Kilichomponza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hiki hapa

IPTL jinsi ulivyoiletea shida na kugonga siasa za nchi hii, ilikuwa si wakati wa kutafuta maoni ya wananchi kwa ajili ya kutaka kuongezea mkataba.
Lakini kaka Ghazwat, si ndio sheria inavyotaka? Au mharifu hana haki kisheria?
 
Ukishazidiwa Misuli ya fikra inabiDi utumie Misuli ya Mwili..
Hzi mambo za nDani sana, km hapakua na haja ya kuhtj Maoni ya wananchi, si Ilikua issue ya kumuita Jamaa pembeni na Kumtonya
Ama alikua Alerted tayari Halafu aka"violate" His master's say??.
But in generally kuna vitu vya nDani sana pengine Havijawekwa wazi
 
Leseni anatoa nani? Mkataba kasaini na nani? Leseni anatoa Ewura(mfano), mkataba kasaini na Tanesco (serikali). Ukipewa mkataba kutafuta leseni ni kazi yako, ukishindwa kupata leseni utashindwa kutimiza mkataba maanake unevunja mkataba.

Ewura akimnyima leseni IPTL automatically IPTL atashindwa kufanya kazi yaani kutimiza mkataba na serikali hivyo shughuli yake imeisha na ndio serikali inachokitaka.

Ni mawazo yangu finyu tu.
 
Hizi kiki za kisinema sinema! kwa staili hii ntaachaje kumuamini Mange Kimambi ... kwa utabiri wake katika hili ... jamani nchi haijengwi kwa kiki tunapotea sasa ...
 
Ndio Upoyoyo wenyewe wa hao Wakurugenzi yaani lesen ya kuzalisha umeme imeisha, na mkataba wa kuuza umeme bado sasa hapo imagine huo umeme watautoa wapi,na hapohapo kwenye mkataba wa Tanesco wameweka kipengele kwamba wazalishe au wasizalishe Tanesco iwalipe, Upumbavu mtupu ndio maana Mr Presidaa anapata kichefuchefu na baadhi ya viongozi aliowakuta
 
Ndio wakome sasa....IPTL ilitajwa kama adui kwa taifa lakini bado wanajipendekeza nayo...timua kabisa hao...big up PM
 
IPTL jinsi ulivyoiletea shida na kugonga siasa za nchi hii, ilikuwa si wakati wa kutafuta maoni ya wananchi kwa ajili ya kutaka kuongezea mkataba.
Sheria inaitaka nini kifanyike na EWURA na je alifuata sheria au hakufuata? Pili hau wadau ni akina nani ambao sheria inataka kupata maoni kutoka kwao?
 
Nadhani kuutaarifu umma walikuwa wanatekeleza hitaji la kisheria pengine. Ni obvious hakuna mwananchi angesema iptl wapewe leseni. Halafu huu utumbuaji wa usiku usiku huu, yaani utadhani hapatokucha vile.
Inaonyesha serikali yetu ilivyomakini na kupiga kazi
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi.

Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ambayo imesainiwa na Mkurugenzi wake, Gerson Msigwa inaeleza kuwa Ngamlagosi amesimamishwa kazi kuanzia Juni 11, 2017.

Kilichomponza ni hiki. Mwishoni mwa wiki iliyomalizika Mamlaka hiyo ilitoa tangazo katika vyombo vya habari kwa umma kwamba Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imepokea maombi ya kuongeza muda wa leseni ya kuzalisha umeme kutoka kwa kampuni ya uzalishaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) "Mwombaji".

Hivyo basi, EWURA ina uarifu umma na wadau mbalimbali kwa ujumla kuwasilisha maoni au pingamizi ili kufanikisha uchambuzi mzuri wa maombi haya.

Taarifa ilitolewa chini ya kifungu cha 19 cha sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, sura ya 414 ya sheria za Tanzania na kifungu cha 8 cha sheria ya umeme, sura ya 131 ya sheria za Tanzania.

Tayari wadadisi wa mambo wanahusisha kusimamishwa kazi huko kunatokana na tangazo hilo la kutafuta maoni ya wananchi ya kutaka kumuongezea mkataba IPTL.

Itakumbukwa kuwa Januari Mosi mwaka huu Rais Dkt. John Magufuli, alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, katika hali inayoonesha kuwa Rais amekerwa na jaribio la (TANESCO) bei ya umeme.

Baada ya Mramba kutenguliwa nafasi yake alipewa Dk. Tito Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa (TANESCO) akimtoa chuo kikuu cha Dar es salaam alikokuwa akifundisha.

Rais Magufuli, alichukua hatua hiyo siku mbili baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuiidhinisha ongezeko la asilimia 8.5 ya bei ya huduma za umeme kwa kilichoelezwa kuwa lengo ni kukidhi gharama za uzalishaji wa umeme.
Sijakuelewa mkuu hujaeleza sababu nn hasa tatizo lililomtoa boss huyo wa Ewura kibaruani, au ana harufu ya Ukawa....
 
Sasa, najiuliza jambo dogo ila kubwa sana,,,, tutafahamuje kuwa atakayepewa mkataba Mpya hana mkono wa IPTL!?

Singasinga uchwara atakubali kutolewa kwenye mrija wa maji ya bahari kirahisi kiivyo!?

Nawaza kwa sauti, ili akina "The bold, Beautiful Nkosazana, Infetry soldier, De delivis, Nifah. Sooth na wengine wote mlifikishe mahala salama ili mchakato wa tender usimamiwe na mikono salama (Just kidding guys by mentioning your IDs :):):D:D).
 
Sijakuelewa mkuu hujaeleza sababu nn hasa tatizo lililomtoa boss huyo wa Ewura kibaruani, au ana harufu ya Ukawa....


Soma aya ya tatu ya utaelewa.

Acha kukimbia Kama Jogoo, ampandapo Tetea.

Kama wewe, ni "Operation kimbunga' au Vyeti Feki' ama ni Incomplete Certificates" basi huwezi ukaelewa.

Tatizo ni kuwa IPTL , wameishitaki serikali na tunawalipa billions of dollars then, Mkurungezi anathubutuje, kupokea tenda ya singasinga anayetuibia!?

Kama na hapo hujaelewa basi Soma vizuri aya ya tatu ya comment yangu utaelewa vizuri.
 
Leseni anatoa nani? Mkataba kasaini na nani? Leseni anatoa Ewura(mfano), mkataba kasaini na Tanesco (serikali). Ukipewa mkataba kutafuta leseni ni kazi yako, ukishindwa kupata leseni utashindwa kutimiza mkataba maanake unevunja mkataba.

Ewura akimnyima leseni IPTL automatically IPTL atashindwa kufanya kazi yaani kutimiza mkataba na serikali hivyo shughuli yake imeisha na ndio serikali inachokitaka.

Ni mawazo yangu finyu tu.


Na hapo, kuna kitu serikali bado itakifanya ambacho kila mtu ataiinulia mikono serikali ya JPM .

Na IPTL pamoja na singasinga hawatakaa wakisahau milele amina!!!

Kikikaribia nitakuja kuleta mrejesho.
 
kinachoisha July ni leseni ya kuzalisha umeme, mkataba wa mauziano unaisha 2022

Sasa hiyo, moja Kwa moja ni kuwa kama hauna lesseni ya kuzalisha maana yake hauna utakachouuza.

If you don't produce automatically you will sell / or supply nothing!!

Hapo , ni sawa na kuwa na tiketi ya bombadier, ila wewe abiria uko feri unangojea kupanda bombadier.
Safari hiyo, automatically itakuwa haipo.

Kwa kifupi, IPTL na singasinga ndiyo kwa kheri kwenye ramani za Biashara hapo Tanzania na mkono wa chuma cha mjerumani utawakamata wote waliotuweka kwenye hasara hii.

Dawa, zinachemka!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom