Wana JF mimi ni mwalimu in profession but kwa huu mshahara wa laki 4 nadhani kutoka ni ndoto.
Katika tasmini zangu nimegundua kilimo cha miti kinalipa sana na watu huku kwe2 wanao miliki misitu ndo matajiri wakubwa.
Kwa sasa nshapanda hekari 10 na Mungu akijaalia ntapanda zaidi kwa sababu inalipa tena kwa gharama ndogo kabisa.
Mfano: Ukinunua shamba la Hekari 1 = 100,000/= na ukapanda Miti aina ya Milingoti inaingia miti 1,000 kwa hekari 1, kila mche wa mti unauzwa Tsh 100 x 1,000 miche = 100,000/=. Wapandaji utawalipa Tsh 25,000/=
Jumla = Tsh 225,000/= kwa hekari moja.
Na kila mwaka uwe na kiasi kidogo cha kuwalipa watu wanaokuwekea fire line ama unaweza komaa mwenyewe.
Miti hiyo utaivuna baada ya miaka 10 Mungu akijaalia, ikiwa tayari miti ya nguzo za umeme na kila mti mmoja utauza Tsh 30,000/= mpaka Tsh 35,000/=
Kwa hiyo ukizidisha mara hiyo miti 1000 ya hekari moja utapata = Tsh 30,000,000/=.
Na kwa miti ya milingoti ina tabia ukivuna inachipua tena na tena maisha yako yote hutopanda tena ila ni kuiplun, kuweka fire line na kuvuna tu
Je ukiwa na heka zaidi ya moja utakuwa wapi baada ya hyo miaka?
Kijana mwenzangu changamka Miaka 10 sio mingi kama tunavyodhani.
Kama nawe mjasilia mali unaetaka fursa hii isikupite ntafute kwa namba 0769 877495.
Mkuu tuko pamoja,
Ni kijiji gani hicho nami nitie timu kaka, natafuta shamba la hivyo mkuu.
Mapanda kaka karibu
kuweni makini pipo wanapigwa sana huko..... utakuja lia!
Mapanda kijiji gani mkuu, au mapanda mtaa gani pale. Naifahamu Mapanda yote, kuanzia Kibengu,Igeleke,Chogo,Ukami,Kipanga,Uhafiwa,Ilogombe,Itimbo,Isipii,Kilosa mpaka masisiwe.
Igeleke kaka.
Teh teh! naona swali la mkuu Malila limemuingiza jamaa mitini.
Igeleke upande upi, upande wote wa kulia kama unakwenda Mapanda ni mali ya Sao Hill, na sasa hivi kuna tifu kubwa kt ya Sao Hill na The Highlands Forest, The Highlands Forest waliingia eneo la serikali kinyume na sheria, wenzao GRL waliingia ubia na Sao Hill ndio maana wako salama.
Mkono wa kushoto kama unakwenda Mapanda umejaa wote, labda pale ktk kilima cha Shule kabla hujafika kwenye shamba la Kabaka. Njia ya kwenda Ilogombe imejaa yote mpaka kule kwa Kalandulunyu kilimani juu kabisa. Kipande kilichobaki kinamilikiwa na familia moja hivi wagomvi sana. Huku upande wa kaskazini kuna msitu wa serikali wa kiasili, ng`ambo ya upande wa msituni kumejaa na kuna mawe sana. Pale bondeni wanapopiga tofali ni mali ya Dc mkuu, sasa ni kipande kipi unachosema wewe?
Biashara zipo nyingi tu ambazo waweza fanya bila kupigwa lakini hizi za miti acha kuwaingiza watu mkenge, naongea ukweliambao nimeona kwa macho yangu labda uhamie huko huko....! nd yale yale ya wakulima wa Mbozi, mtu anakopesha fedha na pembejeo kwa wakulima halafu wakati wa mazao kuvunwa wakulima wanatakiwa kulipa ile mikopo cha ajabu na kushangaza wanamua yule mtu anayewadai na aliyewakopesha kwa nia nzuri tu. Tuwe makini wapendwa mavuno ya miaka 10 si mchezo!By MalilaKupigwa ni sehemu ya mapambano na changamoto ambazo mpambanaji wa biashara yo yote hawezi kukwepa. Kupiga na kupigwa vinaenda sambamba,unachotakiwa kufanya ni kupunguza uwezekano wa kupigwa.Kwa bongo yetu ya sasa,ukiogopa kupigwa hutafanya kitu.
je waweza kunitajia biashara mojawapo ambayo waweza fanya bila kupigwa hapa Tz?
Biashara zipo nyingi tu ambazo waweza fanya bila kupigwa lakini hizi za miti acha kuwaingiza watu mkenge, naongea ukweliambao nimeona kwa macho yangu labda uhamie huko huko....! nd yale yale ya wakulima wa Mbozi, mtu anakopesha fedha na pembejeo kwa wakulima halafu wakati wa mazao kuvunwa wakulima wanatakiwa kulipa ile mikopo cha ajabu na kushangaza wanamua yule mtu anayewadai na aliyewakopesha kwa nia nzuri tu. Tuwe makini wapendwa mavuno ya miaka 10 si mchezo!
Acha kutisha watu, Miti sio mahindi wala maharage. Watu wanatoka kimaisha kikubwa ni uvumilivu. Lakini cha kuwamakini ni kuhakikisha shamba linakuwa lako sio la kukodi.Biashara zipo nyingi tu ambazo waweza fanya bila kupigwa lakini hizi za miti acha kuwaingiza watu mkenge, naongea ukweliambao nimeona kwa macho yangu labda uhamie huko huko....! nd yale yale ya wakulima wa Mbozi, mtu anakopesha fedha na pembejeo kwa wakulima halafu wakati wa mazao kuvunwa wakulima wanatakiwa kulipa ile mikopo cha ajabu na kushangaza wanamua yule mtu anayewadai na aliyewakopesha kwa nia nzuri tu. Tuwe makini wapendwa mavuno ya miaka 10 si mchezo!
Kaka naona unasoma stori za kwenye magazeti ama ni hadith ulisimuliwa, ardhi ipo ya kutosha, kuna kama Hekari 300 (zipo maeneo tofauti), kama upo tayari uje Mafinga nikakuonyeshe nauli ntakulipia ya kwenda na kurudi. Sio unaropoka uonekane na wewe unaijua Historia.
Mapanda kijiji gani mkuu, au mapanda mtaa gani pale. Naifahamu Mapanda yote, kuanzia Kibengu,Igeleke,Chogo,Ukami,Kipanga,Uhafiwa,Ilogombe,Itimbo,Isipii,Kilosa mpaka masisiwe.
Kaka ardhi ipo ya kutosha, kuna kama Hekari 300 (zipo maeneo tofauti), kama upo tayari uje Mafinga nikakuonyeshe nauli ntakulipia ya kwenda na kurudi.