Kilimo cha tija kinahitaji mipango mikakati yenye ubunifu

Kilimo cha tija kinahitaji mipango mikakati yenye ubunifu

Fikra Angavu

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
301
Reaction score
106
Habari wadau.

Ni miaka mingi sasa tumekua tukiambiwa na kuaminishwa kua kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa letu, kauli mbiu nyingi sana tumezisikia kuhusu kilimo na hamasa pia kutoka serikalini na wadau wa kilimo nchi nzima... tumekua tukiletewa vitendea kazi, madawa na pembejeo lakini bado havikidhi mahitaji ya jamii za wakulima na taifa kiasi cha kufanya kilimo kidumae/ kiendelee tu kuwepo pale pale miaka nenda miaka rudi.
lakini swali najiuliza... ni kweli tunahitaji tu hizo pembe jeo na uhamasishwaji kujikita katika kilimo na kukifanya kiwe na tija...?
idadi kubwa ya wakulima Tanzania ni wale wanaotumia kilimo kujipatia chakula na kuuza kidogo kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku.
najua wananchi tunatakiwa kujituma zaidi ili kuinua kilimo kwa faida yetu na taifa kwa ujumla, ila serikali inayo nafasi kubwa sana katika kushiriki katika hili na kufanya kilimo kiwe na tija zaidi.
Kwa mawazo yangu machache nikaona kuna haja serikali na wadau waungane kufanya hili.

Tanzania tumejaaliwa sana ardhi yenye rutuba, rasilimali watu wenye nguvu na uwezo wa kufanya mambo makubwa kwenye kilimo... na uzuri Kila mkoa Tanzania una sifa zake katika kilimo, karibuni mikoa yote Tanzania ina mazao ya biashara na mingine haina lakini kwa mipango na mikakati mazao yote yanaweza kuletea faida wananchi na taifa kwa ujumla. mfano Tanga kuna matunda ya kila aina, Mtwara kuna korosho... kagera kuna ndizi... dodoma kuna zabibu, hapo kanda ya ziwa kuna pamba nk.

Kupitia Wizara ya Kilimo ambayo mimi sioni kazi yao kubwa au labda sifatilii.

Serikali iandae mipango madhubuti kisayansi tena kwa ubunifu zaidi wa kuigawa Tanzania kimikoa au kanda kulingana na mazao yanayolimwa.

kila mkoa uandaliwe kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya wao kulima kwa tija ili kurahisha usimamizi. serikali kupitia mikoa na wizara ya kilimo... wakae watenge maeneo kujenga masoko na kuandaa mikakati wa kuwashawishi wawekezaji kujenga viwanda vya usindikaji katika kila mkoa kwa mazao husika.

kila mkoa au kanda ukiwa na masoko makuu ya mazao wanayolima itapelekea kujulikana kabisa ukanda upi au mkoa upi kuna limwa nini... wafanya biashara wanajua kabisa wapi pakwenda kununua nini... hili litaleta ushindani wa kimikoa na kusababisha upatikanaji wa chakula mwaka mzima kwani kila mkoa utakua ukilima mwaka mzima.
Hivi ikiwa hivi kutakua na njaa kweli...?
Hapa lazima kutatokea ziada ambayo ndio itauzwa nje ya nchi. wakulima watakua masikini kweli... ikiwa elimu na upatikanaji wa vifaa vya kilimo vikipatikana kupitia mkakati huu...?
Kwa sasa kuna tabaka katika kilimo... wenye pesa ndio hufanya kilimo cha kimaendeleo... wasio na pesa hulima kwa ajili tu ya kula LAZIMA HILI LIONDOKE.

MAZINGIRA MAZURI YATAKAYOANDALIWA NA MIPANGO MIJI MIKOANI NA WIZARA YA KILIMO yatasababisha fursa nyingi sana pembeni ya mpango huu... wenye kuifanya kilimo na uvuvi Tanzania kua na tija na kuondokana na umasikini kwa wananchi na TAIFA.

TUOGEZENI MAWAZO AU TUKOSOANE ILI KUYAJENGA.
AHSANTE
 
Wazo zuri sana kimsingi kila mkoa/kanda ikiwa ina mazao yake yakulima itasaidia sana kutokomeza njaa ma bwana shamba kny. serikali ikitoa mwongozo ya mazao tukajua tunahitaji tani ngapi kwa mwaka kwa mazao fulani ili kukidhi mahitaji nadhani njaa itapotea kabisa namuunga mkono mgombea wa uraisi hashim rungwe alikua na nia kama hii ya kupoteza kabisa tatizo la njaa...back to the point umeongea point sana mkuu
 
sio tu kujua tani ngapi zinahitajika na kutokomeza njaa... pia kutaleta ushindani baina ya mikoa, itaongeza ufanisi na ubora wa mazao kwenye ushindani wa soko la nje...! kutakua na faida nyingi sana.
 
sio tu kujua tani ngapi zinahitajika na kutokomeza njaa... pia kutaleta ushindani baina ya mikoa, itaongeza ufanisi na ubora wa mazao kwenye ushindani wa soko la nje...! kutakua na faida nyingi sana.

kweli kabisa mkuu hii itafaa sana kwenye ile mikoa inayolima mazao yanayofanana hii inaweza pelekea tukapata surplus ya kuuza nje au pengine kusaidia nchi zenye njaa. sijui ni lini tutaamka vitu kama hivi vitaisogeza ile tanzania ya viwanda karibu kuliko inavyofikirika
 
kuna misemo inatutafuna wenyewe... usimuamshe alielala... wageni wanakuja kutuchukuia malighafi zetu.. huku tukiwa tumelala.
 
Back
Top Bottom