Kilimanjaro: Ajali mbaya ya Basi la Freys la Arusha-Tanga

Alexandry Nemesi

JF-Expert Member
Jun 7, 2014
1,499
579
Wakuu kumetokea ajali mbaya katika eneo la Maili sita,Mkoani Kilimanjaro Asubuhi na watu kadhaa wamefarika nakujeruhiwa ikihusisha Basi la Freys.

Basi la Frey's limepata ajali Kibosho Road Moshi. Wenye ndugu jamaa na marafiki ambao walikuwa wanasafiri na basi hilo muwajulie hali. Basi lililokuwa likisafirisha abiria kutoka Arusha kwenda Tanga.

Madereva tuwe MAKINI barabarani.
17352278_1549542941725639_6653176849963340605_n.jpg
17458066_1549542871725646_7850248660359867254_n.jpg
17498445_1549542725058994_6075620196039781018_n.jpg
17309390_1549542721725661_8938494791789558764_n.jpg
17426035_1549542701725663_158367553294789767_n.jpg
17361584_1549542705058996_778799209126751684_n.jpg

17342848_10208976293109030_4028657602152677199_n.jpg

Hapa wamefuta jina la basi ili lisipigwe picha. Hii tabia nashauri Polisi waikomeshe kwa sababu imekuwa ni kawaida kwa wenye magari kufuta nembo zao baada ya kupata ajali
 
Nadhani ni Frey's ya kutoka Tanga kwenda Singida. Naijua hio gari Slogan yao ni "Kristo Tumaini Letu",ina rangi nyeupe na bluu. Endelea kutupa taarifa
 
Weka picha,ajali imesababisha na nini,idadi ya majeruhi,walio kufa ili kuwa na uhakika zaidii,ongeza taarifa tafadhalii
 
Uwiiiiiiiiiiii, jamani! hayo mabasi ya kwenda Tanga! Kilimanjaro, ngoja nipige simu kwa ndugu na jamaa!!
 
Poleni wote mliopata ajali. Mwenyezi Mungu awajaalie mpate ahueni kwa haraka. Na wale wote walioondokewa na wapendwa wao, Mwenyezi Mungu awajaalie moyo wa subira na uvumilivu. Mwenyezi Mungu awapokee kwa huruma na upole Marehemu wote. TUMETOKA KWAKE NA KWAKE NDIO MAREJEO YETU WOTE.
 
Jamani basi ndo basi ninalopandaga kwenda Singida mara kwa mara duuuuu
Wapumzike kwa amani
 
Hatari sana. Pole nyingi kwa waliopatwa na matatizo hayo.Nipo naelekea Moshi na Bus la Simba mtoto..
 
Back
Top Bottom