Kilichobadilika Tanzania kwa sasa

Kilichobadilika Tanzania kwa sasa

6By6 Miguno

Member
Joined
Apr 20, 2025
Posts
75
Reaction score
107
Miaka michache nyuma tuliogopa sana kifo, Ni dhahiri kuna wenzangu na mimi ambao tulikuwa hatuna hata ujasiri wa kushuhudia maiti kwa macho.

Uongozi huu umefanikiwa kutubadili kwenye roho, Kutoka uzuri hadi ubaya, woga hadi ujasiri.

Nakiri kusema kwamba kufika hivi sasa tumekuwa majasiri sana kutokana na tuliyoshuhudia, Hakuna tena tukio la kifo lenye kutosha kufanya tupate mshtuko.

Tumeshuhudia risasi ikitua mwilini kwa mtu na damu ikiambaa kwenye sura ya ardhi… Sauti za mabomu na risasi tushazoea, Na kweli tumeelewa kuwa ukisikia Pah ujue haijakupata hivyo wakati ujao hatutolala chini tena kwani tutajua imetukosa hivyo tutasonga mbele.

Tunashukuru sana uongozi huu kwa hilo, Lakini ujasiri huu tuliopata nawasihi viongozi wote mnaochochea hasira za wananchi wenu mjue kujilinda na isiwepo siku akatokea yoyote kati yenu akajichanganya na kuingia mikono ya wananchi hawa mliowatoa ubinadamu kwani unyama ambao utasuuza nyoyo zao pengine labda kula nyama yako.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom