Kilimanjaro waongoza kwa kutumia benki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimanjaro waongoza kwa kutumia benki

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by PayGod, Feb 9, 2011.

 1. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kilimanjaro waongoza kwa kutumia benki

  UTAFITI umebaini kwamba Mkoa wa Kilimanjaro, unaongoza kwa kutumia huduma za kibenki kwa asilimia kubwa na kuwa na idadi kubwa ya watu waoelewa na kudhubutu kuanzisha biashara mbalimbali.

  Kwa mujibu wa utafiti huo, Mkoa wa Kilimanjaro ni mkoa unaoongoza kwa kuwa na uelewa mkubwa katika Kanda ya Kaskazini kuhusiana na huduma za kifedha na kufuatiwa na Arusha, na Manyara.

  Hayo yalisemwa jana na mtafiti kutoka taasisi ya utafiti wa masuala ya uchumi na kijamii Tanzania (ESRF), Dora Semkwiji wakati akiwasilisha taarifa hiyo, katika warsha ya mahitaji na vikwazo vya kupata huduma za kifedha nchini.
  Semkwiji alisema wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro, wamekuwa na uelewa mkubwa katika masuala ya fedha kwa kuwa wanazingatia mafunzo na kutumia uzoefu walionao katika shughuli za kibiashara tangu wakiwa wadogo.

  Alisema taarifa hizo, zimepatikana baada ya ESRF kufanya utafiti katika kanda zote Tanzania na kubaini, uliopewa jina la Fin scope na kusisha sampuli ya watu 7,680 kuoanishwa na Idara ya Takwimu ya Taifa (NBS).

  Alisema utafiti huo, ulilenga zaidi katika upatikanaji na vikwazo kuhusu huduma za kibenki nchini na ni jinsi gani wananchi wana uelewa wa matumizi ya huduma za kibenki.

  Akiwasilisha taarifa hiyo, alisema Kanda ya Kaskazini inaongoza kwa kutumia huduma za kibenki kwa asilimia kubwa na kutumia mikopo kwa kiasi kikubwa zaidi.

  “Huu ni utafiti wa pili kufanyika na wa kwanza, ulifanyika mwaka 2006 na utafiti huu wa pili, umefanyika katika kanda nane za Tanzania na tunachokifanya sasa ni kutangaza matokeo katika kila kanda, kuhusiana na kile tulichobaini na wadau waweze kutoa maoni yao, baada ya hapo tunawakilisha matokeo kwa taasisi inayoshughulikia maboresho ya huduma za kifedha Tanzania (FSDT), ambao wametupa sisi jukumu hilo,”alisema Semkwiji.

  Alifafanua zaidi kuwa, Landa ya Lindi, inayoongoza kwa wananchi wake kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na matumizi ya huduma za kibenki.

  Warsha hiyo, iliwakutanisha wafanyakazi wa serikali ngazi ya mkoa na wilaya, taaisi mbalimbali zinazohusika na utafiti nchini na vyuo vya elimu ya juu kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Singida na Kilimanjaro.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidore Shirima alisema umefika wakati sasa mashirika mbalimbali na taasisi, kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali za kifedha.

  Alisema tafiti, zilizofanyika zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuisaidia serikali jinsi ya kusimamia mashirika ya kifedha na kuwafikia wananchi wote.
   
Loading...