Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,436
- 5,229
Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Bw. Geofrey Kiliba, amesema kuwa wadhifa wake ndani ya jumuiya hiyo haumzuii kutoa pongezi kwa viongozi wa serikali wanaotekeleza wajibu wao ipasavyo kwa manufaa ya wananchi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kiliba alisisitiza kuwa TAHLISO haijajikita kumpigia chapuo Rais Samia Suluhu Hassan, bali maoni yake ni ya utashi binafsi kufuatia mafanikio makubwa ambayo Rais Samia ameyatekeleza tangu aingie madarakani.
“Wapo wanaomtazama Rais Samia kwa mitazamo mbalimbali – kama Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, au kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi. Mimi namzungumzia kama Rais wa nchi yangu, na mimi ni sehemu ya wananchi wake,” alisema Kiliba.