F Family_hammer Member Joined Jan 2, 2016 Posts 29 Reaction score 11 Oct 6, 2019 #1 Kitu ambacho kinafanya Mdalasin kuwa tofauti na mimea mingine zaidi ya kuwa kiungo bora pia utoa mafuta kutoka kwenye mizizi, gamba na majani, ambayo yana kemikali zinazotofautiana. HALI YA HEWA NA UDONGO Ubora wa Mdalasini utegemea udongo wenye rutuba na hali ya hewa nzuri. Mvua nyingi za kutosha 1,750-3,500 mm kwa mwaka. Udongo wenye rutuba na usioruhusu maji kutuama Joto kwa wingi Hewa yenye unyevunyevu KUSIA MBEGU KWENYE VITALU Mbegu hupatikana kwenye miti iliyokomaa Sia mbegu kwenye kitalu zikiwa nusu sentimeta chini ya udongo Baada ya kuchipua, mbegu huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kufikia umri wa kupandikiza shambani Panda miche wakati wa masika Panda kwa nafasi ya 2m x2m. Nafasi hizi huwezesha miti kutoa machipukizi mengi. Nafasi kubwa hufanya miti kuwa na matawi mengi pia mashina hayanenepi wala kurefuka. UTUNZAJI Acha machipukizi kwenye shina Toa matawi kwenye mashina ili kunenepesha mashina Weka shamba katika hali ya safi Zuia magonjwa kama.Vinundu (galls)wanaosababishwa na utitiri na wadudu scales na mealbugs kwa kutumia dawa za sumu kama Selecron, Karate nk. KUVUNA Mdalasini uanzwa kuvunwa baada ya miaka mitatu toka upandwe na uvunwa mara mbili kwa mwaka. Mazao ya mdalasini ni maganda ya mashina ya miti Kata shina la mti,na tenganisha maganda na mti kwa njia ya kumenya Kuwa mwangalifu ili ganda litoke vizuri bila kupasukapasuka Seli za nje ya ganda la mdalasini ni chungu hivyo ni vizuri ziondolewe kwa kukaruza kwa kisu Kausha vizuri siyo kwenye jua kali Mavuno 0.25 kg – 10kg maganda yaliyokaushwa kwa mti mmoja. Kiasi cha mazao hutegemea ukubwa na umri wa mti Ubora wa mdalasini hushuka kulingana na umri wa mti. Mti wa umri mkubwa hutoa mganda yenye ubora wa chini. MATUMIZI Mdalasini baada ya kukaushwa ikiwa umesagwa au bila kusagwa hutumika kama: Kiungo kwenye chakula na vitafunwa kama keki, mandazi,vitumbua Vikolezo kwenye vinjwaji km. chai, kahawa Dawa ya tumbo hasa wakati wa kuvimbiwa, kutoa hewa tumboni pia kuongeza hamu ya chakula Dawa ya ngozi Husaidia kutibu UTI Majani ya mdalasini uongeza radha kwenye chai. Kwa mahitaji ya miche ya mdalasini tuwasiliane kwa namba 0713629999, Bei ya mche ni shilingi 5000 tu.
Kitu ambacho kinafanya Mdalasin kuwa tofauti na mimea mingine zaidi ya kuwa kiungo bora pia utoa mafuta kutoka kwenye mizizi, gamba na majani, ambayo yana kemikali zinazotofautiana. HALI YA HEWA NA UDONGO Ubora wa Mdalasini utegemea udongo wenye rutuba na hali ya hewa nzuri. Mvua nyingi za kutosha 1,750-3,500 mm kwa mwaka. Udongo wenye rutuba na usioruhusu maji kutuama Joto kwa wingi Hewa yenye unyevunyevu KUSIA MBEGU KWENYE VITALU Mbegu hupatikana kwenye miti iliyokomaa Sia mbegu kwenye kitalu zikiwa nusu sentimeta chini ya udongo Baada ya kuchipua, mbegu huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kufikia umri wa kupandikiza shambani Panda miche wakati wa masika Panda kwa nafasi ya 2m x2m. Nafasi hizi huwezesha miti kutoa machipukizi mengi. Nafasi kubwa hufanya miti kuwa na matawi mengi pia mashina hayanenepi wala kurefuka. UTUNZAJI Acha machipukizi kwenye shina Toa matawi kwenye mashina ili kunenepesha mashina Weka shamba katika hali ya safi Zuia magonjwa kama.Vinundu (galls)wanaosababishwa na utitiri na wadudu scales na mealbugs kwa kutumia dawa za sumu kama Selecron, Karate nk. KUVUNA Mdalasini uanzwa kuvunwa baada ya miaka mitatu toka upandwe na uvunwa mara mbili kwa mwaka. Mazao ya mdalasini ni maganda ya mashina ya miti Kata shina la mti,na tenganisha maganda na mti kwa njia ya kumenya Kuwa mwangalifu ili ganda litoke vizuri bila kupasukapasuka Seli za nje ya ganda la mdalasini ni chungu hivyo ni vizuri ziondolewe kwa kukaruza kwa kisu Kausha vizuri siyo kwenye jua kali Mavuno 0.25 kg – 10kg maganda yaliyokaushwa kwa mti mmoja. Kiasi cha mazao hutegemea ukubwa na umri wa mti Ubora wa mdalasini hushuka kulingana na umri wa mti. Mti wa umri mkubwa hutoa mganda yenye ubora wa chini. MATUMIZI Mdalasini baada ya kukaushwa ikiwa umesagwa au bila kusagwa hutumika kama: Kiungo kwenye chakula na vitafunwa kama keki, mandazi,vitumbua Vikolezo kwenye vinjwaji km. chai, kahawa Dawa ya tumbo hasa wakati wa kuvimbiwa, kutoa hewa tumboni pia kuongeza hamu ya chakula Dawa ya ngozi Husaidia kutibu UTI Majani ya mdalasini uongeza radha kwenye chai. Kwa mahitaji ya miche ya mdalasini tuwasiliane kwa namba 0713629999, Bei ya mche ni shilingi 5000 tu.
bBusneM JF-Expert Member Joined Sep 10, 2019 Posts 288 Reaction score 590 Oct 18, 2019 #2 Ukivuna unauzia wapi? Soko lipo la kutosha?
kinywanyuku JF-Expert Member Joined Jul 13, 2015 Posts 3,849 Reaction score 3,065 Oct 20, 2019 #3 Mashamba yapo wapi
Smart911 Platinum Member Joined Jan 3, 2014 Posts 166,163 Reaction score 184,883 Oct 20, 2019 #4 Ahsante kwa elimu... Cc: mahondaw
Azizi Mussa JF-Expert Member Joined May 9, 2012 Posts 9,197 Reaction score 7,532 Dec 27, 2019 #5 Mbegu za kutosha kama kilo moja hivi zinapatikana wapi?
Baba Joseph17 JF-Expert Member Joined Jul 15, 2013 Posts 9,518 Reaction score 9,792 Dec 27, 2019 #6 Hujasems mikoa ipi inafaa kwa kilimo cha zao hilo
MLUGURU JF-Expert Member Joined Mar 30, 2012 Posts 3,002 Reaction score 3,882 Dec 30, 2019 #7 Hujasema ekari 1 inaingia miche mingapi?pia hujasema mche ikianza kuvuna unakaa kwa miaka mingapi mpaka kuacha kuvuna. Sent using Jamii Forums mobile app
Hujasema ekari 1 inaingia miche mingapi?pia hujasema mche ikianza kuvuna unakaa kwa miaka mingapi mpaka kuacha kuvuna. Sent using Jamii Forums mobile app
N Nehemia One Member Joined Jun 23, 2020 Posts 25 Reaction score 18 Apr 2, 2022 #8 Smart911 said: Ahsante kwa elimu... Cc: mahondaw Click to expand... Karibu Nehemia One Pvt Co Ltd upate miche ya mdalasini Call: +255699589177
Smart911 said: Ahsante kwa elimu... Cc: mahondaw Click to expand... Karibu Nehemia One Pvt Co Ltd upate miche ya mdalasini Call: +255699589177
N Nehemia One Member Joined Jun 23, 2020 Posts 25 Reaction score 18 Apr 2, 2022 #9 Azizi Mussa said: Mbegu za kutosha kama kilo moja hivi zinapatikana wapi? Click to expand... Kampuni ya Nehemia One Pvt Co Ltd unazalisha na kuuza miche Kwa wawekezaji wa KILIMO cha Mdalasini Kwa shs. 2600 Kwa mche. Call/ watssap +255699589177
Azizi Mussa said: Mbegu za kutosha kama kilo moja hivi zinapatikana wapi? Click to expand... Kampuni ya Nehemia One Pvt Co Ltd unazalisha na kuuza miche Kwa wawekezaji wa KILIMO cha Mdalasini Kwa shs. 2600 Kwa mche. Call/ watssap +255699589177