Kilio cha wadau na Wakulima wa Pamba chapata ukombozi

Kilio cha wadau na Wakulima wa Pamba chapata ukombozi

chipoteka

Member
Joined
Jan 9, 2015
Posts
66
Reaction score
25
Moja kati ya sekta muhimu ktk uchumi wa kanda ya ziwa ni zao la Pamba.Wananchi na wakazi wengi wa eneo hili wamekuwa wanategemea pamba kama sehemu ya maisha yao.Maeneo ya shinyanga,Mwanza,Geita,Simiyu na Mara Pamba hujulikana kama dhahabu nyeupe,lakini kwa miaka kadhaa "dhahabu nyeupe" imekumbwa na misukosuko ya hapa na pale ktk soko la Ndani na nje ya nchi.

Kati ya ahadi za Waziri mwenye dhamana na Wizara ya Kilimo na Ushirika Mh.Steven Massatu Wassira wakati ameteuliwa tena kushika wizara hiyo ni kushughulikia deni la serikali kwa wakulima ambalo tayari limeanza kulipwa na kuangalia upya tatizo la zao la pamba.

Kwa kushirikiana na wadau wa Pamba kanda ya ziwa,ili kuhuisha na kuinua upya zao la Pamba,Mh.Wassira atakuwa na Mkutano na wadau hao kuanzia 23/02-24/02 katika ukumbi wa BOT Mwanza.Lengo la Mkutano huo ni kujadili changamoto mpya ktk sekta ya kilimo na zao la Pamba kwa ujumla,kuchanganua mbinu mpya za kuinua Kilimo cha pamba ktk eneo la kanda ya ziwa ambako uchumi wa Watu wengi katika ngazi ya kaya hutegemea Kilimo ili kujikimu.

Mh.Wassira amewahikishia wakulima na wadau wa Pamba kupata suluhisho la kudumu la changamoto na matatizo ya pamba,kwa kutumia BRN serikali itaweka kipaumbele ili kuinua zao la pamba,Wadau wa Pamba wametoa pongezi kwa Mh.Wassira kwa jinsi anavyoshughulikia matatizo ya wakulima kwa haraka na kutatua kero zao,wamemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kumrudisha Wassira ktk wizara hiyo kwani mipango mingi aliyokuwa ameianzisha hapo awali salsa inazidi kupata msukumo chini ya Wassira
attachment.php

ImageUploadedByJamiiForums1424686795.640698.jpgImageUploadedByJamiiForums1424686868.931060.jpg
 
Naona Zao la pamba kwa miaka ya kanda ya ziwa linashika hatamu upya. Nakuombea sana Wassira uwasaidie watu hao maana wewe ndie tegemeo lao miaka yote.

Asante Mungu kwa ajili ya Wassira na tunaamini ukitangaza nia wakulima sasa ni wakati wa kukuunga Mkono ili uwatee ukiwa rais wa Jamhuri ya Muungajo wa Tabzabia 2015/. Nakuombea Wassira wewe ndie uliyeletwa.
 
Duuhh mbona mnaleta utoto. Huyu Wasira kwa nini hili la Pamba hakulipigania tangu awali, au hakuwa anaingia kwenye vikao vya Baraza la mawaziri?
 
Back
Top Bottom