Lawkeys umepotea sana ndugu yangu.. nafikiri hilo japo sio rasmi lakini lina harufu ya ukweli maana mabenki yetu bwana ni tatizo tu, wako kibiashara zaidi na sio kuisaidia nchi kuimarika kiuchumi.Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tz Tsh. 1850 ilinunua 1 USD, hii ilikuwa mwaka jana tu! Lakini wiki hii Tsh 1598 imenunua 1 USD. Kwa haraka ninaona kwamba Tsh imepata awheni haraka kuliko ilivyotarajiwa na wengi.
Nimepata taarifa zisizo rasmi (heresay) kwamba mabadiriko haya ya haraka yametokana na utafiti uliofanywa na BOT uliogundua kwamba mfumo wa malipo ya import ya mafuta uliokuwepo ndio umechangia kwa kiasi kikubwa. Mfumo uliokuwepo awali ulikuwa ni kwa Commercial banks kutumika kulipia imports za mafuta nao walikuwa waki hike rates ili kujipatia faida kubwa.
Lakini sasa malipo yote yanafanywa kupitia BOT hivyo hakuna tena nafasi ya kufisadi. Inasemakana kwamba tangu kubalishwa kwa mfumo ndio TSH imeendele kufanya vizuri.
Wanaoujua ukweli wa jambo hili bonyezeni botton.
Sidhani kama hiyo ni sababu maana kilichofanyika hakijawahi kutokea Tanzania eti shilingi kutengamaa kwa zaidi ya sh 200 dhidi ya dollar..! hilo usemalo wewe ni zile fluctuations za 20-50 shillingsImports huwa zinapungua wiki au siku chache kuelekea mwisho wa mwaka (kama inavyotokea karibia na bajeti ya serikali). Kwa maana hiyo demand ya US Dollars inapungua kulinganisha na supply yake na hivyo exchange rate kuwa favourable kwa local currency.
...Hii inaweza kuwa sababu ya maana zaidi -kuelezea kwanini thamani imepanda baada ya kushuka kwa kasi- kwani siku zote mafuta yalikuwa yakiagizwa na hatukuona trend ile ya mwishoni mwa mwaka. Uwezekano wa speculation -hasa pale ilipotoka 1800 hadi 2000- ni mkubwa zaidi.Imports huwa zinapungua wiki au siku chache kuelekea mwisho wa mwaka (kama inavyotokea karibia na bajeti ya serikali). Kwa maana hiyo demand ya US Dollars inapungua kulinganisha na supply yake na hivyo exchange rate kuwa favourable kwa local currency.
Nilipenda sana niwe mchumi, ila du Dr. Kalamage alinifanya nikimbie!
Mkuu uko nyuma kidogo,Ndullu alishasema mwaka juzi hatuna akiba ya dhahabu=(wajanja kushauza) na sasa tunaweka akiba in euro na dolari,hili lilizua tafrani bungeni wakitaka kujua dhahabu yote iliyonunuliwa na BOT late 80 early 90's zilienda wapi ??Tanzania ilibidi ijikwamue kwa kuuza akiba ya dhahabu zake benki ya dunia baada ya kuona hali ni ya hatari, kisiasa na kiuchumi, hilo la imports kupungua mwisho wa mwaka ilikuwa zamani kwa sasa huongezeka maana migodi haifungwi mkaburu hana likizo, waenda china, dubai kama kawaida tena wanabebana na bidhaa huwa nyingi kipindi hicho. Nawasilisha
Vile vitu vilivyopanda bei kwa kisingizo kwamba Tshs ipo weak kwa sasa vimepunguzwa bei? - kwangu mimi sioni tofauti. Actually mabadiliko haya yananiumiza sana. Kwa sasa natumia pesa nyingi zaidi kwa huduma zile zile kuliko miezi michache hapo nyuma (wakati dollar ipo juu)
mi'naona kama hamna kilicho wahi pungua bei hapa tz toka kipandeVile vitu vilivyopanda bei kwa kisingizo kwamba Tshs ipo weak kwa sasa vimepunguzwa bei? - kwangu mimi sioni tofauti. Actually mabadiliko haya yananiumiza sana. Kwa sasa natumia pesa nyingi zaidi kwa huduma zile zile kuliko miezi michache hapo nyuma (wakati dollar ipo juu)