Haipingiki: Hii ndio Top 10 ya binadamu wanaochukiwa zaidi Tanzania kwa sasa

Louis II

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Messages
2,683
Points
2,000

Louis II

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2018
2,683 2,000
Angalizo: Huu ni utafiti (usio rasmi) nilioufanya kwa muda mrefu kutoka katika jamii inayonizunguka na kwa kiasi kikubwa kutoka katika mitandao ya kijamii ikiwemo hii JamiiForums.

Kwanza, Mtu ili apendwe yampasa afanye mambo yanayoipendeza jamii, awe na upendo kwa wengine, asiwe na ubaguzi wa aina yoyote, afuate sheria na taratibu zilizowekwa (Katiba husika), na mwisho kabisa aepuke "kujimwambafai". Mtu akifanya kinyume na hayo, jamii humchukia na kumpuuza kwani anakuwa amevunja miiko na utaratibu wa jamii yake hivyo, watu watapunguza mapenzi kwake.

Kwa hapa kwetu Bongo kuna watu wametokea kuchukiwa sana kutokana na matendo yao yanayotia mashaka na yanayokarahisha kundi kubwa la jamii ya watu wa bongo. Hawa watu ni wababe, ni wabaguzi, ni waonevu, na mbaya zaidi wamejimwambafai (Kwa sauti ya upole ya Mzee JK) kwa sababu ya nafasi na hadhi zao katika jamii zao. List yenyewe ni hii ifuatayo:-

(10). RPC Mambosasa: huyu ni kamanda wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam. Huyu udhaifu wake ni kushindwa kufanya kazi kisheria na kusimamia haki ipasavyo. Double standards zimeharibu mvuto wake katika jamii, kwani nani amesahau yale madudu yaliyotokea hadi binti Akwelina akauliwa hadharani na askari wa jeshi la polisi na ushahidi ukakosekana katika mazingira yaliyoonekana kuwa ni planned? Kuanzia pale Watu walipoteza imani na utendaji kazi wake.

(9). Mwigulu Nchemba:- huyu aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi. Ni katika kipindi chake mambo mengi ya uhalifu na uonevu yalitamalaki. Watu walitekwa, walibambikiziwa kesi na wengine waliuawa na kutupwa mitoni na baharini. Ni wakati wa uongozi wake ambapo binti Akwelina alikufa kifo cha kinyama kwa kupigwa risasi na askari polisi ambao wapo chini ya wizara yake. Chakushangaza bwana huyu alikaa kimya na waliopaza sauti aliwakejeli waziwazi akitetea uovu unaondelea ila mwishowe alitumbuliwa kwa aibu. Nani atakupenda kwa hali hii?

(8). David Lusinde A.K.A Kibajaji:- kama sijakosea huyu ni mbunge wa Mtera (CCM). Huyu bwana mkubwa analiaibisha Bunge kwani hoja zake "tata" zinatia mashaka juu ya uimara na umakini wa wawakilishi wa wananchi bungeni hasa hawa wa CCM. Huyu ni mzee wa porojo, mipasho, ubaguzi na kejeli kwa wenzake hasa wa upande wa upinzani hata kwenye hoja za msingi zenye kujenga yeye huchomekea mipasho na kejeli zake. Watu Werevu hawawezi kumkubali huyu jamaa.

(7). William Malecela (LeMutuz):- Kwakweli huyu mzeekijana hapendwi na watu wengi. Mambo anayofanya kwa umri wake yanatia mashaka juu ya uimara wa fikra zake. Kwanza ni mzee wa vitoto (hiyo sio ishu sana), mbaya zaidi anapenda show offs za kitoto. Siku hizi naye amegeuka kuwa spika ya Lumumba na kijana wake Makonda. Ni mbishi sana na anatetea hata mambo ya hovyo ilimradi tu atete tumbo lake. Tembelea kurasa za huyu bwana na utayaona yote haya.

(6). Jerry Muro:- Mkuu wa Wilaya ya Arumeru hahaha!...this guy is something else! Jamaa anapenda sifa sana na ana dharau zilizopitiliza hata kwa waliompita umri. Kila anachofanya bwana Jerry, watu (hasa wa mitandaoni) wanakipinga vibaya mno kwani mambo yake mengi anayofanya hayaakisi weledi na cheo chake cha ukuu wa wilaya. Ni mbaguzi sana, hana staha, ana majivuno na anapenda kujimwambafai bila sababu ya msingi.

(6). Alex Mnyeti:- RC wa Manyara mwenye kauli tata zenye kuleta mgawanyiko katika jamii. Huyu bwana hana mshipa wa aibu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚(nadhani wale wenzangu na mimi mshanielewa).

(4). Ally Happy :- Kijana huyu aliutwaa uaRC wa Iringa kimasihara baada ya kufanya vitimbi/vimbwangwa vingi pale Kinondoni. Huyu jamaa ni gwiji wa sifa na ufahari usio na maana. Ana chuki za waziwazi kwa kundi fulani la watu na huzionesha chuki zake waziwazi bila uficho. Amelewa madaraka!!!

(2). Cyprian Musiba:-.kwanini akosekane huyu bwana? Huyu amechafua hali ya hewa vibaya sana maana mpaka Vigogo hawajui itokako nguvu ya huyu bwana. Huyu jamaa hana aibu, haogopi na ana moyo mgumu (roho mbaya) kwa ameongoza katika kuwachafua watu kwa mgongo wa uwanaharakati wa kumtetea rais. In short hii ni spika ya redio iliyojificha mahali fulani. Anachukiwa mno!!

(1). Paul Makonda:- πŸ˜‚πŸ˜‚Ladies and Gentlemen namtambulisha kwenu kinara wa listi hii bwa Paulo. Huyu hastahili kuelezewa sana maana aliyofanya na anayoendelea kufanya yanatia mashaka juu ya uhusiano wake na Mheshimiwa sana. Kiufupi Paulo hupendwi ndugu yangu au pengine watu wanakuonea wivu? Mimi sijui kwakweli!

Nimalizie kwa kuwashauri hawa watu kuwa bado nafasi wanayo, Watanzania ni wasahaulifu na wasamehefu. Wakifanya mema watapewa thamani na kupendwa kama wengine.

NB: JF is where we dare to talk openly. Let's be open.
 
Root

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
34,738
Points
2,000

Root

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2012
34,738 2,000
Wakuchukiwa ni CCM maana bila wao hao watu wana akili nzuri. Kwani huoni wanaotoka upinzani kwenda huko wanaiuwa na ujeuri na kusahau yote waliyotendewa na CCM
 
mandella

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2011
Messages
2,905
Points
2,000

mandella

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2011
2,905 2,000
Angalizo: Huu ni utafiti (usio rasmi) nilioufanya kwa muda mrefu kutoka katika jamii inayonizunguka na kwa kiasi kikubwa kutoka katika mitandao ya kijamii ikiwemo hii JamiiForums.

Kwanza, Mtu ili apendwe yampasa afanye mambo yanayoipendeza jamii, awe na upendo kwa wengine, asiwe na ubaguzi wa aina yoyote, afuate sheria na taratibu zilizowekwa (Katiba husika), na mwisho kabisa aepuke "kujimwambafai". Mtu akifanya kinyume na hayo, jamii humchukia na kumpuuza kwani anakuwa amevunja miiko na utaratibu wa jamii yake hivyo, watu watapunguza mapenzi kwake.

Kwa hapa kwetu Bongo kuna watu wametokea kuchukiwa sana kutokana na matendo yao yanayotia mashaka na yanayokarahisha kundi kubwa la jamii ya watu wa bongo. Hawa watu ni wababe, ni wabaguzi, ni waonevu, na mbaya zaidi wamejimwambafai (Kwa sauti ya upole ya Mzee JK) kwa sababu ya nafasi na hadhi zao katika jamii zao. List yenyewe ni hii ifuatayo:-

(10). RPC Mambosasa: huyu ni kamanda wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam. Huyu udhaifu wake ni kushindwa kufanya kazi kisheria na kusimamia haki ipasavyo. Double standards zimeharibu mvuto wake katika jamii, kwani nani amesahau yale madudu yaliyotokea hadi binti Akwelina akauliwa hadharani na askari wa jeshi la polisi na ushahidi ukakosekana katika mazingira yaliyoonekana kuwa ni planned? Kuanzia pale Watu walipoteza imani na utendaji kazi wake.

(9). Mwigulu Nchemba:- huyu aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi. Ni katika kipindi chake mambo mengi ya uhalifu na uonevu yalitamalaki. Watu walitekwa, walibambikiziwa kesi na wengine waliuawa na kutupwa mitoni na baharini. Ni wakati wa uongozi wake ambapo binti Akwelina alikufa kifo cha kinyama kwa kupigwa risasi na askari polisi ambao wapo chini ya wizara yake. Chakushangaza bwana huyu alikaa kimya na waliopaza sauti aliwakejeli waziwazi akitetea uovu unaondelea ila mwishowe alitumbuliwa kwa aibu. Nani atakupenda kwa hali hii?

(8). David Lusinde A.K.A Kibajaji:- kama sijakosea huyu ni mbunge wa Mtera (CCM). Huyu bwana mkubwa analiaibisha Bunge kwani hoja zake "tata" zinatia mashaka juu ya uimara na umakini wa wawakilishi wa wananchi bungeni hasa hawa wa CCM. Huyu ni mzee wa porojo, mipasho, ubaguzi na kejeli kwa wenzake hasa wa upande wa upinzani hata kwenye hoja za msingi zenye kujenga yeye huchomekea mipasho na kejeli zake. Watu Werevu hawawezi kumkubali huyu jamaa.

(7). William Malecela (LeMutuz):- Kwakweli huyu mzeekijana hapendwi na watu wengi. Mambo anayofanya kwa umri wake yanatia mashaka juu ya uimara wa fikra zake. Kwanza ni mzee wa vitoto (hiyo sio ishu sana), mbaya zaidi anapenda show offs za kitoto. Siku hizi naye amegeuka kuwa spika ya Lumumba na kijana wake Makonda. Ni mbishi sana na anatetea hata mambo ya hovyo ilimradi tu atete tumbo lake. Tembelea kurasa za huyu bwana na utayaona yote haya.

(6). Jerry Muro:- Mkuu wa Wilaya ya Arumeru hahaha!...this guy is something else! Jamaa anapenda sifa sana na ana dharau zilizopitiliza hata kwa waliompita umri. Kila anachofanya bwana Jerry, watu (hasa wa mitandaoni) wanakipinga vibaya mno kwani mambo yake mengi anayofanya hayaakisi weledi na cheo chake cha ukuu wa wilaya. Ni mbaguzi sana, hana staha, ana majivuno na anapenda kujimwambafai bila sababu ya msingi.

(6). Alex Mnyeti:- RC wa Manyara mwenye kauli tata zenye kuleta mgawanyiko katika jamii. Huyu bwana hana mshipa wa aibu (nadhani wale wenzangu na mimi mshanielewa).

(4). Ally Happy :- Kijana huyu aliutwaa uaRC wa Iringa kimasihara baada ya kufanya vitimbi/vimbwangwa vingi pale Kinondoni. Huyu jamaa ni gwiji wa sifa na ufahari usio na maana. Ana chuki za waziwazi kwa kundi fulani la watu na huzionesha chuki zake waziwazi bila uficho. Amelewa madaraka!!!

(2). Cyprian Musiba:-.kwanini akosekane huyu bwana? Huyu amechafua hali ya hewa vibaya sana maana mpaka Vigogo hawajui itokako nguvu ya huyu bwana. Huyu jamaa hana aibu, haogopi na ana moyo mgumu (roho mbaya) kwa ameongoza katika kuwachafua watu kwa mgongo wa uwanaharakati wa kumtetea rais. In short hii ni spika ya redio iliyojificha mahali fulani. Anachukiwa mno!!

(1). Paul Makonda:- Ladies and Gentlemen namtambulisha kwenu kinara wa listi hii bwa Paulo. Huyu hastahili kuelezewa sana maana aliyofanya na anayoendelea kufanya yanatia mashaka juu ya uhusiano wake na Mheshimiwa sana. Kiufupi Paulo hupendwi ndugu yangu au pengine watu wanakuonea wivu? Mimi sijui kwakweli!

Nimalizie kwa kuwashauri hawa watu kuwa bado nafasi wanayo, Watanzania ni wasahaulifu na wasamehefu. Wakifanya mema watapewa thamani na kupendwa kama wengine.

NB: JF is where we dare to talk openly. Let's be open.
Yaani nilikua natafuta wa kwanza ... Usingemuweka yeye top one basi list ingikua batili
 
Forum statistics

Threads 1,379,052
Members 525,304
Posts 33,733,325
Top