Jana vituo vya habari vikiwemo radio na televison wametangaza wananchi wa vijiji vya DODOMA wanakula UBUYU na wa Tanga hamna hata ubuyu wanakufa, na watoto wameeacha shule na ndoa zimevunjika wanaume wao wamekimbia kwenda kutafuta chakula na hawajarudi tena labda wengine mauti yamewakuta njiani. Serekali ichukue hatua za haraka na irudishe ule msaada wa ZIMBABWE wapatiwe hao wanachi wenzetu chakula wanaokufa.
Poleni sana ndugu zangu. Bila shaka wakuu wamesikia kilio na kuona kwenye luninga sasa mtapata misaada ya chakula.
Hujafungwa mikono na miguu lakini mvua hazikunyesha na wakulima hawakupata mazao. Unataka watumie mikono na miguu waliyonayo kuteka watu na magari njiani? Unata wahame vijiji vyao? na wakihama wanakwenda wapi penye unafuu? Mjini kwenyewe kumejaa sana sasa hivi na pia ombaomba siku hizi hawapati sana, watu "wamefulie"Firsr of all wananchi wenyewe ni wa kulaumiwa kwani kufa njaa na hujafungwa mikono wala miguu ni uzembe, second serekali haina mkakati wowote madhubuti kwa lolote la nchi hii,kama hata umeme karne hii ni tabu unatarajia nini?ujinga mtupu
Walitangaza pia ni serikali kwani ni mkuu wa wilaya pamoja na mbunge wake.baru unaongea point gan? inamaana wakuu hawajui mpaka vitangazwe kwenye vyombo vya habari? hii ni kutokuwajibika kwa viongozi husika katika eneo hilo. kuanzia mwenyekiti, katibu mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya mkurugenzi, na mpaka mbunge wao, wote hawana maana, kingine unawezaje kusema hakuna mtu ataekufa na njaa wakati wanaokufa wapo? mi nashangaa nchi hii kwakweli..ghaaa boring..nauwezo naingia msituni
Hipocrisy tu imewajaa viongozi wetu. Halafu tunasema maisha bora kwa kila mtanzania.