Kilimo cha mirungi Kenya: Kenyatta atoa $10 million

Mavindozii

JF-Expert Member
Oct 20, 2012
2,111
2,779
Kenyatta atoa dola 10m za kilimo cha mirungi

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kwamba serikali yake itatenga dola za Kimarekani 10 milioni za kusaidia wakulima wa mirungi kwenye bajeti ya mwaka ujao wa kifedha.

Wakulima hao wameathirika sana kufuatia hatua ya baadhi ya nchi za Ulaya kupiga marufuku uuzaji wa mirungi, maarufu pia kama miraa, katika mataifa hayo.

Hutumiwa sana na watu wa jamii ya Wasomali na hutegemewa sana na jamii zianzoishi katika maeneo ya mashariki ya Mlima Kenya, miongoni mwa watu wa jamii ya Wameru.

Pesa hizo zitatolewa kupitia Wizara ya Kilimo.

Rais Kenyatta ametangaza hayo alipokuwa akitia saini mswada unaotambua mirungi kuwa mmea wa kuzalishia taifa mapato kuwa sheria.

Sheria hiyo itaifanya serikali kuweka mikakati ya kutangaza, kuzalisha na kusambaza na kuuza zao hilo.

Rais Kenyatta amesema kutaundwa pia jopo kazi la kuangazia changamoto zinazokabili sekta ya ukuzaji wa mirungi ambayo itatoa mapendekezo kwa serikali.
 
Mh!!! 10 million kwa ajili ya kilimo cha mirungi hahahahahaha!!! Mbona huyu mheshimiwa anazidi kutuharibia waume zetu???!!!!! Watalamu wa hichi kilimo cha mirungi watujuze vizuri kwa Tz itakuwaje
 
Sisi huku tunafunga mtu miaka 29 sijui kisa kakutwa na rumbesa ya gomba
 
sio mbaya kwani hata huku kwetu tunalima hivyo hatutaagiza kutoka huko bali watakua mshindani wetu
 
Hiii kitu ina halibu sana vijana wetu wa mashi,Arusha Na vijana wetu waliopo Magomeni,ilala Na kinondoni wana saga kama mbuzi
 
Back
Top Bottom