jsenyinah
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 249
- 339
Habarini za leo wandugu, ni matumaini yangu kwamba 'boxing day' imekwenda salama kabisa mkiwa na familia zenu.
Leo nimeamua kutiririka kuhusu agenda tajwa hapa juu, KILIMO BIASHARA. Tukitekeleza haya yafuatayo,tutaondokana na umaskini kwa kuwa na uhakika wa uzalishaji wa mazao ya kilimo yatakayotoshereza kwa matumizi ya nyumbani na kwa ajili ya biashara.
Bidhaa za kilimo namaanisha zile zitokanazo na MIFUGO,UVUVI na MAZAO (ya mboga mboga,matunda, nafaka).
MAZAO YA MBOGAMBOGA:
Hapa namaanisha mazao yanayochukua miezi 2 mpk 4 kuanzia kupanda mpk kuvuna.Mfano: Pilipili kali, pilipili mbuzi, nyanya,hoho, nyanya, bamia, biringanya, vitunguu (maji na saumu), cabbage, nyanya chungu/ngogwe nk.
Mazao haya n ya muda mfupi ambayo mtaji wake siyo mkubwa kwa kuanza na maeneo madogo.
MAMBO YA KUZINGATIA:
Lima kwa formula (kitaalam) zaidi. Hapa namaanisha kwamba,fahamu mambo yafuatayo kabla ya kuanza kilimo:-
1. Fahamu ukubwa wa eneo lako katika vipimo vya mita square.
Hii itakusaidia kujua idadi ya (kiwango cha) mbegu , kiwango cha mbolea, kiwango cha madawa, kiwango cha maji kinachotakiwa, kiasi halisi cha pesa utakachokuwa ukiwalipa vibarua wako na mwisho utaweza kukisia ni kwa kiasi gani utaweza kupata (production rate).
Vitu hivi vitakufanya ujue mtaji wako utatoshereza kwa kiasi gani.
2. Kuwa na soko la uhakika na zuri
Hii inategemeana na msimu unaolima na ubora wa mazao yako kwa mteja.
TATIZO la kukosekana kwa soko la uhakika hutokana na mkulima kulima kwa awamu awamu,na kwa kushuka na kupanda (kinyume na mahitaji ya mteja).
Mfano: Mtu anazalisha robo heka leo, msimu ujao halimi, msimu mwingine analima zao analojisikia yeye. Kwa namna hii unakuwa unamyumbisha mteja na ndo chanzo cha kutafuta dalali.
Tuwe na 'constant and continuous supply ' ili tuweze kumeet local & international markets kwa kufuaya Global Agricultural Practise (GAP).
Ukiweza kuzalisha continuously na quality products, mteja atakufuata popote ulipo na hapo ndipo utaweza kufaidika na kilimo.
3. Kilimo cha kutegemea mvua hakifai
Kila zao lina uhitaji wake wa maji (crop water requirement) ili liweze kukua na kuzaa vzr kulingana na hatua za ukuaji. Huu ndo umuhimu wa umwagiliaji.
Mvua yenyewe hunyesha bila kujali mmea unataka maji (kwa kiwango gani) au hautaki.Maji ya mvua yafaa kuvunwa, kutunzwa kwa ajili ya umwagiliaji.
4. Wakati wa kuweka dawa, mbolea, parizi lazima vizingatiwe.
Kwa leo inatosha.