KILIO CHA AJIRA: Ukimya wa Rais Magufuli waleta hofu

Hivi jamani hili tatizo litaisha lini na serikali hii ya awamu ya tano iweze kuajiri vijana maana wanahamu sana wakafanye kazi kama kauli mbiu inavosema kazi tu tunavokaa mtaani tutajiingiza ktk makundi hatarishi !!

Mkiendelea kulalamika nyuma ya keyboard tu bila kuionyesha serikali kwa vitendo tatizo lenu basi endeleeni kuumia tu, nobody cares.
 
Tumemalizia pabaya sana. Bora uchaguzi ungekuwa mwaka huu.
Walichotufanyia ccm sitakisahau kbsa. They are animals
 
Inaonekana ajira ya kuajiriwa serikalini ni tatizo sana, na pia watu wanapomaliza vyuo mbalimbali wanategemea kuajiriwa,hv wataalam wetu wa masuala ya elimu bado hawajaona umuhimu wa kua na mitaala ambayo itatusaidia mtu kujiajiri ili amalizapo shule aweze kuendesha maisha yake au wameona kua hilo haliwezekani?
 
Usitegemee serikali kumaliza tatizo la ajira, kinachowezekana ni kuwajengea watz mazingira ya kuzalisha ajira
 
Ndio muhitaji mabadiliko sio kung'ang'Ania ccm
Siwezi kuishabikia CCM hata siku moja bora nishaibikie timu ya mpira kuliko hawa jamaa.
Hawajali maumivu ya watu kbs. Wenyew wanakula na kunywa hawawez kuwakumbuka wengine
 
Na kung'ang'ania kuajiriwa wakijua kabisa kwamba ofisi hazitoshi ni aina nyingine ya kasoro anayokuwa nayo mtu ambae hajaelimika wanaitaje sijui uj.....
Mtaji wa kujiajiri uko wapi? hata hivyo mfumo wa elimu yetu haulengi kumuandaa mhitimu kujiajiri
 
Mheshimiwa Mkuu wa nchi, ni msema kweli, na ni mpenzi wa Mungu. Alitoa tamko kuwa Baada ya uhakiki wa wafanyakazi hewa utakapokamilika ndipo ajira zitatolewa na Wafanyakazi wanaostahili kupandishwa madaraja watapandishwa. Alisema zoezi lingechukua muda mwezi mmoja na Nusu, lakini halitozidi miezi miwili. Tamko lilitoka 22.06.016
 
Mtaji wa kujiajiri uko wapi? hata hivyo mfumo wa elimu yetu haulengi kumuandaa mhitimu kujiajiri
Elimu ya ujasiliamali wanavyouita wao inaletwa na shida, na hakuna sehemu wanapogawa mtaji, kwamba walio na mitaji kuna sehemu walipewa na pia ujue hakuna mtaji mdogo, unaweza ukaanza na kufyeka tu nyasi kwa upanga wa kuazima na baadae ukawa bilionea sema tukishapita darasani tunachagua kazi ila "mimi" ni wa tofauti nikikupa historia yangu huwezi kuamini
 
Hivi jamani hili tatizo litaisha lini na serikali hii ya awamu ya tano iweze kuajiri vijana maana wanahamu sana wakafanye kazi kama kauli mbiu inavosema kazi tu tunavokaa mtaani tutajiingiza ktk makundi hatarishi !!
Mwezi ujao serikali inaanza upya kuhakiki watumishi wa umma. Nadhani wakimaliza wanaweza kuanza kufikiria masuala ya ajira
 
Back
Top Bottom