BilioneaPATIGOO
JF-Expert Member
- Jun 23, 2012
- 12,320
- 11,322
3/5/2016
YAH: BARUA YA WAZI KUTOKA KWA WALIOKUWA WATUMISHI WA MUDA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) KWENDA KWA MH. RAIS WA JAMHURI YAMUUNGANO WA TANZANIA.
Mheshimiwa Rais, sisi ni wafanyakazi tuliokuwa tukiitumikia mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambao mikataba yetu ya ajira ilisitishwa mnamo tarehe 07/03/2016 kupitia chombo cha habari (TBC). Taarifa hiyo ilitolewa na kaimu Mkurugenzi mkuu wa NIDA Dr. Modestus Kipilimba ambapo kwa mujibu wake idadi yetu tulikua wafanyakazi 597.
Mheshimiwa Rais, tunapenda kuujulisha umma wa watanzania kua sisi wafanyakazi 597 tuliokua watumishi wa NIDA bado hatujalipwa stahiki zetu ikiwa na pamoja na mishahara yetu ya kuanzia Januari 2016 mpaka mikataba yetu ilipositishwa, michango ya mifuko ya jamii GEPF, PSPF, NSSF, LAPF, PPF na NHIF, na stahiki nyingine.
Mheshimiwa Rais, tunapenda kusema kwa pamoja kwamba taarifa ambazo zimekua zikitolewa na kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dr. Modestus Kipilimba kupitia vyombo vya habari kwamba eti ameshatulipa stahiki hizo, taarifa hizo ni za uongo, tumelitumikia taifa letu kwa upendo, kujitoa na uaminifu wakati mwingine bila kulipwa chochote kama ilivotokea kipindi cha kati ya Januari na Machi 2016 tulifanya kazi bila kulipwa ujira wowote, mheshimiwa Rais utapata wapi watumishi kama hawa?? leo taifa limetuacha tuko mtaani hatuna pa kushika licha ya kwamba wengi wetu ni vijana
wenye nguvu na elimu kubwa.
Mheshimiwa Rais, tunashindwa kuamini kama leo hii tumekuwa watu wakulilia haki halali inayotokana na jasho letu ndani ya nchi hii iliyokwisha pata uhuru. Tunatambua kuwa nchi hii inaendeshwa katika misingi ya sheria na kusimamia haki ya kila mwananchi kama katiba yetu ya mwaka 1977 ilivyoamuru, lakini Mh. Rais haya yanayoonekana mbele yetu ni kinyume na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Ujira ni sehemu halali tunayostahili kulipwa kutokana na jasho letu.
Mheshimiwa Rais, kushindwa kutulipa stahiki zetu hadi hivi sasa, madhara na athari vimeendelea kujitokeza kwetu kama vile kushindwa kabisa kuendesha maisha yetu, kushindwa kuhudumia familia zetu, wazazi wetu, ndugu zetu na taifa kwa ujumla, wengine wamepata matatizo ya kiafya kama kupooza baadhi ya viungo vya mwili, pia wengine wamefukuzwa kwenye nyumba walizokua wamepanga kwa kukosa kodi, athari nyingine pia zimejitokeza katika familia zetu maana wengi wetu tulikua tegemezi katika familia zetu, hizi ni athari za jambo hili linavyoendeshwa hivi sasa.
Mheshimiwa Rais, kilio chetu kikubwa ni malimbikizo ya mishahara yetu ya miezi 3, yaani kuanzia mwezi Januari mpaka mwezi Machi mwaka huu wa 2016 ajira yetu ilipositishwa, michango yetu ya mifuko ya hifadhi ya jamii kuanzia tulipoanza kuchangia hadi kusitishwa ajira zetu, pia stahiki zetu zote zinazotamkwa kisheria katika kifungu cha 44 cha sheria ya Ajira na Mahusiano ya kazi ya mwaka 2004 inayohusu taratibu za kusitisha mikataba ya Ajira.
Tunamuomba Kaimu Mkurugenzi wa NIDA atamke wazi ni lini atatulipa madai yetu na sio kueneza ahadi zisizotekelezeka tunasema hivyo kwasababu kupitia vyombo vya habari alitoa taarifa kua anaanza kutulipa kuanzia tarehe 13 Aprili 2016, lakini tulipofata hilo agizo tuligundua yalikua sio malipo bali uhakiki wa taarifa zetu na uchukuaji picha wa kila mmoja wetu, lakini pamoja na kwamba tulitii agizo hilo lakini bado malipo ya mishahara pamoja na stahiki zetu hayajaweza kufanyika hadi hivi sasa.
Tunaambatanisha taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari pamoja na taarifa nyingine ili vitumike kama vielelezo vya jinsi kaimu Mkurugenzi NIDA anavyoupotosha umma kwa kutoa taarifa ambazo ni tofauti na inavyotolewa katika vyombo hivyo vya habari.
Mheshimiwa Rais, tunakuomba kwasababu tunajua wewe ni kiongozi wa nchi lakini pia wewe ni mzazi una watoto kama sisi, tunatambua mzazi bora ni yule asiependa kuona watoto kati ya watoto wake wakiteseka kwa namna yoyote ile, tunatambua kwamba wewe ni mtu makini umefika wakati sasa wa wewe kutoa tamko juu ya suala letu, wanao tunateseka sana.
Tunatanguliza shukrani.
Imetolewa na sisi wafanyakazi wakiwa na wanyonge waliositishiwa mikataba ya ajira
MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA(NIDA).