wamepanga kwa kukosa kodi, athari nyingine pia zimejitokeza katika familia zetu maana wengi wetu tulikua tegemezi katika familia zetu.
Mheshimiwa Rais, kilio chetu kikubwa ni malimbikizo ya mishahara yetu ya miezi 3, yaani kuanzia mwezi Janari mpaka mwezi Machi mwaka huu wa 2016 ajira yetu ilipositishwa, michango yetu ya mifuko ya hifadhi ya jamii kuanzia tulipoanza kuchangia hadi kusitishwa ajira zetu, pia stahiki zetu zote zinazotamkwa kisheria katika kifungu cha 44 cha sheria ya Ajira na Mahusiano ya kazi ya mwaka 2004 inayohusu taratibu za kusitisha mikataba ya Ajira.
Tunamuomba Kaimu Mkurugenzi wa NIDA atamke wazi ni lini atatulipa madai yetu na sio kueneza ahadi zisizotekelezeka tunasema hivyo kwasababu kupitia vyombo vya habari alitoa taarifa kua anaanza kutulipa kuanzia tarehe 13 Aprili 2016, lakini tulipofata hilo agizo tuligundua yalikua sio malipo bali uhakiki wa taarifa zetu na uchukuaji picha wa kila mmoja wetu, lakini pamoja na kwamba tulitii agizo hilo lakini bado malipo ya mishahara pamoja na stahiki zetu hayajaweza kufanyika hadi hivi sasa.
Tunaambatanisha taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari pamoja na taarifa nyingine ili vitumike kama vielelezo vya jinsi kaimu Mkurugenzi NIDA anavyoupotosha umma kwa kutoa taarifa ambazo ni tofauti na inavyotolewa katika vyombo hivyo vya habari.
Mheshimiwa Rais, tunakuomba kwasababu tunajua wewe ni kiongozi wa nchi lakini pia wewe ni mzazi una watoto kama sisi, tunatambua mzazi bora ni yule asiependa kuona watoto kati ya watoto wake wakiteseka kwa namna yoyote ile, tunatambua kwamba wewe ni mtu makini umefika wakati sasa wa wewe kutoa tamko juu ya suala letu, wanao tunateseka sana.
Tunatanguliza shukrani.
Imetolewa na sisi wafanyakazi wakiwa na wanyonge waliositishiwa mikataba ya ajira
MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA(NIDA).
IMG-20160413-WA0013.jpg
 
Nakumbuka NEC tuliona Pikipiki, meza, viwanja tupu, picha zisizo za wahusika kwenye ID za NEC.. .. do huu mradi umeingiliwa sana na utakosa maana na Identification ya mtz halisi...
 
Huu mradi sijui unakoelekea..
Lakini kama hawa vijana wameshafany kazi na wanadai kuwa hawajalipwa mishahara hili ni tatizo la unfair termination...
Linaweza kupelekea hawa watu wakalipwa wakati wote kama wako kazin toka tarehe ya termination..
Pia najiuliza mbona nilishasoma kweny gazeti kuwa wamelipwa hii sarakasi ya hapa siielewi kabisa ipo siku hapa pataota jipu.
 
ivi waziri wa mambo ya ndani yupo hai? waziri wa kazi je? suala la nida limekua gumu wahindi wakitunyanyasa sijui tutakmbilia wapi poleni vijana haki ya mtu haipotei inachelewa tu
 
View attachment 344256
HIZO NDIZO ATHARI ZA UKURUPUKAJI, UKITAWALIWA NA MIHEMKO MARA ZOTE HAYA
 
KILA LENYE MWANZO LINA MWISHO WAKE LAKINI, NA HUU NI UDIKTETA
 
kweli hawa wahanga wameonewa mno,heri kifungo cha gereza ambalo unaliona na unakuwa unajua kipindi gani kifungo kitaisha kuiliko kifungo cha aina hii.

Mamlaka iliwasitisha ajira ya watu hawa toka March ikitambua kabisa walitumikia miezi mitatu ambayo hawajalipwa.Toka mwezi huo hadi leo bado mamlaka hawajaweza kulipa zaidi huyo Mkurugenzi anajisafisha kwenye magazeti kuwa amewalipa,tena wiki kama tatu zilizopita akaweka ratiba ya malipo yatakavyokuwa yanafanyika na kuwaweka tention wakijua kwamba hatimae kilio chao kimefikia tamati.

Cha kusikitisha vijana hao wakakuta mengine kwamba si malipo bali ni uhakiki kutoka watu wa hazina kujua kuwa kweli ni wajiriwa kabla ya kuja kuwalipa.Kinachoshangaza ni kwamba mamlaka bado imekuwa kimya wakila bata bila kuwa na huruma kwa hawa wahanga kwa kuwalipa madai yao.
Kweli huyu mkurugenzi ana roho ya aina gani!!inamaana furaha yake ni kuona vijana hawa wanahangaika??Je,hatambui kilio cha hawa watu ni laana kubwa hasa kwa kudai amewalipa angali hakuna alichokifanya.Kazi yake ni kujisafisha kwenye media tu.
 
Hapa pana jipu si bure, thread kama hii nakutana nayo tena kwa mara ya pili.
Huyo kiongozi mpya inaonekana ni mtu wakukurupuka sio mtendaji mzuri.
Ama nafasi aliyo nayo haifiti kuwa mtawala kuna haja yakuangalia upya hili.. Tunataka watu wanaoweza kwenda kasi moja na Magufuli hasa watu wa maamuz nakuthubutu.. Huyu anashindwa nin analea viporo mpaka leo. Hafai
 
Vijana wa NEC Nlisikia hyo hyo DG aliwarusha sasa ameletwa nida anataka awarushe na nyinyi pia,, vijana endeleeni kukaza kamba bahati nzuri nyinyi wengi wenu MNA elimu ya kutosha diploma, Degree na masters holders coz nawafahamu wengi wenu najua hawezi kuwaburuza kama wale form 4 na 6 wa nec
 
Jasho la mtu haliliwi kirahisi rahic....anachokifanya huyo kiongoz wa NIDA si uungwana...aliwatangazia umma kuwa anamalizana na vijana aliowasimamisha ajira ili maisha yao yaendelee kumbe ni mbwembwe mbele ya jamii imuone wa maana kumbe nae tapeli na n jipu linalohitaj kutumbuliwa na kujazwa utambi kusafisha na vilivyomo ndan...huu n usawa wa utandawaz tupo pamoja nanyi kuweza kuwapazia saut na mtapata stahik zenu...ni jasho lenu na mnastahili zaid ya hiki mnachopigania.
 
nawauliza na kuwahoji.
je mlishawahi kwenda kuuona uongozi wenu kabla hamjaleta uzi huu ili kuwa na majibu ya uhakika kwa yanayoendelea? ?
Rais amezungumzia suala la watumishi hewa mmesema kulikuwa na uhakiki ukiendelea, which is ok, pesa ya walipa kodi imepotea sana mikononi mwa watumishi hewa. suala hili mmejibiwa vipi.
je kama hamjawaona viongozi husika na kupata majibu ya uhakika hamuoni kama mnajenga mahusiano ambayo siyo mazuri na mwajiri mkuu ambaye ni serikali. ukizingatia your still young and mnategemewa kuliongoza Taifa la kesho.
angalieni msije mkawa mnatumiwa nanyi mkatumika bila kujijua. nawashauri muwe careful
 
ivi waziri wa mambo ya ndani yupo hai? waziri wa kazi je? suala la nida limekua gumu wahindi wakitunyanyasa sijui tutakmbilia wapi poleni vijana haki ya mtu haipotei inachelewa tu
Watetezi wake wanasema hao walioachishwa wamechangia anguko la kitwanga
 
Huu mradi sijui unakoelekea..
Lakini kama hawa vijana wameshafany kazi na wanadai kuwa hawajalipwa mishahara hili ni tatizo la unfair termination...
Linaweza kupelekea hawa watu wakalipwa wakati wote kama wako kazin toka tarehe ya termination..
Pia najiuliza mbona nilishasoma kweny gazeti kuwa wamelipwa hii sarakasi ya hapa siielewi kabisa ipo siku hapa pataota jipu.
Mkuu naona limeshakuwa tambazi
 
ivi waziri wa mambo ya ndani yupo hai? waziri wa kazi je? suala la nida limekua gumu wahindi wakitunyanyasa sijui tutakmbilia wapi poleni vijana haki ya mtu haipotei inachelewa tu
Watetezi wake wanawahusisha hao waliotumbuliwa na anguko la mlevi
 
Back
Top Bottom