Kilimanjaro: Kada wa CHADEMA atekwa na kuuawa kikatili

Daniel Mjema

Member
Jul 23, 2007
77
84
Kada wa CHADEMA katika Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, Anitha Swai, ameuawa na watu wasiojulikana na maiti yake kuokotwa eneo la TPC, umbali wa takribani kilometa 5 toka Moshi mjini, huku gari lake likipatikana limetelekezwa eneo la Bomambuzi

=========

Kada wa CHADEMA katika Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, Anitha Swai ameuawa katika tukio lililogubikwa na wingu zito.

Taarifa za awali zilizopatikana usiku huu zimedai kuwa Anitha ambaye aligombea ubunge wa viti maalum mwaka 2015, alitekwa nyara wilayani Rombo na kuuawa maeneo ya TPC nje kidogo ya mji wa Moshi.

Vyanzo mbalimbali vya habari vimedokeza kuwa mara ya mwisho mwanasiasa huyo alionekana akiwa na watu wawili wilayani Rombo siku ya Jumatatu, Februari 27 na kuaga wanaelekea Arusha.

Hata hivyo, tangu siku hiyo Anitha hakuonekana hadi maiti yake ilipogunduliwa leo (Alhamisi) jioni maeneo ya TPC huku gari lake likiwa limetelekezwa maeneo ya Bomambuzi mjini Moshi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kuokotwa kwa mwili huo, lakini amekataa kuthibitisha kama ni wa kada huyo wa CHADEMA.

"Ni kweli kuna tukio hilo, lakini ninachoweza kusema bado hajatambuliwa na mwili wake umepelekwa KCMC ili ndugu waweze kuutambua," amesema.

Hata hivyo, Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Mawenzi mjini Moshi, Hawa Mushi amethibitisha kuwa aliyeuawa ni kada wa chama chao, lakini chanzo na nani waliohusika hakijajulikana.

Hawa amesema taarifa zilizothibitishwa ni kuwa mwili wake ulipatikana maeneo ya TPC huku simu iliyopatikana katika gari yake ndiyo iliyosaidia kumtambua.

Chanzo: Mwananchi

R.I.P Dada yetu na Mwenyezi Mungu atawalipa waliyotoa uhai wako kwani kwa Mungu kila kitu kimehifadhiwa.
 
so sad!! Siasa za kiafrika ni ngumu kushughulika nazo
hakuna kitu wanadamu tuko assured kama Kifo kwani imeandikwa kila mtu ataionja kifo hivyo tuamini ameenda KUPUMZIKA tusitafute ameendaje tutakuwa Wazambi na wachonganishi. RIP -SHEMEJI
 
Kada wa Chadema katika Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, Anitha Swai ameuawa katika tukio lililogubikwa na wingu zito.

Taarifa za awali zilizopatikana usiku huu zimedai kuwa Anitha ambaye aligombea ubunge wa viti maalum mwaka 2015, alitekwa nyara wilayani Rombo na kuuawa maeneo ya TPC nje kidogo ya mji wa Moshi.

Vyanzo mbalimbali vya habari vimedokeza kuwa mara ya mwisho mwanasiasa huyo alionekana akiwa na watu wawili wilayani Rombo siku ya Jumatatu, Februari 27 na kuaga wanaelekea Arusha.

Hata hivyo, tangu siku hiyo Anitha hakuonekana hadi maiti yake ilipogunduliwa leo (Alhamisi) jioni maeneo ya TPC huku gari lake likiwa limetelekezwa maeneo ya Bomambuzi mjini Moshi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kuokotwa kwa mwili huo, lakini amekataa kuthibitisha kama ni wa kada huyo wa Chadema.

"Ni kweli kuna tukio hilo, lakini ninachoweza kusema bado hajatambuliwa na mwili wake umepelekwa KCMC ili ndugu waweze kuutambua," amesema.

Hata hivyo, Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Mawenzi mjini Moshi, Hawa Mushi amethibitisha kuwa aliyeuawa ni kada wa chama chao, lakini chanzo na nani waliohusika hakijajulikana.

Hawa amesema taarifa zilizothibitishwa ni kuwa mwili wake ulipatikana maeneo ya TPC huku simu iliyopatikana katika gari yake ndiyo iliyosaidia kumtambua.

Chanzo: Mwananchi
 
R.I.P Kamanda Umetangulia.

Mukipata Taarifa ya Chanzo cha Kifo Chake Tupeni Taarifa
Pole Kwa Family ya Marehemu.
 
Mhhhhhhh siasa hizi? Bora nibaki mwanaharakati wa fake ID pekee.
R.I.P Anitha
 
Usiogope mkuu si kila mauaji ni ya kisiasa.
Hata wachaga wakidhulumiana au kuchukuliana waume basi ni siasa jamani
 
Kada wa Chadema katika Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, Anitha Swai, ameuawa na watu wasiojulikana na maiti yake kuokotwa eneo la TPC, umbali wa takribani kilometa 5 toka Moshi mjini, huku gari lake likipatikana limetelekezwa eneo la Bomambuzi

Source:Mwananchi Online

Kada wa Chadema katika Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, Anitha Swai ameuawa katika tukio lililogubikwa na wingu zito.

Taarifa za awali zilizopatikana usiku huu zimedai kuwa Anitha ambaye aligombea ubunge wa viti maalum mwaka 2015, alitekwa nyara wilayani Rombo na kuuawa maeneo ya TPC nje kidogo ya mji wa Moshi.

Vyanzo mbalimbali vya habari vimedokeza kuwa mara ya mwisho mwanasiasa huyo alionekana akiwa na watu wawili wilayani Rombo siku ya Jumatatu, Februari 27 na kuaga wanaelekea Arusha.

Hata hivyo, tangu siku hiyo Anitha hakuonekana hadi maiti yake ilipogunduliwa leo (Alhamisi) jioni maeneo ya TPC huku gari lake likiwa limetelekezwa maeneo ya Bomambuzi mjini Moshi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kuokotwa kwa mwili huo, lakini amekataa kuthibitisha kama ni wa kada huyo wa Chadema.

"Ni kweli kuna tukio hilo, lakini ninachoweza kusema bado hajatambuliwa na mwili wake umepelekwa KCMC ili ndugu waweze kuutambua," amesema.

Hata hivyo, Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Mawenzi mjini Moshi, Hawa Mushi amethibitisha kuwa aliyeuawa ni kada wa chama chao, lakini chanzo na nani waliohusika hakijajulikana.

Hawa amesema taarifa zilizothibitishwa ni kuwa mwili wake ulipatikana maeneo ya TPC huku simu iliyopatikana katika gari yake ndiyo iliyosaidia kumtambua.

Chanzo: Mwananchi
Itakuwa wenyewe Ben wamempoteza na huyu tena
 
Back
Top Bottom