Kilio cha maji safi mpaka lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilio cha maji safi mpaka lini?

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Aug 12, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Licha ya jitihada mbalimbali za serikali na wadau mbalimbali katika kufikisha huduma ya maji safi na salama kwa wananchi bado hali imekuwa tete kwa asilimia kubwa ya wananchi kwani huduma hiyo imeendelea kuwa kitendawili ambacho hakijulikani lini kitateguliwa.

  Ni jambo la kawaida sana unapoambatana na viongozi wa serikali na hata unapotembelea eneo fulani kukumbanana malalamiko ya ukosefu wa maji.

  eEhemu nyingine unapata kauli za kusikitisha zaidi unaposikia wakisema kuwa tangu nchi ipate uhuru mwaka 1961 hawajawahi kuwa na huduma ya maji safi kijijini kwao.

  Katika hili waathirika wakubwa ni wanawake na watoto kwani hulazimika kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kusaka maji ambayo bado hayatoshelezi mahitaji yao ya kila siku.

  Katika baadhi ya maeneo hapa nchini hususan vijijini wananchi wamefikia hatua hata ya kuoga mara moja kwa siku na hata kutumia chombo kimoja wakati wa kula ili wasipate usumbufu kuviosha.

  Hata hivyo sehemu nyingine uhaba huu umeteneneza ajira kwa vijana ambapo ndoo ya lita 20 za maji huuzwa kati ya sh. 400 hadi 500.

  Katika wilaya za Mwanga, Same, Hai, Siha, Moshi vijijini na Rombo na wilaya nyingine katika mikoa mingine ya Tanzania Bara, bado kuna tatizo kubwa la maji na wananchi hulazimika hutumia muda mwingi kusaka maji badala ya kuzalisha.

  Pamoja na matatizo hayo zipo baadhi ya Manispaa hapa nchini ambapo kutokana na kuwepo kwa mamlaka za majisafi na majitaka zimeweza kuwa na huduma ya uhakika,ikiwemo Manispaa ya Moshi lakini katika baadhi ya mikoa kama Dar es Salaam huduma hiyo imekuwa adimu na ambapo katika baadhi ya maeneo ndoo moja huweza kufika hata shi 700.

  Nchi yetu imebarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji na raslimali nyingi lakini kilichosababisha huduma hiyo kuendelea kuwa adimu kwa wananchi ni uwezo mdogo wa serikali katika kujenga miundombinu ya maji na kuwasambazia wananchi wake kutokana na ukweli kwamba kwa kiasi kikubwa bajeti ya nchi yetu inategemea misaada ya wahisani kutoka nje ya nchi.

  Kila mwaka serikali imekuwa ikitangaza mikakati thabiti ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wanachi lakini bado tatizo la maji lipo kwa kiasi kikubwa na haijulikani ni lini litapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

  Jitihada hizo katika baadhi ya maeneo zimeonekana wazi huku katika baadhi ya maeneo ikiwa ni kitendawili kutokana na kukithiri kwa migogoro aidha baina ya serikali na wananchi kutokana na ushirikishwaji duni wa wananchi na hata mwekezaji na wananchi hali inayosababisha kuwepo kwa hujuma ya miundombinu.

  Katika kila kikao cha Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania cha , kilio kikubwa cha wabunge ambao hukiwasilisha kwa serikali ni ukosefu wa maji katika majimbo yao hali inayosababisha mateso na taabu kubwa kwa wananchi.

  Katika kikao cha bajeti cha Bunge mwaka huu, ,Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof.Mark Mwandosya alisema kuwa serikali imekuwa ikitekeleza mradi wa majisafi na usafi wa mazingira vijijini katika wilaya 14 hapa nchini kwa fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia kuanzia mwaka 2002 hadi 2008.

  Mpaka sasa kati ya vijiji 138 vilivyokuwa vinufaike, na mradi huo , vijiji 119 mradi huo umeshakamilika .

  Anasema hadi sasa serikali imekamilisha mchakato wa kupata wataalam washauri watakao saidia halmashauri kupitia programu ya Maji na Usafi wa Mazingira vijijini ikiwa ni pamoja na wahandisi kuajiriwa na upatikanaji wa vifaa ili kuifanya programu hiyo kuwa endelevu.

  Waziri Mwandosya anasema baada ya kuandaa sera ya maji mwaka 2002,mwaka 2007/08 serikali ilianza kutekeleza programu ya sekta ya maji ambapo sheria mbili mpya ya usimamizi wa raslimali za maji na sheria ya huduma za maji na usafi wa mazingira zilipitishwa na Bunge Aprili 27 na 28 mwaka huu.

  Anasema programu hiyo inatekelezwa kwa makundi makuu manne ya wadau ambao ni wananchi,taasisi zisizo za kiserikali,madhehebu ya dini na halmashauri na serikali kuu.

  Anasema kuhusu usafi wa mazingira kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii wananchi huhamasishwa usafi wa mazingira na mtu binafsi katika jamii.

  Kutokana na kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama hususan maeneo ya vijijini bado maradhi ya kuhara na kipindupindu yameendeea kuwaandama wananchi kutokana na ukweli kwamba maradhi mengi yanatokana na maji yasiyo salama.

  Prof Mwandosya anasema katika mwaka wa fedha 2008/09 taarifa za mikoa husika zilionyesha kuwa miradi ya maji 1,151 kati ya 2,470 sawa na asilimia 47 ilikamilika ambapo pia vituo vya kuchotea maji 2,873 vimejengwa na watu wapatao 692,000 wananaufaika na huduma ya maji .

  Mei 2009 halmashauri na sekrtarieti za mikoa kwa ajili ya kutekeleza progaramu hiyo katika vijiji kumi kwa kila halmashauri nchini,ambapo zaidi ya shilingi bilion 60.15 zimetumika. Anasema mwezi Juni mwaka huu zaidi ya shilingi billion 25.11 zitatumika kwa halmashauri zote kwa ajili ya kujenga uwezo wa halmashauri husika kugharamia wataalam washauri watakaoanza kazi za usanifu wa miradi ya maji katika vijiji vilivyoainishwa na kila halmashauri.

  Waziri Mwandosya anasema pamoja na utekelezaji huo pia ipo miradi iliyotekelezwa nje ya fedha za mfuko wa pamoja wa programu ya maendeleo ya sekta ya maji ukihusisha ukarabati na ujenzi wa mabwawa kama vyanzo vya maji kwa ajili ya miradi ya maji na usafi wa mazingira hasa katika maeneo kame.

  “Katika kipindi cha mwaka 2008/09 ujenzi wa mabwawa 18 umefanyika na kufikia katika hatua mbalimbali za utekelezaji,kati yake 14 yalianza kujengwa mwaka huo huo wakati bwawa moja la Mugumu ujenzi wake ulianza zamani na mabwawa matatu ni muendelezo wa yale yaliyoanza kujengwa mwaka 2007/08”anasema.

  Pamoja na programu ya maendeleo ya sekta ya maji kuna miradi inatekelezwa ikifadhiliwa na asasi au mataifa mbalimbali ikiwemo miradi ya Moshi vijijini na Hai mkoani Kilimanjaro inayotekelezwa kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW).

  Anataja miradi mingine kuwa ni mradi wa maji wa Monduli na Longido mkoani Manyara unaotekelezwa na serikali kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika ,mradi wa maji mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, Mara , Mwanzana Tabora inayotekelezwa kwa kushirikiana na serikali ya Japan pamoja na mradi wa maji wa Shinyanga na Dodoma unaotekelezwa kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya Korea.

  Anasema katika kutekeleza miradi mikubwa ya maji vijijini kwa vijiji kumi kwa kila halmashauri,wataalam mbalimbali wameanza kuajiriwa kwa ajili ya kusanifu na kwamba halmashauri zimegawanywa katika makundi matatu likiwemo kundi la halmashauri 82,jingine la halmashauri 17 na kundi la halmashauri 33.

  Anasema kati ya halmashauri hizo halmashauri 38 zimeshapata wataalamu washauri,rasimu za mikataba zimeshapata ridhaa ya Benki ya Dunia kwa ajili ya halmashauri kusaini mikataba kati yake na wataalam washauri huku halmashauri 25 wataalamu hao wameshaanza kazi za usanifu,halmashauri 13 zimepata ridhaa ya kusaini mikataba, sita zimepata ridhaa ya rasimu na saba zimepata ridhaa lakini hadi sasa hazijasaini mikataba.

  Februari mwaka huu Prof Mwandosaya anasema ajira za wahandisi 96 waliajiriwa ili kutekleza miradi hiyo sanjari na halmashauri na sekretarieti kupatiwa nyezo za kufanyia kazi ikiwemo magari 123,pikipiki 252,Kompyuta 111 na vifaa vya mawasiliano ambavyo hadi Disemba mwaka huu vitakuwa vimesambwazwa.

  Anasema pamoja na jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata majisafi na salama lakini bado kuna changamoto nyingi ikiwemo kukosekana kwa wakandarasi wenye sifa na uzoefu unaokidhi utekelezaji wa programu katika maeneo kadhaa ya halmashauri nchini.

  Pamoja na miradi na mikakati mbali mbai ya maji kuwepo inaonekana kilio cha maji kwa wananchi kiko pale pale.

  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...