Kilichotupishanisha watu weusi na wazungu (watu weupe) ni kutambua nini maana ya thamani ya muda..

Zionist

JF-Expert Member
Dec 5, 2017
1,830
2,882
Mzungu anathamini muda kuliko kitu chochote. Hata elimu yao imefupishwa sana.wote wanaoenda shule wanafundishwa kwa lugha ya nyumbani ( kama unaelewa utafahamu ni kwa sababu gani) mtoto anapoingia shule ya awali anaangaliwa kipaji, kisha kinakua recorded, kwa ajili ya future reference, kwa hiyo wakisha jua hilo, mwanafunzi anakua na miaka chini ya kumi yupo chuo kikuu kuanzia alipo maliza shule ya awali.

Hiyo yote ni ku cover muda ili kuendeleza kipaji kabla mtoto hajapevuka kuingia kwenye ulimwengu wa familia kwenye kukwazika na majukumu yatakayo poteza kipaji.

MAONI: tutathmini lugha ya kufundishia, tu detect vipawa vya watoto wetu wakiwa shule za awali, tukisha elewa hivyo vipawa aendelee navyo kwa masomo yahusiyo kipawa chake.

Wasomi wa lugha wabadilishe lugha ya vitabu kwenda kwenye lugha mama. Tufupishe miaka ya shule za msingi na sekondari.

Mungu awabariki.
 
Mkuu na sisi pia kuna tunaujali muda katika baadhi ya mambo, ulishawahi kupewa ahadi ya papuchi na demu mpya ukachelewa kweli?
 
Kuna tafsiri nyingi. Upande mwingine naona wazungu wanaendelea kwa kuwa wana tamaa (Greedy).

Sisi waafrika tulilidhika na maisha yetu ya nyumba za nyasi, wake wa 4, kashamba pembeni, hadithi jioni kutoka kwa wazee, hapo si fresh. Ndo maana mpaka sasa hivi, mkulima anaweza pata milioni 60, lakini bado anaishi kwenye nyumba ya ajabu.

Wazungu wana tamaa, kila anachopata anaona hakitoshi, anataka kingine, mpaka wakaona waje kuchukua na vyetu afrika, kitu kinachoendelea fanyika mpaka leo.

Kwa maisha ya sasa, yes muda sisi kwetu bado hatuuchukulii maanani kabisa. Pia kuridhika kwetu bado kuna tuponza. Ukipata kakazi cha mshahara hata laki 2 tu, tunaona maisha tumesha yapatia. Bata batani.
 
Umeongea Jambo kubwa ila kwa akili za viongozi waTz Ni ngumu Sana kufanyia kazi. Embu fikiria umoja wa Africa Mashariki umeruhusu kitu kinaitwa " free labour mobility" kwa watu was jumuiya hii. Ila kijana wa Form 4 Kenya anaruhusiwa kwenda chuo anakaa miaka mitatu anamaliza chuo. Anakuwa anamzidi mwaka mmoja kukaa mtaani kijana wa kitanzania walieanza nae shule mwaka mmoja. Sasa fikiria huyo mtoto wa kikenya hatakuja achukue nafasi ya kazi Tanzania huku huyo mtanzania akiwa Bado shule?
Tukitaka maendeleo zaidi ya wakenya na nchi za ukanda wetu tukubali kubadilisha mfumo wetu wa elimu
 
Mkuu, pengine sisi watu weusi tuna hekima zaidi, hizo mbio zote za kukimbizana na muda mwisho wake ni kaburini na hakuna utakachoenda nacho huko. Kwa msingi huo, tule bata tu,niko hapa PUB KIDIMBWI nagonga balimi zangu baridi taratibu, wala sina haraka.
 
Hapa kazini kwangu kuna mkorea mmoja. Hata simu tuu anayotumia kila kitu kipo ktk kikorea japo ni iphone.
 
Kuna tafsiri nyingi. Upande mwingine naona wazungu wanaendelea kwa kuwa wana tamaa (Greedy).

Sisi waafrika tulilidhika na maisha yetu ya nyumba za nyasi, wake wa 4, kashamba pembeni, hadithi jioni kutoka kwa wazee, hapo si fresh. Ndo maana mpaka sasa hivi, mkulima anaweza pata milioni 60, lakini bado anaishi kwenye nyumba ya ajabu.

Wazungu wana tamaa, kila anachopata anaona hakitoshi, anataka kingine, mpaka wakaona waje kuchukua na vyetu afrika, kitu kinachoendelea fanyika mpaka leo.

Kwa maisha ya sasa, yes muda sisi kwetu bado hatuuchukulii maanani kabisa. Pia kuridhika kwetu bado kuna tuponza. Ukipata kakazi cha mshahara hata laki 2 tu, tunaona maisha tumesha yapatia. Bata batani.
Nimekuelewa 100% , je tufanyeje ?
 
Naunga Mkono Hoja

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
Mungu Ibariki Morogoro
 
Mkuu uko sahihi kabisa, tatizo kubwa lipo kwenye definition yenyewe ya maisha na mafanikio.

Back
Top Bottom