Kilichotokea leo Monaco: Mcheza kwao utunzwa

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
21,084
56,506
Msilale bila kujikumbusha kwamba Charles Lecrec (Ferrari) mtoto wa miaka 26 kutoka Monaco, kashika namba 1 uwanja wa nyumbani, Circuit de Monaco kwa kutumia muda wa 2:23:15.554 (saa: dk : sekunde. mil second).

images (25).jpeg

Ni habari mbaya kwa Max the Mad Max the Super Max kwa kushika nafasi ya 6 ivyo kutoingia podium kabisa leo. Sio mbaya kwakua bado anaongoza ligi.

Madereva 10 waliochukua point leo ni kama hawa:

PS: Huyu Yuki anakuja aisee..

Screenshot_20240526-211722.png

Kwahiyo hadi sahivi, msimamo wa Ligi upo hivi:

Screenshot_20240526-212614.png

Leo mwanzoni kabisa madereva watatu walicrash kwahiyo hawakumaliza ata Lap 1. Ila wako salama.

Screenshot_20240526-212835.png

Haya tukutane Canada tar 9. Asanteni
 
Verstappen namkubali sana na ndio anayenifanya kuangalia hayo mashindano
 
Ila Lecrec ni mmoja kati ya wanaofanya vzr sana kwenye ligi kwahy kuwa hapo sio kwa bahati mbaya japokuwa bado amezidiwa na verstappen, Lewis Hamilton Ndio amejifia 😂
 
Mkuu, ungeelezea uhusiano kati ya msemo wa Mcheza kwao hutunzwa na ushindi wa kijana huyo.

Je, kuna upendeleo wowote ambao dogo kaupata kutokana na yeye kuwa ardhi ya nyumbani uliopelekea ushindi?
 
Moja kati ya circuit ya hovyo kabisa ku host mashindano ya f1 ni hii ya Monaco, Shindano linakosa ladha kwa maana circuit hairuhusu overtaking kwaio magari yanakuwa yanafatana tu mwanzo hadi mwisho wa shindano.. Ni upumbavu kutamaza mashindano ya magari ambapo eneo la kushindania haliruhusu gari la nyuma kulipita la mbele..
 
Hawa jamaa kuna mahala walikosea mkuu maana siku zinavyokwenda wanazidi kupotea na magari yao yanapata sana hitilafu.
Huu mchezo unaitaji zaidi ubora wa gari ndipo ubora wa dereva unapoonekana,.
Kuanzia mwak 2021 Red bull ndio anatengeneza gari bora zaid la mashindano ndio maana Max Verstapen amekuwa hakamatiki, kwaio madereva wengine wote wamekuwa wanaonekana wa kawaida kwa sababu mshindani wao amewazid kwenye ubora wa gari.
Vivo hivyo hata wakati kina Lewis Hamilton, Fernando Allonso, Michael Schumacher n.k walipokuwa wakitamba, kampuni zao ndio zilikuwa zikitengeneza gari bora za mashindano kwa wakati huo..
 
Kweli kabisa mkuu ubora ndio huketa matokeo bora ktk haya mashindano.
 
Mimi nikitumia MB zangu kufungua uzi alafu nisielewe kinachozungumzwa sikuwahi kukubali lazima na Mimi nikomenti hivyo hivyo .

Anyway kweli huyo jamaaa ni balaa sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom