Timu ya Soka ya Taifa ya Tanzania Bara ,Kilimanjaro Stars leo imeifunga timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars kwa goli 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru jijini. Pichani Mshamburiaji wa timu ya Kilimanjaro Stars Tomas Ulimwengu akiruka juu kukwepa daruga kutoka kwa mchezaji wa wa Harambee Stars Jamas Situma
Gaudence Mwaikimba wa Kilimanjaro Stars (kushoto) akiumiliki mpira huku akiangaliwa kwa makini na Osborne Monday
Baadhi ya mashabiki waliofurika uwanja wa Uhuru wakishuudia mchezo huo.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars wakishangilia goli lililofungwa na Gaudence Mwaikimba